So unapoteza (18-12) 6% bila sababu yoyote, kwanini uiweka hiyo 50 mil benki na kisha kuchukua mkopo wa 40? Kwanini usinguchukua 40 out of hiyo 50 yako ukaitumia kwenye biashara then ukaweka 10 benki?
Situation ambayo kuchukoa mkopo against fixed deposit inaleta maana ni kwenye dharula, kwa mfano una 50 mill fixed deposit bank ikatokea dharula ukahitaji 40 mil, lakini baadhi ya fixed deposit account haziruhusu kuchukua hela zako kabla ya mda wa makubaliano bila kulipa faini, so kama fixed deposit yako ni ya 1 year ukichukua kabla ya hapo kuna penalty fee unapigwa. Hapa ndo ina make sense kuchukua mkopo badala ya kutoa hela zako kwa kuwa kunakuwa hakuna penalty.
Yote haya yanategemea hiyo penalty ni kiasi gani na riba za fd/loan ya fd/loan ya kawaida of course.