Swali kwa unaefahamu zaidi kuhusu laini za Faith za Halotel

Swali kwa unaefahamu zaidi kuhusu laini za Faith za Halotel

Joined
Aug 31, 2022
Posts
5
Reaction score
20
Katika biashara ya kuuza bando, baada ya laini za Corp na Super Corp zilizokuwa tegemeo la wauza bando kuzuiwa mwezi May, laini za Faith zimekuwa kama tegemeo lililobaki kwa baadhi ya wauzaji kwa sababu zina access ya package ambazo zinaweza kufanya biashara ya bando iwe na maana

Lakini kuna jambo sijapata uhakika nalo. Nimeambiwa kuwa laini hizi za Faith hazifanyi kazi kwenye mikoa yote, bali zinapatikana au zinafanya kazi zaidi kwenye baadhi ya mikoa kama Dar, Arusha, Dodoma n.k. Kwa upande wa Kanda ya Ziwa, nimeambiwa Mwanza, Shinyanga na maeneo mengine hazina hazipatikani

Pia nimeambiwa ukiisajili Dar ukaenda nayo tusene Shinyanga kuna uwezekano menu zake au hizo packages zikatoweka kwa sababu ya location/region

Sasa sijui kama taarifa hii ni kweli au nimepangwa tu😅

Kama kuna mtu anayefahamu mfumo wa hii kitu kwa undani, je kweli kuna restriction ya mikoa? Na kama ipo, inahusianaje na menu/package kuonekana au kutokuonekana?

Nataka kupata clarification kutoka kwa mtu anayefahamu kabla sijafanya maamuzi ya biashara kwa taarifa za kusikia😁
 

Attachments

  • Mfano wa bei za wauzaji kwa sasa.png
    Mfano wa bei za wauzaji kwa sasa.png
    1.4 MB · Views: 16
Hizi lain zipo kuna mtu aliniambia kua amesajili sana lain hizo ila sahizi nikama wamesima sijajua kam watasajili ten
 
Back
Top Bottom