Swali la Kimajungu: Kwanini Mhuhujumu Uchumi Idd Simba yuko nje?

Amiliki

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Posts
2,085
Reaction score
1,005
Ndugu wanabodi,

Kwa uelewa wangu, sheria ya Uhujumu Uchumi nchini inamnyima dhamana mtu "yeyote" aliyeshitakiwa mahakamani kwa kosa hilo. Lakini jambo la ajabu nilaloendelea kulishuhudia ni kwamba hata baada ya mashtaka ya akina Idd Simba kurekebishwa na kuangukia kwenye makosa ya Uhujumu uchumi bado wameendelea kuwa nje kwa dhamana. Je hii sheria ya Uhujumu Uchumi ilishabadilishwa? Kama la, je nchi hii sheria moja huwa inatumika tofauti kwa watu wawili tofauti?
Nawakaribisha wenye uelewa na si watu wanaokuja kutetea kwa misingi ya kabila au dini ya mtu.
 
Mi nilijua yupo nje ya nchi..anyway muulize ana msimamo gani kuhusu gesi ya Mtwara?
 
Ndugu wanabodi,

Kwa uelewa wangu, sheria ya Uhujumu Uchumi nchini inamnyima dhamana mtu "yeyote" aliyeshitakiwa mahakamani kwa kosa hilo. Lakini jambo la ajabu nilaloendelea kulishuhudia ni kwamba hata baada ya mashtaka ya akina Idd Simba kurekebishwa na kuangukia kwenye makosa ya Uhujumu uchumi bado wameendelea kuwa nje kwa dhamana. Je hii sheria ya Uhujumu Uchumi ilishabadilishwa? Kama la, je nchi hii sheria moja huwa inatumika tofauti kwa watu wawili tofauti?
Nawakaribisha wenye uelewa na si watu wanaokuja kutetea kwa misingi ya kabila au dini ya mtu.

Unadhani akiiba anakula pekeake? wanajua wakimweka ndani maslahi yao pia yataharibika
 
yuko nje anaota jua, ngoja jua lizimike 2015 kama hajarudi ndani mwenye bila kuambiwa.
 
Mkuu unakuwa kama mgeni katika nchi hii?! Umeshawahi kumuona mhujumu uchumi au fisadi gani yupo jela??! Kila siku tunaambiwa kuna mafisadi lakini hamna hata mmoja aliyewahi kufungwa.
 
Back
Top Bottom