Swali kwa wanaoamini uwepo wa Mungu

Swali kwa wanaoamini uwepo wa Mungu

Je kwanini mnaomba maisha marefu hapa duniani wakati Kuna maisha mazuri mbinguni Kwa baba , kwanini kifo kinaogopwa wakati ni njia ya kwenda Kwa baba kula Raha , kufurahi maisha mazuri yasiyo na dhiki

Imani za Mungu ziko tofauti. Wapo wenye kuamini:

1. Ukifa straight mbinguni au motoni au kwenye kibano kwanza mpaka unyooshe maelezo.
2. Ukifa unalemaa kaburini hadi ufufuo ndipo motoni au mbinguni.
3. Ukifa straight motoni au mbinguni.
4. Nk

Sasa Mkuu hapo huoni tu kwa nini watu wanamwamini Mungu na pia kuomba maisha?

Usisahau hata Yesu aliomba kikombe kumpisha na walioepushwa kifo, Mungu alisema kawaokoa kwa muda huo.

MK254, Mzee Kigogo, Moisemusajiografii au nasema uongo?
 
Mimi sina tatizo na habari za Mungu zikiwa presented kama imani.

Imani haihitaji uthibitisho, haihitaji kuwa kweli. Definition ya imani ni kukubali kitu bika uthibitisho wala uhakikinkwamba ni kweli.

Imani kila mtu anaweza kuwa na yake na zikapingana na kila mtu akawa na haki ya kuwa na imani yake.

Nina tatizo na habari za Mungu zikiwa presented kama fact.

Fact inahitaji uhakiki na uthibitisho, inahitaji kuwa kweli.

Fact haiwezekani kila mtu akawa na yake.
Hapo shida shida ni hawa waamini kusema imani sio imani bali ni hakika🤔🤔🤔
 
Huu uzi hautopata wachangiaji wengi mana unaongelea ukweli unaoumiza
Unaongelea ukweli gani?kwamba kuna mtu anaogopa kufa?

Utaogopaje kitu ambacho kwa namna yoyote huwezi kushindana nacho?yaani utake usitake chenyewe kipo tu na kitakujia tu ufunge mlango kuanzia wa getini mlango mkubwa mpaka wa chumbani kwako kitakuja na kitakuchukua tu!mbwa utamuogopa kwa sababu unajua akija atakung'ata na kichwani utajenga picha jinsi ya kupambana nae na jinsi ya kuhimili maumivu ya meno yake haya niambie kifo utakijengea taswira gani ya kupambana nacho?
 
Unaongelea ukweli gani?kwamba kuna mtu anaogopa kufa?

Utaogopaje kitu ambacho kwa namna yoyote huwezi kishindana nacho?mbwa utamuogopa kwa sababu unajua akija atakung'ata na kichwani utajenga picha jinsi ya kupambana nae na jinsi ya kuhimili maumivu ya meno yake haya niambie kifo utakijengea taswira gani ya kupambana nacho?
Sio kila mtu huogopi kifo kwa namna hiyo🤗
 
Hutopata jibu linalojitosheleza wanaruka ruka kama senene hawana majibu ya kueleweka
 
Unaongelea ukweli gani?kwamba kuna mtu anaogopa kufa?

Utaogopaje kitu ambacho kwa namna yoyote huwezi kushindana nacho?yaani utake usitake chenyewe kipo tu na kitakujia tu ufunge mlango kuanzia wa getini mlango mkubwa mpaka wa chumbani kwako kitakuja na kitakuchukua tu!mbwa utamuogopa kwa sababu unajua akija atakung'ata na kichwani utajenga picha jinsi ya kupambana nae na jinsi ya kuhimili maumivu ya meno yake haya niambie kifo utakijengea taswira gani ya kupambana nacho?
Sawa kufa ili uende mbinguni
 
Sio kila mtu huogopi kifo kwa namna hiyo🤗
Inaposemwa mtu anaogopa kitu fulani utathibitisha kupitia kumuona huyo mtu akijaribu kukikimbia hicho kitu,eg juzi Kariakoo ghorofa limedondoka ungewaona waliojaribu kukimbia ungesema wale wanaogopa kudondokewa na kuta za ghorofa na kweli walikimbia maana madhara yake ni makubwa.

Sasa mfano huu huu ubebe ingia nao pale Muhimbili wards za Mwaisela upate picture kwa wale wagonjwa waliolala hawawezi useme kifo wanakikimbiaje?sahihi isemwe “watu tunaogopa visababishi vya kifo na siyo tunakiogopa kifo”.
 
Hapo shida shida ni hawa waamini kusema imani sio imani bali ni hakika🤔🤔🤔
Hawaelewi hata imani ni nini.

Ukisema imani ni hakika ni sawa na useme imani si imani 😂😂😂
 
Kwanini mnaomba maisha marefu hapa duniani wakati kuna maisha mazuri mbinguni kwa baba?

Kwanini kifo kinaogopwa wakati ni njia ya kwenda kwa baba kula raha, kufurahia maisha mazuri yasiyo na dhiki?
Sababu wengi hawajui Muumba kusudi lake kutuumba sio kufa bali kuishi umilele hapahapa juu ya nchi.Rejea

Hosea 13:14
Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.

1korintho 15:26
Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

Hata kwa akili ya kawaida hakuna mzazi anaezaa mtoto ili amuue sasa Muumba wako si ni zaidi.
 
Binafsi huwa naomba maisha marefu, na naomba Mungu anipe muda zaidi ili nitende mema zaidi na niwe katika nafasi nzuri ya kupokelewa siku nikirejea kwake.

Pia naomba Maisha marefu ili nitimize ndoto za hapa duniani, nilee watoto mpaka wakue, nikiondoka nisiache watu njia panda....

Mwisho kabisa Mungu ndiye hupanga tuishi kwa muda gani, na maamuzi yake hayana kasoro wala makosa, akiamua vyovyote ni kwa matakwa yake.
 
Sababu wengi hawajui Muumba kusudi lake kutuumba sio kufa bali kuishi umilele hapahapa juu ya nchi.Rejea

Hosea 13:14
Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.

1korintho 15:26
Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

Hata kwa akili ya kawaida hakuna mzazi anaezaa mtoto ili amuue sasa Muumba wako si ni zaidi.
Sikuelewi apo ko mauti ni adui na MUNGU wako atakuepusha na mauti mara MUNGU wako aseme wewe ni mavumbi , mavumbin utarudi🤔
 
Sikuelewi apo ko mauti ni adui na MUNGU wako atakuepusha na mauti mara MUNGU wako aseme wewe ni mavumbi , mavumbin utarudi🤔
Yes Mauti na kifo sio kusudi la Muumba kama wengi wanavyodhani kupitia mapokeo mbalimbali.

hiyo mavumbini utarud ni laana baada ya dhambi sio kusudi.

Mhubiri 3:11
Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
 
Kifo hakimpeleki mtu kwa Mungu. Ukisoma Biblia kama ni mkristo inasema kifo ni kama usingizi tu,wafu watafufuliwa hapo siku ya mwisho na kuhukumiwa. Wenye haki wataenda mbinguni na wenye dhambi ni moto wa kuwateketeza milele .
 
Tatizo ni kuwa hakuna mwenye ukweli kuhusu roho inaenda wapi baada ya kifo. Mbinguni ni nadharia tu ya kufirikika. Hii ipo hasa kwa dunia ya tatu.
 
Moja ya sababu inaofanya watu waogope kufa ni majukumu hasa ya malezi unajiuliza wanao Bado wadogo ukifa wataishije ili Hali tegemeo lao niwewe

Wale ambao watoto wao wameshakuwa na wanajitegemea mara nyingi hufa kwa amani

Utafiti mmoja unasema wanaokufa huku wakiacha watoto wadogo hufa kwa kuweweseka wakati wale ambao wanawatoto wanojitegemea hufa kwa amani

Ukitaka kuhakiki Hilo fuatilia msg za waliokuwa wakiandika waliofukiwa na kifusi kariakoo utaona kwanini walikuwa wanatamani waendelee kuishi
 
kwa kuongezea Tu maandiko yanasema yesu kristo died at 33 years old!
hakuhitaji umri mrefu kukamilisha kilichomleta!Nimesikia preachers wakitafsiri hii kwamba
HE DIED AFTER FINISHING WHAT HE WAS SENT FOR,SO TO LIVE LONG DOESNT MEAN YOU ARE BLESSED!
EVEN THE APOSTLE PAUL DIED AFTER FINISHING HIS WORK!FAITH NA FACT ni mafuta na maji
 
Kifo kinaogopwa na hata ambao hawaamini kuna maisha baada ya kifo, mtu anakwambia ukifa ndio kila kitu kimeishia hapo ila bado unakuta kifo anakiogopa.
 
Back
Top Bottom