Swali kwa wataalamu wa masuala ya mikopo

mojoki

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
1,313
Reaction score
290
Ndugu wadau kama ukiwa na Tshs 10 Million, unaweza kuitumia benki kupata mkopo? (Ikatumika kama collateral), Kama jibu litakua sio hapana, Je unaweza kupata mkopo hadi wa Tshs ngapi?...

Msaada tafadhali kwa mwenye hufahamu.
 
Kama ni fixed deposit, utapata up to 80% ya hiyo amount, which will serve as collateral.
 
Kwa ngaz ya mshahara ya tgts e. Nkihitaji m 15 crdb ntapata? Naomba kujuzwa
 
Kwa ngaz ya mshahara ya tgts e. Nkihitaji m 15 crdb ntapata? Naomba kujuzwa

Unaweza kupata mkuu kama utachukua 12m. TGTS E utakuwa unacheza katikati ya laki 7+ mpaka 9+. Kwa kawaida malipo ya mwezi au makato kwenda kwenye mkopo sharti yazizidi asilimia 60% ya mshahara. Tuchukulie unapata 1m utaruhusiwa kukopa kiasi ambacho utalipa kiwango cha juu laki nne hii sheria kaka ya utumishi.
Sasa kama utalipa laki nne 40% kila mwezi kwa miezi 12 ni 4.8m. Kawaida mkopo kwa mtumishi wa fasta usio na kwere ni miaka mitatu hivyo ukikopa 12m na riba ya 18% itakuwa 13.8 pamoja na riba,bima tuchukulie 500k iwe 14.3. Hiyo 14.3 utaweza ilipa kwa miaka mitatu kwa makato ya laki 4 kila mwezi kwa miaka 3. Nenda kakope kaka kamata mpunga huo. Hiyo ni kikokotozi cha Reduced balance method ambacho crdb wanakitumia sana.
 
Kama ni fixed deposit, utapata up to 80% ya hiyo amount, which will serve as collateral.

Mkuu benki gani wanatoa gawio la 80% kwa fixed deposit?? na kwa muda gani?
 
Kasema mkopo sio gawio, read.
 
Kama ni fixed deposit, utapata up to 80% ya hiyo amount, which will serve as collateral.

Can u speak with figures coz nashindwa kuelewa ukisema up to 80% ya hiyo amount

Tuseme ndo nina 10 million....
 
Can u speak with figures coz nashindwa kuelewa ukisema up to 80% ya hiyo amount

Tuseme ndo nina 10 million....

Security ya mkopo ni hiyo 10m, so utapewa say 8m,
 
Ninashukuru sana kiongozi
 
Mkuu benki gani wanatoa gawio la 80% kwa fixed deposit?? na kwa muda gani?

Unaweza kuweka pesa Fixed accoint upokee Riba kidogo tena ukakope bank huku utalipa Riba kubwa? kwa nn usichukue hiyo pesa uliyoweka Fixed ukafanyie mambo yako???
mfano fixed utapokea riba ya asilimia 3% wakati ukikopa utatozwa riba ya asilimia 18% tofauti 13%
think again!!!
 
Keng'oni
Mie sijaleta mada hiyo alieleta ni mtu mwingine. Japo nakubaliana na ukweli kwamba fixed account inaweza tumika kama dhamana,hizo tofauti za charges muhusika ndie zitamhusu. Asante pia kwako
 
kama ukiweka fixed deposit ya high yield unapata riba ya 12%, assume umedeposit millioni 50. Then unakopa 40 million at 18% unafanya biashara inayokupa return ya above 30%, umekosa nini?
 
Ndugu wadau kama ukiwa na Tshs 10 Million, unaweza kuitumia benki kupata mkopo? (Ikatumika kama collateral), Kama jibu litakua sio hapana, Je unaweza kupata mkopo hadi wa Tshs ngapi?...

Msaada tafadhali kwa mwenye hufahamu.

hapo unacheza na hesabu! kukopa bank kwa kutumia fixed deposit kama colateral ni sawa na kujikaanga kwa mafuta yako mwenyewe!
 
hapo unacheza na hesabu! kukopa bank kwa kutumia fixed deposit kama colateral ni sawa na kujikaanga kwa mafuta yako mwenyewe!

jibidiishe upate elimu ya uelewa wa mambo ya kifedha, biashara za kibongo bado hazijawa regulated zina, nyingi zina return kubwa kubwa tu, kwa hiyo it makes sense kukopa kufanyia biashara hizo against a fixed deposit as a collateral
 
Haileti maana yoyote kama fedha unayopata kutoka benki ni ndogo kuliko collateral unayoweka
 
pesa unayo mkononi.. unaogopa kuitumia unaiweka bank fixed halafu hapo hapo unakopa bank kwa riba kubwa?

why usitumie pesa yako kufanya mambo yako... unajibebesha madeni yasiyo na msingi wakati hela unayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…