MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,580
Ninakubaliana na hoja na maelezo yako. Nina swali dogo tu: Je, unadhani unaweza "kumnyima" kwa muda gani? Maana umesema kwamba hujisikii, je unaweza usijisikie kwa miezi 6 au 7 au hata mwaka mzima? Ikifikia hapo kwamba hujisikii kwa miezi zaidi ya 6, kwanini usiombe talaka ili kila mmoja aendelee na maisha yake? Ili uwe huru kupata mtu mpya ambae utakuwa unajisikia kumpa.
Hilo linapunguza uwezekano wa yale yaliyompata Clementina. Clementina alikuwa kwenye hali mbaya sana, that day kama mjamaica asingekumbuka kuvaa zana, Clementina wala asingekumbuka kumwambia vaa condom. Kuna maamuzi mengine ambayo yana risk kubwa sana, unajua uhanga ukizidi sana, mtu anaweza kufanya unthinkable. Baada ya kumaliza kufanya ndio anakuja kugutuka na kujiuliza, hivi nimefanya nini? Majuto ni mjukuu!
Aksante Keil kwa swali lako. Ndio maana nikasema si kwamba tunawanyima kwa kupenda kwani kama alivyosema SMU wote tunafaidi katika hilo. Hivyo basi kwa mimi naamini ni kitu cha muda tu .... hasa kama umekosewa na mtu hajaomba msamaha au hamjayazungumza. Ninakubali kabisa kuwa Clementina alivuka mpaka -- that was just too much kiasi kwamba niliguna wakati nasoma kipande kile. Kushindwa kukutimizia haja ile kwa siku mbili au tatu kwangu is reasonable kabisa na kama hakuna suluhisho kwa maana ya kuzungumza juu ya lolote linalozichafua hisia zangu kwa kweli hakuna game. Unless we sit down and clear the way.
Bila hivyo ntalala kama gogo kweli tena.
