Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Huu ni muendelezo wa kutoa habari kuhusu utafiti wangu wa kitaalamu huhusu namba za serikali ambazo zinapatikana Wizara ya Fedha, kwenye report ya serikali ya kila mwaka.
Ni muunganiko wa nyuzi ambazo nimekuwa nikizotoa na kuzipa jina 'Namba zinanuka'
. ‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii
. ‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?
Leo nitauliza tu swali la kichokozi baada ya kupitia Wage Bill ya Serikali kuanzia mwaka wa fedha 2016 mpaka 2019.
Nilichogundua ni kwamba, wage bill inakuwa kubwa siku hadi siku, haiakisi kitendo cha serikali kutimua wafanyakazi hewa maelfu na kitendo cha kutokuongeza mishaara kwa watumishi wa umma.
Ki nadharia, kitendo cha kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki, pamoja na kutoongeza mishaara kungetosha kabisa kuwa kunapunguza wage bill ya serikali. Sasa tunavyoona serikali imefanya hayo yote na bado tunaona wage bill inaongezeka, lazima tuhoji, Je, nini kinasababisha hii wage bill kupanda mwaka hadi mwaka?
Ukiangalia kwa makini hiyo chart hapo juu, utagundua kwamba, kutoka mwaka wa fedha wa 2018 mpaka 2019, wage bill ime shoot kwa takribani asilimia 24.96% (Kutoka Trillioni 8.6 mwaka wa fedha 2017, mpaka Trillioni 10.9 mwaka wa fedha 2019)
Unakaa ukijiuliza, je sababu haswa ya serikali kutokuongeza watumishi mishahara ilikuwa ni ipi, kama bado wage bill inaendelea kupanda mwaka hadi mwaka?
Kwa nnavyoona inawezekana kuna mismanagement fulani ambayo mimi na wewe hatuijui, labda serikali siku moja watoke kidedea kutujibu hili swali la ni kwanini pamoja na hatua zote za 1) Kuondoa wafanyakazi hewa, 2) Kutumbua wenye vyeti feki, 3) Kustopisha kuajiri kwa miaka zaidi ya mitatu, 4) Kustisha ongezeko la mishaara kwa watumishi wa serikali, lakini bado wameshindwa kudhibiti ongezeko kubwa la wage bill ambalo linaonekana wazi kwenye namba za serikali na kwenye report za kibajeti.
Kuna nini haswa kinaendelea? Au ndo ule usemi wa wataisoma namba unatimia?
Uzi Tayar.
N. Mushi

| Year | 2016 | 2017 | 2018 | 2019 |
| Wages, salaries, and employee benefits in Tzs '000 | 8,783,734,521 | 8,652,125,857 | 10,129,046,518 | 10,927,828,010 |
| % change | N/A | -1.50% | 17.07% | 7.89% |