jose mjasiriamali
JF-Expert Member
- Sep 17, 2014
- 1,773
- 1,614
10 Bwana akasema, βUmefanya nini? Damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
11 Na sasa umlaaniwa wewe uifunguaye kinywa chake kuipokea damu ya ndugu yako mkononi mwako.
12 Utakapolima ardhi haitakupa tena mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Mambo ya Walawi 17:11:
"Kwa kuwa uhai wa mwili umo katika damu..."
| Kipengele | Maana |
|---|---|
| Damu ya Habili | Ushawishi wa haki, inalia mbele za Mungu kwa kulipiza |
| Ardhi | Shahidi na chombo cha hukumu, ikiwa imechafuliwa na dhambi |
| Laana | Hukumu ya Mungu dhidi ya uovu wa mwanadamu |
| Kaini | Mfano wa mtu anayepuuza dhamira, hataki kuwajibika, haonyeshi toba |
Waebrania 12:24:
"...na kwa damu ya kunyunyizwa, inayo nena mambo mema kuliko damu ya Habili."
βArdhi kama Shahidi katika Biblia: Kutoka kwa Abili hadi kwa Yesu.β
Mungu wa kweli ni mmoja. Lakini mbali na yeye, wapo miungu wengine wanaoabudiwa na kupewa sifa. Nao hufanya ishara nyingi na dhahiri kwa wafuasi wao. Mungu wa kweli, ni upendo amani na utukufu. Mungu hakai kwenye chuki wala mafarakano.Kwahyo ile kauli ya kusema mungu ni mmoja we umeilewa vipi?
Nani kakwambia ardhi "imelaaniwa"?Salaam, Shalom!
Njooni tujadili,
Nikiongea Mimi sana, labda nakuzuia pia kufikiri in deep.
Ni hivi, KITABU CHA( Genesis 3:17, 4:10-11) Kaini anafanya suiside, anamuua nduguye Habil, damu inamwagika ardhini.
Sasa inapotoka adhabu, hakuadhibiwa Cain pekeake, ardhi pia inapewa laana.
Laana inatokana na Ardhi yenye kinywa( mdomo) kufungua mdomo wake na kuipokea damu ya Habil isiyo na hatia.
Hiyo ni DHAMBI mbele za Mungu.
Ndipo tujue, ardhi ni kiumbe hai kabisa kinachosikia, chenye tumbo, kinywa, na ufahamu.
Swali: Kwanini Ardhi inahukumiwa kwa kosa la Kaini?
SOURCE:
Genesis 3:17,
Akamwambia Adam, kwa kuwa uneisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambayo nilikuagiza nikisema, usiyale, Ardhi imelaaniwa kwa ajili yako, kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za MAISHA yaki.
Genesis 4:10-11
10: Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka Katika ardhi.
11:Basi sasa umelaaniwa WEWE Katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako
Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako, fuatisha sala hii:
Ee Mungu katika jina la Yesu Kristo, nina kukiri wewe kuwa bwana na mwokozi wa maisha yangu, ninatubu dhambi zangu zote, ninaomba unisamehe, ulifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uliandike jina langu katika kitabu cha uzima, nipe uwezo wa kuishi maisha matakatifu, dhambi isinishinde, uovu usinishinde, ulevi usinishinde, uzinzi usinishinde, uchawi usinishinde, ninaomba hayo kupitia jina la Yesu Kristo aliye Bwana na mwokozi wa maisha yangu.. Amen
Karibuni π
Ukitaka kutafsiri vifungu vya biblia kwa usahihi, lazima uwe mtaalamu wa kufahamu figures of speech zilizotumika, na hasa lugha za asili zilizotumika katika uandishi wa Biblia kama vile Kiebrania, na Kigriki. Ni kama ilivyo kwa sheria. Ukitaka kutafsiri sheria kwa usahihi, lazima kwanza usome sheria (au usomee sheria), na rules of interpretation, na kuzielewa, ikiwa ni pamoja na kujua kanuni za kisheria (legal principles mbalimbali), na precedents. Vinginevyo, kujua tu kusoma na kuandika, huwezi kutafsiri sheria kwa usahihi, hata kama wewe ni mbobezi katika disciplines zingine. Hata Biblia iko hivyo. Shida ni kwamba kila mtu akisoma Biblia anadhani anaweza kuitafsiri kwa usahihi kwa sababu maneno aliyoyasoma anaona yanajieleza yenyewe, jambo ambalo ni kosa kubwa tunalolifanya, na ndiyo maana kwa vile tunasoma Biblia kama "kitabu cha historia" (kwamba kilichoandikwa ndicho kilichotokea, na kwa mtiririko ulivyo - chronologically), then lazima tukwame mahali fulani. Na katika mkwamo huo, ni wazi tutaona "Mungu kalaani ardhi", "Mungu aliumba dunia/ulimwengu kwa siku sita, na ya saba akapumuzika", na hiyo siku sliyopumuzika ni Jumamosi (Sabato). Tunaona pia "Adamu na Eva walipokula tunda na kujificha, wakati Mungu anatembea katika bustani ya Edeni, Mungu hajua walipojificha, hivyo ilibidi aulize "Adamu, Adamu uko wapi?", etc. Mwisho wa yote, lugha ya binadamu ni limited, haiwezi kumuelezea Mungu kikamilifu, na ndiyo maana Mungu si mwanadamu, na mwanadamu si Mungu. Mwenye kuelewa, na aelewe.Salaam, Shalom!