Swali kwa wanadini wenzangu

Swali kwa wanadini wenzangu

Mwalaye

Senior Member
Joined
Jun 17, 2021
Posts
171
Reaction score
233
Hivi tunajuaje kwamba mtu fulani kapokewa peponi saaafi kabisa?

Maana nilikuwa na jamaa yangu, daa!! Alikufa kwa accident, alikuwa nazo kidogo.

Hayo maombi bana, we acha tu!

Tulizuiwa hata kulia tusije tukawakasirisha wahusika! Maana wakati huo mahali saaafi ndio palikuwa panaandaliwa!

Lakini kimoyomoyo nikawa najiuliza, mmh! mbona jamaa alikuwa na mchepuko wa kinyamwezi mzuri kwelikweli!!

Sasa Kuna aina ngapi za peponi?
 
Shida yako hasa ni ipi:
• Kujua mtu aliyepokelewa peponi
• Kujua aina ya pepo
• Jamaa yako kufariki kwa ajali
• Jamaa yako kuwa nazo kidogo
• Maombi kwa jamaa yako
• Kuzuiliwa kulia msibani
• Kuandaliwa mahali safi
• Au jamaa kuwa na mchepuko/michepuko?
 
Hivi tunajuaje kwamba mtu fulani kapokewa peponi saaafi kabisa?
Maana nilikuwa na jamaa yangu, daa!! Alikufa kwa accident, alikuwa nazo kidogo.
Hayo maombi bana, we acha tu!
Tulizuiwa hata kulia tusije tukawakasirisha wahusika! Maana wakati huo mahali saaafi ndio palikuwa panaandaliwa!
Lakini kimoyomoyo nikawa najiuliza, mmh! mbona jamaa alikuwa na mchepuko wa kinyamwezi mzuri kwelikweli!!
Sasa Kuna aina ngapi za peponi?
وَلِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

[ AL I'MRAN - 129 ]
Na ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Yeye humsamehe na humuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye kurehemu.
 
Hakuna cha pepo; ni mazingira waliojiwekea watu ili wasiogope kifo
 
Mbinguni au peponi tunaingia kwa huruma za Mungu , na sio kwa kipimo cha matendo yetu. Dhambi sio sababu ya mtu kuto ingia peponi ila inaweza ikawa sababu ya ghadhabu ya Mungu juu yake
 
Wala hatuaemi kuwa mtu huyu ni WA peponi au wa motoni isipokuwa yule ambaye imemshuhudilia dalili kutoka kitabu Cha Allah na Sunna za mtume wake. Kwahiyo funga mdomo wako juu ya kuwatabiria watu pepo au moto.
 
Back
Top Bottom