Swali kwa wafanyabiashara wa Tanzania

ureni

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
1,261
Reaction score
530
Wakuu kuna kitu kimoja nimekiona kwa wafanyabiashara wengi wa Tanzania ambacho naona kama kinaendelea na kuzoeleka kwa wafanyabiashara wengi sina uhakika kama wako sahihi lakini kwa mtazamo wangu naona hawako sahihi.

Kuna wakati nilienda duka fulani kununua vitu ambavyo nauhakika ningemwingizia kipato kama mteja nilifika pale asubuhi nikakuta wamefungua nusu nikiwa na maana wahusika wote wapo lakini wamefungua grill tu kiasi cha kwamba unaweza kuwaona wahusika wote nikaulizia ile bizaa niliyokua naihitaji wakaniambia ipo lakini mda wa kufungua duka bado unaweza kusubiri nikawasisitiza kwa vile nilikua na haraka wakakataa nikaona isiwe shida nikaenda duka lingine nikanunua.

Hivyo hivyo ilishawahi kutokea tena jioni nilienda kwa duka moja wakawa wanafungasha kufunga nikawa nataka kununua bidhaa wakaniambia hatuuzi mda wa kufunga umefika.

Sasa mimi swali langu hawa wafanyabiashara wa Tanzania ni kuwa wametosheka hela sana au hawajui biashara manake mie nafikiria kama nikiwa mfanyabiashara siwezi hata siku moja kumkataa mteja eti kwa sababu mda wa kufunga au kufungua bado kwa staili hii tutaendelea kuachwa mbali na wenzetu sana tusipobadilika.
 
Wengine wanaendesha biashara zao kwa masharti makali... Wakiyavunja wanafilisika. Sasa unataka wafilisike kwa ki sh mia mbili chako?
 
kama ni duka kubwa mida ya jioni ni mida mibaya anaweza kuja mtu kumbe ni jambazi akakomba mapato yote
asubuhi vilevile baadhi huwa wanakuwa bado hawajapeleka hesabu benki hivyo ni uoga tu si chochote
 
MKUU, BIASHARA ZA BONGO ZINAENDESHWA KWA NGUVU YA USHRIKINA KWA 90% NA 10% NI JITIHADA BINAFSI. Kwa hyo hayo ni masharti
 
Wengine wanaendesha biashara zao kwa masharti makali... Wakiyavunja wanafilisika. Sasa unataka wafilisike kwa ki sh mia mbili chako?
Hio " mia mbili chako" zamani wakati ukiwa mdogo ulikua ukipewa unafurah unaenda kununua pipi na big g...leo umepata hela unaidharau.
Endelea.

What goes around always comes around
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…