Weka ID yako ya kweliNdiyo maana ya kuwawakilisha wananchi kwa hali na mali haijalishi kuna nn..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Weka ID yako ya kweliNdiyo maana ya kuwawakilisha wananchi kwa hali na mali haijalishi kuna nn..
Ili ugundue nn?Weka ID yako ya kweli
Si nafuu utawala huu CAG anasoma ripoti na uwizi tunausikia. Magufuli alipoambiwa Tsh 1.5 Trillion hazijulikani matumizi yake alimfukuza kazi Prof Assad.Hicho kichaka cha Magu mnachokitumia kuficha uozo kinaendelea kukauka mda si mrefu mtakosa la kuongea then ndipo mtampa heshima yake Magu.
Ulishamsikia Assad akitamka kuna upotevu wa 1.5tr,kama kuna clip ipo nitumie?Si nafuu utawala huu CAG anasoma ripoti na uwizi tunausikia. Magufuli alipoambiwa Tsh 1.5 Trillion hazijulikani matumizi yake alimfukuza kazi Prof Assad.
Tumpongeze Samia kwa kupokea ripoti ya CAG inayoonyesha udhaifu wa Serikali yake.
Nakoleza tuu, na hilo la kuwa na unafuu wa "kupokea" akiwa anamaana Hayati hakupokea ripoti hiyo, ni upotoshaji.Ulishamsikia Assad akitamka kuna upotevu wa 1.5tr,kama kuna clip ipo nitumie?
Je kwenye report ipo hiyo hebu refer page no mimi nikarudie kuisoma upya,labda niliruka sehemu ya 1.5tr?
Tatizo lenu mnapendwa kusimuliwa na kushika maneno ya wanasiasa.
Narudia tena kichaka mlicho zoea kukisingizia kwa mistakes za awamu hii kina endelea kukauka na hamna pakijificha.
Uzi ufungwe , post hii imemaliza kila kituUkitaka wauseme wauawe? The answer is very simple!
Rip ben watch 8 (kama ni kwel ulisha restishwa eny😭😭), pole sana mtoto mtundu lisuh, pole sana mzee maropu na mzee kinainah, pole sana kijana wa nnauye kwa kutaka kubastolishwa hadharan, polen waokotwa virobani bichi, pole na wengine wengi, poleni poleni poleni.....Ndiyo maana ya kuwawakilisha wananchi kwa hali na mali haijalishi kuna nn..
Pasco wa JF ulitaka ben watch 8 wawe wangap ndo uridhike Mkulu?Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu hizi za 'Kwa Maslahi ya Taifa" nikiandika kuhusu jambo lolote la kisiasa, kiuchumi ua kijamii kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, ikiwemo kupongeza, kukosoa, au kushauri kupitia ushauri wa bure kwa mtindo wa swali, halafu jibu utalitoa mwenyewe.
Makala ya leo ni swali la ushauri wa bure kwa viongozi wetu, na haswa wanasiasa wetu, kuhusu kitu kinachoitwa Karma, japo ni kitu cha kufikirika tuu, lakini kipo na kinafanya kazi, yaani Karma is Real!.
Swali lenyewe ni kwa viongozi na wanasiasa wetu wa awamu iliyopita ambao bado wapo kwenye awamu hii, kama waliuona udhalimu wowote wa awamu Iliyopita, na wakaunyamazia, is it right kuusema sasa kwenye awamu hii au kwa vile waliona na wakanyama, ni bora waendelee kunyamaza?.
Naanza bandiko hili kwa maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere "Awamu yetu ilikuwa na mazuri yake, na mengine ya kijinga" . Kauli hii ni kuthibitisha serikali za awamu mbalimbali zinaweza kufanya mambo mema na mazuri, lakini pia zinaweza kufanya mambo mabaya na ya kijinga ukiwemo udhalimu!. Kuhusu hili la udhalimu niliwahi kushauri Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!
Huu ni ushauri kwa viongozi wetu, kama kuna mambo mabaya ya udhalimu wa awamu iliyopita, ukayaona na dhamira yako ikakuambia they are not right, lakini kwa sababu ya uoga, akaamua kunyamaza na kuunyamazia huo udhalimu, then jee tuwashauri, kwa vile waliouona huo udhalimu na kuunyamazia, hata baada ya kuingia awamu nyingine, wao waendelee kunyamaza and take their secrets to their graves?.
Kama wakati mambo ya kidhalimu yanatendeka, wewe kiongozi ukiona na ulinyamaza na hukusema wala kukemea, kwa mujibu wa sheria ya karma, mtu unahukumiwa kwa matendo yako tuu na sio kwa mawazo yako au kwa maneno yako.
Ila mtu ukiona maovu yanatendeka na ukanyamaza kimya bila kukemea, karma inakuhesabu wewe ni mshirika wa uovu ule, kitendo cha kuona na kunyamaza, kinakufanya wewe kuwa ni sehemu ya uovu ule as an accessory either before the facts or after the facts. Karma will only spare you kama utaendelea kunyamaza na salama yako ya karma isikurudi ni kwasababu mtendaji uovu huo, au udhalimu huo sio wewe!, wewe kosa lako ni kujua/kuona uovu unatendeka, hukukemea, hukuzuia.
Lakini kwa awamu hii ya sasa, wewe uliyeunyamazia uovu wa awamu iliyopita, hauna the audacity wa kuutaja uovu wowote wa awamu iliyopita kwasababu uliunyamazia wakati ukitendeka. Watu pekee wenye uwezo wa kuzungumzia uovu, udhaifu na udhalimu wa awamu iliyopita ni wale tuu ambao walisimama imara, wakaupinga, wakausema na wakaulalamikia uovu huo wakati ukitendeka, ili kuuzuia.
Hawa viongozi wa sasa na wanasiasa wa sasa wanao izungumzia awamu iliyopita in a negative way, lakini enzi zile walikuwepo na walinyamaza, karma ya maovu na udhalimu wa awamu iliyopita, haitawaacha salama, lazima itawashughulikia tuu, kwa kuyasema sasa ni kuwahesabu ni kama kumsema vibaya marehemu ambaye hawezi kujitetea!, hivyo ki karma, kosa hilo ni kosa kama kosa la the consecration of the dead!.
Nimetoa ushauri huu, kufuatia baadhi ya viongozi wetu na wanasiasa wetu wa sasa ambao pia waliokuwepo awamu iliyopita na sasa wapo awamu hii, wakikosoa baadhi ya mambo ya awamu iliyopita, ambapo enzi hizo yakifanyika waliona na walinyamaza, sasa Mama anarekebisha mambo, ndio tunawaona sasa wakiibuka na kuanza kusema!.
Naendelea kusisitiza ile haki ya kuona kitu au kusikia kitu na kunyamaza, Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
ukiisha amua kunyamaza, ni unanyamaza mpaka mwisho!, na sio ulinyamaza enzi zile uovu na udhalimu unafanyika, halafu sasa leo baada ya kuona Mama ana fanya mambo, ndio sasa na wewe ndio unaongea!. Karma itakutafuna!.
Ushauri kama huu pia niliwahi kuutoa kwa wanasiasa hama hama Angalizo kwa Wanasiasa hamahama; Japo ni haki yenu lakini msisahau fadhila. Kuweni watu wa shukrani, mtabarikiwa sana, vinginevyo karma Itawahusu!
Hitimisho
Nimalizie kwa lile swali la bandiko hili kwa viongozi na wanasiasa wetu wa awamu iliyopita ambao bado wapo kwenye awamu hii, kama waliuona udhalimu wowote wa awamu Iliyopita, na wakaunyamazia, is it right kuusema sasa kwenye awamu hii au kwa vile waliona na wakanyama, ni bora waendelee kunyamaza?.
Kwa wasioijua karma ni nini karibu mitaa hii "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!
Waseme au wanyamaze?
Paskali
Rejea za baadhi ya mandiko ya kukemea wakati wenyewe wangalipo.
- Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga, Kutasaidia?!.
- Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?.
- Awamu ya tano: Kuweni Wakali, msionee! Tangulizeni utu na ubinaadamu kwanza!
- Madeni ya Taifa: Kuna Kitu Very Serious CAG Amekisema!. Hii kitu haiko sawa and it’s not Right. Je, tunakwenda wapi?!
- Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!
- Nimetishwa, kushitushwa na kuogopeshwa na kauli hii ya Rais Magufuli. Alimaanisha nini?
- TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe
Mkuu Retired, huyu ni wewe, leo imekuweje? Prof. Anna Tibaijuka, ulikaa kimya wakati unahudumu katika Serikali kandamizi ya hiki unachokikemea sasa kulinda maslahi yako, na sasa kaa kimya!Ukitaka wauseme wauawe? The answer is very simple!
ila naunga mkono hoja yako.Wenye akili hatutakusikiliza! Ulikuwa sehemu ya mfumo kandamizi, hukusema lolote ukitetea kwenda "chooni". Leo usitudanganye,ni kwa vile uko nje ya mfumo, lakini huna dhati ya moyo kutetea haki!
Kama ulikubali kushirikiana na wauaji wa wakati ule, leo nyamaza! Nyamaza kabisa, wahutubie hao "ngedere" wasiojua kuwa ukiunguza msitu ukachekelea unaungua, ikifika jioni usilalamike wapi pa kulala!
Ni mimi kabisa, but My point is: kama kweli unautetea msimamo wa demokrasia/haki kama alivyojinadi,( na kweli alichokisema kiko sahihi kabisa) , basi jitenge nao! Ukikaa nao watesaji/wauaji tutakusema kuwa wewe pamoja na kuwa unaiona haki, lakini wewe si mfia haki! Ukiwa Upinzani, unaweza kuangalia hali ikoje, maana lengo ni to prerserve life if needed to be so and therefore sometimes you decide to take other cause to save life!! Ikishindikana then , unasema liwalo na liwe kama walivyoapa maandamano ya 23/9!Mkuu Retired, huyu ni wewe, leo imekuweje? Prof. Anna Tibaijuka, ulikaa kimya wakati unahudumu katika Serikali kandamizi ya hiki unachokikemea sasa kulinda maslahi yako, na sasa kaa kimya! ila naunga mkono hoja yako.
P
Pascal Mayalla , nimekuvuliakofia kwa kutunza kumbukumbu. You are very smart!Ukitaka wauseme wauawe? The answer is very simple!
Mkuu Retired , thanks for appreciation, kofia rasmi mtanivulia 2025 wakati HII inakwenda kutimia.Pascal Mayalla , nimekuvulia kofia kwa kutunza kumbukumbu. You are very smart!
Mazishi ya mtu ambaye ni figure ya taifa ni tofauti na ambaye siyo figure ya taifaWanyamaze tu
Kabla ya maziko Waislamu huwa wanauliza kama kuna madai yoyote kwa marehemu
Uko kibinadamu zaidi 😂Mazishi ya mtu ambaye ni figure ya taifa to tofauti na ambaye siyo figure ya taifa