Swali kwa Rais Samia: Tukope nje Trilioni 1 kwa masharti au tudhibiti wizi wa Trilioni 2 kodi za Watanzania?

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Kiukweli pamoja na kazi nzuri anazofanya Mh Rais Dr Samia Suluhu Hassan pamoja na watumishi wema na wanaomshauri vizuri juu ya ustawi wa Taida letu la Tamzania ni vizuri tuliangalie na hili.

Mpaka sasa yayumukinika kuwa Wizi na upotevu wa pesa za umma zinazoishia mikononi mwa watu wachache hasa wenye nguvu na madaraka serikalini ni nyingi Takribani Trilioni 2.

Inasikitisha kwamba unamkamua mwananchi kwa Tozo na kodi mbali mbali mwenye kipato kidogo kwa gia la kujenga Nchi kumbe hizo hela zinaenda kujenga uchumi wa watu wachache.

Kwamba Natuma pesa elfu 10 kijijini kwa bibi yangu serikali ina ikata sh 500.
Tunajikusanya watanzania milioni 5 tunachangia bilioni 1 zinazoenda kuliwa na watu wawili au watatu tu.

Kama kweli serikali ya Rais Samia imejizatitikupambania wananchi ili tazame na hili.

Ipo siku hata hao wanaotukopesha pesa za maendeleo watatuchoka.

Inakuwa kama Taifa Rais anatoka nje kwenda kutafuta vijisentikutuletea wanawe atujengee shule na hospitali harafu kundi la watu wachache wanazitapanya?

Hao wanaotukopesha Tril 1, then tunaiba Tril 2 naona wakiendelea kutupa hizo hela basi itakuwa wanaunga mkono huo wizi na kwamba kuna namna wanafaidika na huo mfumo.

Sasa Mh Rais Wangu Mpenda Haki na Maendeleo hawa watu wanakupanda Mabegani.

Kama wanawezekana tumia sheria na kanuni waliohusika wawajibishwe.

Kama ni watu wenye nguvu sana hawawezekani basi waache waendelee kula. Sisi tutaendelea kunyonywa tu.
 
Marais wengine wote waliopata kuliongoza taifa letu, waliipata nafasi hiyo kwa njia ya sanduku la kura. Aidha wote walikuwa ni wanaume, na wenye kuungwa mkono na mfumo dume uliotamalaki hapa nchini.

Sasa tunaye Mama, tena ni zao la kikatiba tu nje ya mfumo wa sanduku la kura, na tena ni mama wa Kiisilamu, na ni mke mdogo katika ndoa ya mitaala, na tena sana anatoka upande wa Zanzibar. CCM waache majungu, na wala wasimhujumu kwa vigezo hivyo vya kibaguzi na vya kijinsia, kama wanaenda naye mpaka 2025 ni sawa, lakini kama sivyo wawe wawazi.
 
Kuna watu report ya CAG mwaka Jana walitajwa na mwaka huu wametajwa tena na mwakani hao hao watatajwa tena

Mwarobaini wa haya yote ni kuweka sheria ya kunyonga mafisadi

Hata wabunge wanaogopa kutunga hi sheria maana wanajua wasipo nyongwa wao basi watanyongwa watu wao wa karibu
 
Tunakopa halafu tunakuja kuwapa watu wanazitumbua kwa masuala yao binafsi
 
Kuna watu report ya CAG mwaka Jana walitajwa na mwaka huu wametajwa tena na mwakani hao hao watatajwa tena

Mwarobaini wa haya yote ni kuweka sheria ya kunyonga mafisadi

Hata wabunge wanaogopa kutunga hi sheria maana wanajua wasipo nyongwa wao basi watanyongwa watu wao wa karibu
Naunga mkono hoja
 
K
Marais wengine wote waliopata kuliongoza taifa letu, waliipata nafasi hiyo kwa njia ya sanduku la kura. Aidha wote walikuwa ni wanaume, na wenye kuungwa mkono na mfumo dume uliotamalaki hapa nchini.

Sasa tunaye Mama, tena ni zao la kikatiba tu nje ya mfumo wa sanduku la kura, na tena ni mama wa Kiisilamu, na ni mke mdogo katika ndoa ya mitaala, na tena sana anatoka upande wa Zanzibar. CCM waache majungu, na wala wasimhujumu kwa vigezo hivyo vya kibaguzi na vya kijinsia, kama wanaenda naye mpaka 2025 ni sawa, lakini kama sivyo wawe wawazi.
KWa hiyo unataka kusema Jpm alikuwa zao la sanduku la Kura?
 
Kuna watu report ya CAG mwaka Jana walitajwa na mwaka huu wametajwa tena na mwakani hao hao watatajwa tena

Mwarobaini wa haya yote ni kuweka sheria ya kunyonga mafisadi

Hata wabunge wanaogopa kutunga hi sheria maana wanajua wasipo nyongwa wao basi watanyongwa watu wao wa karibu
Mbona unakimbilia kunyonga? Chukueni hata sheria hizi hizi zilizopo nyepesi.
 
Back
Top Bottom