Swali kwa Mwakinyo: Je, ulizuiliwa kununua viatu huko Uingereza?

Swali kwa Mwakinyo: Je, ulizuiliwa kununua viatu huko Uingereza?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Maandiko matakatifu yanasema "Mpumbavu huamini kila neno bali mwenye hekima huchunguza sana".
Haya Mwakinyo nijibu haya maswali;

1. Ulizuiliwa kununua viatu huko Uingereza?

2. Promoter wako hakuweza kufanya mchakato wa kukutafutia vifaa kazi baada ya kupoteza vifaa vyako?

3. Hivyo viatu ambavyo havijakufiti ulivigundua kuwa unfit baada au kabla ya kuvivaa?

4. Kulikuwa na shuruti katika kuvaa hivyo viatu?

5. Ulipewa viatu na hao wenyeji wako kwa kuzingatia order yako? yaani ulitaja size au ulitupiwa tu kama mgao wa jeshi?
 
Huyu jamaa anafanya niamini ameuza game, kwamba hajui size za viatu vyake, pia viatu alivalia ulingoni au kabla ya kuingia ulingoni.
 
Jamaa kavuta mkwanja wake akajisemea yanini mie 😂
 
mzamini wake ni sportpesa na ili limefanywa makusudi !
 
Ndiyo hatari ya kuyaruhusu makampuni ya betting kuingia katika ufadhili wa michezo. Nchi hizi ambazo utawala wa sheria bado una walakini na watu hawana maadili tutapata shida saaana.

Bado match fixing katika ligi haijakolea.
 
Back
Top Bottom