Swali la kichokozi: Pamoja na Watumishi hewa kuondolewa na Serikali kutokuongeza mishahara, mbona gharama za mishahara zinapanda kila uchwao?

Swali la kichokozi: Pamoja na Watumishi hewa kuondolewa na Serikali kutokuongeza mishahara, mbona gharama za mishahara zinapanda kila uchwao?

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Huu ni muendelezo wa kutoa habari kuhusu utafiti wangu wa kitaalamu huhusu namba za serikali ambazo zinapatikana Wizara ya Fedha, kwenye report ya serikali ya kila mwaka.

Ni muunganiko wa nyuzi ambazo nimekuwa nikizotoa na kuzipa jina 'Namba zinanuka'

. ‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii
. ‘Namba zinanuka’ – kwanini nasema bado uchumi wetu upo kwenye mkwamo?

Leo nitauliza tu swali la kichokozi baada ya kupitia Wage Bill ya Serikali kuanzia mwaka wa fedha 2016 mpaka 2019.

Nilichogundua ni kwamba, wage bill inakuwa kubwa siku hadi siku, haiakisi kitendo cha serikali kutimua wafanyakazi hewa maelfu na kitendo cha kutokuongeza mishaara kwa watumishi wa umma.

Ki nadharia, kitendo cha kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki, pamoja na kutoongeza mishaara kungetosha kabisa kuwa kunapunguza wage bill ya serikali. Sasa tunavyoona serikali imefanya hayo yote na bado tunaona wage bill inaongezeka, lazima tuhoji, Je, nini kinasababisha hii wage bill kupanda mwaka hadi mwaka?

nambaaaa.JPG

Year
2016​
2017​
2018​
2019​
Wages, salaries, and employee benefits in Tzs '0008,783,734,5218,652,125,85710,129,046,51810,927,828,010
% changeN/A
-1.50%​
17.07%​
7.89%​

Ukiangalia kwa makini hiyo chart hapo juu, utagundua kwamba, kutoka mwaka wa fedha wa 2018 mpaka 2019, wage bill ime shoot kwa takribani asilimia 24.96% (Kutoka Trillioni 8.6 mwaka wa fedha 2017, mpaka Trillioni 10.9 mwaka wa fedha 2019)

Unakaa ukijiuliza, je sababu haswa ya serikali kutokuongeza watumishi mishahara ilikuwa ni ipi, kama bado wage bill inaendelea kupanda mwaka hadi mwaka?

Kwa nnavyoona inawezekana kuna mismanagement fulani ambayo mimi na wewe hatuijui, labda serikali siku moja watoke kidedea kutujibu hili swali la ni kwanini pamoja na hatua zote za 1) Kuondoa wafanyakazi hewa, 2) Kutumbua wenye vyeti feki, 3) Kustopisha kuajiri kwa miaka zaidi ya mitatu, 4) Kustisha ongezeko la mishaara kwa watumishi wa serikali, lakini bado wameshindwa kudhibiti ongezeko kubwa la wage bill ambalo linaonekana wazi kwenye namba za serikali na kwenye report za kibajeti.

Kuna nini haswa kinaendelea? Au ndo ule usemi wa wataisoma namba unatimia?

Uzi Tayar.

N. Mushi
 
Nadharia mbili!
1.Fedha zinazoongezeka ndio huliwa(ufisadi) wa awamu hii!yaani ajira hewa,madaraja hewa,increment hewa zisizolipwa hulipwa wao na kuzitumia wao wenyewe badala ya wafanyakazi!!!

2.Divide and rule kuna wafanyakazi kama wa TISS,JESHI NA TAKUKURU NDIO HUINGIZIWA BAJETI YA MASLAHI YA WAFANYAKAZI!WENGINE Wamesahaulika au hawana impact ya moja kwa moja kwa utawala huu kama kundi nililotaja mwanzo!kwa hiyo stahiki zao zimetamalaki kuliko kundi kama walimu,madaktari na wengineo!

NADHANI HIVYO LABDA WENGINE WANIPE MWANGA!!!
 
Nadharia mbili!
1.Fedha zinazoongezeka ndio huliwa(ufisadi) wa awamu hii!yaani ajira hewa,madaraja hewa,increment hewa zisizolipwa hulipwa wao na kuzitumia wao wenyewe badala ya wafanyakazi!!!
2.Divide and rule kuna wafanyakazi kama wa TISS,JESHI NA TAKUKURU NDIO HUINGIZIWA BAJETI YA MASLAHI YA WAFANYAKAZI!WENGINE Wamesahaulika au hawana impact ya moja kwa moja kwa utawala huu kama kundi nililotaja mwanzo!kwa hiyo stahiki zao zimetamalaki kuliko kundi kama walimu,madaktari na wengineo!!!!NADHANI HIVYO LABDA WENGINE WANIPE MWANGA!!!
Yaweza kuwa
 
Acha siasa za kishamba, kila mwaka serIkali inaajiri
Hili jibu lako ni fact ama opinion?

Hebu njoo na takwimu ambazo zina justify ulichokisema. Vinginevyo labda unatufurahisha.

Halafu labda tunaishi Tanzania tofauti sana, unavosema suala la ajira mpya kwenye huu utawala.
 
Nadharia mbili!
1.Fedha zinazoongezeka ndio huliwa(ufisadi) wa awamu hii!yaani ajira hewa,madaraja hewa,increment hewa zisizolipwa hulipwa wao na kuzitumia wao wenyewe badala ya wafanyakazi!!
Utakuwa upo sahihi sana mkuu, kwenye hizo point zote mbili. Of which pia kama haswa ni kweli, ina maana tunaelekea mule mule kwenye 'MISMANAGEMENT OF PUBLIC FUNDS' maana ikumbukwe hizi ni pesa za walipa kodi

Hususani point ya chini, inawezekana kabisa wafanyakazi wa vyombo vya ulinzi wameneemeka at the expense of wafanyakazi wanazengo..
 
Teua, Tumbua! Simamisha kazi, Rudisha! Ulinzi binafsi wa mijitu yenye miraba minne kama wa yule Rais wa Iraq/Kuwait Muammar Gaddafi na mivifaa ya kustaajabisha, Ajira za Wakuu wa Mikoa, Wilaya, nk. ambao hawana faida yoyote ile kwa Nchi isipokua Ccm.

Ila kwa Watumishi wengine, mambo yako pale pale. Hakuna mabadiliko, zaidi tu unavutwa shati na yale makato ya 15% ya bodi.
 
Au umepata aibu kuuliza! Mwenzako hapo juu anabisha kuwa serkali haiajiri kila mwaka!
Hao ndio vijana wanaweza kuingia Jamii forum nakuropoka ila wanashindwa kuingia wavuti ya utumishi kuangalia ajira zinazotangazwa
Sina, wala sitaki hata kusema neno
 
Mbona mishahara imeongezwa kimyakimya tangu 2017 mpaka 2020. Kama hujaona nyongeza jua kuwa huna umuhimu kwa mtawala.
Pole kwa hii post
 
Au umepata aibu kuuliza! Mwenzako hapo juu anabisha kuwa serkali haiajiri kila mwaka!
Hao ndio vijana wanaweza kuingia Jamii forum nakuropoka ila wanashindwa kuingia wavuti ya utumishi kuangalia ajira zinazotangazwa
Hahahaha kweli "imeajiri kila mwaka" sijui unamfanya nani mjinga
 
Teua, Tumbua! Simamisha kazi, Rudisha! Ulinzi binafsi wa mijitu yenye miraba minne kama wa yule Rais wa Iraq/Kuwait Muammar Gaddafi na mivifaa ya kustaajabisha, Ajira za Wakuu wa Mikoa, Wilaya, nk. ambao hawana faida yoyote ile kwa Nchi isipokua Ccm.

Ila kwa Watumishi wengine, mambo yako pale pale. Hakuna mabadiliko, zaidi tu unavutwa shati na yale makato ya 15% ya bodi.
Kabisa mkuu hilo la tengeu teua pia inawezekana ndo sababu THE BREED ametoa pia hoja nzuri sana

******

Nadharia mbili!
1.Fedha zinazoongezeka ndio huliwa(ufisadi) wa awamu hii!yaani ajira hewa,madaraja hewa,increment hewa zisizolipwa hulipwa wao na kuzitumia wao wenyewe badala ya wafanyakazi!!

2. Divide and rule kuna wafanyakazi kama wa TISS,JESHI NA TAKUKURU NDIO HUINGIZIWA BAJETI YA MASLAHI YA AFANYAKAZI!WENGINE Wamesahaulika au hawana impact ya moja kwa moja kwa utawala huu kama kundi nililotaja mwanzo!kwa hiyo stahiki zao zimetamalaki kuliko kundi kama walimu, madaktari na wengineo!!

NADHANI HIVYO LABDA WENGINE WANIPE MWANGA!!!
 
Acha siasa za kishamba, kila mwaka serkali inaajiri
Mkuu, namba hazina chama, ingependeza uje na takwimu kuthibitisha ulichosema.

Wala usidhani mimi nimekuja na hizi namba kwa minajili ya kuponda.

Kama wewe unadhani unanufaika na system iliyopo madarakani, usidhani kwamba ni guarantee ya kizazi chako kunufaika na system ya wakati unaokuja.

Ndo mana saa nyingine, huwa nawaasa hata CCM kuwa na jicho la kizalendo hasa wakati tunachambua baadhi ya mambo, sio kila kitu ni cha kupinga. Kuna vingine unavipokea na kuvihoji positively maana vina impact hata kwenye kizazi chako

Usijiangalie wewe, angalia wajukuu wa watoto zako.
 
Back
Top Bottom