Swali kwa wanajamii

Swali kwa wanajamii

Mponda Mponda

New Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
4
Reaction score
0
Nawasalimia ndugu zangu na naomba kuuliza ili walio na elimu wanisaidie
Swali ni kuwa ninataraji kupata mkopo wa milioni 10 nami ninazo kama milioni tatu kibindoni.Pesa hizo nataka ninunulie gari aina ya Hiace nilitumie kama gari la usafiri kwenda na kurudi kazini lakini pia iwe inasanya abiria hapa Dar es Salaam,
mkopo huo narejesha ndani ya miaka minne, je wakubwa biashara hiyo ya kusanya abiria itanilipa au niachane na mpango huo ninunue gari tu dogo
Asanteni
 
Biashara hiyo itakulipa maana ni lazima watu watoke sehemu moja kwenda nyingine ktk kutafuta maisha...wasiwasi wangu mkubwa ni hiyo pesa..13ml kwa hiace sidhani kama itakuwa ni hiace nzuri..hiace nzuri kwa biashara ni manual pia iwe disel,vinginevyo itasumbua na faida itakuwa ndogo..maana hiace sutomatic ambayo ni petrol inauzwa bei ya chini lakini ki biashara si nzuri...nakupa homework kidogo tafuta dereva yoyote wa daladala mwulize hiace gani ya kununua na njia gani ni nzuri yenye faida atakwambia...siku hizi watu wengi wanapenda hiace super roof(dungu)kwa siku wawezapata 50,000/kulingana na njia lakini bei yake ni 25ml na zaidi..hisinunue hiace kwa kuangalia udogo wa bei itakusumbua
 
Back
Top Bottom