Swali la kizalendo: Mabeberu ni kina nani?

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Dunia inaenda kwa kasi sana, ukizubaa unaachwa!

Wakati wa vita baridi neno Mabeberu lilitumika sana hapa Tanzania. Enzi zile beberu alikuwa ni mtu yoyote asiye mjamaa, mpinga mapinduzi, anayeamini katika soko huria na uliberali.

Polepole neno mabeberu lilianza kufifia baada ya kuanguka kwa ukuta wa Berlin, na nchi zetu zikaanza uchumi na siasa za kiliberali. Hata mabeberu makaburu tukawakaribisha na kuanza kuwaita wawekezaji!

Kimsingi neno beberu likafa.

Hivi karibuni Mh Rais ameanza kurudisha msamiati huu wa Mabeberu, akimaanisha watu wote wa nje wanaompinga sera za nchi.

Swali langu hapa ni je, hawa ambao tunawaita mabeberu tunawajuaje, kwa sera zao, imani zao, au kitu gani?

Au inategemeana tu na muktadha. Kesho Canada anaweza kuwa beberu kesho asiwe.

Ni muhimu kuweka wazi hii Sera yetu hasa inasimamia nini?

Mungu ibariki Tanzania!

BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU
---
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Zinaitwa lugha za majukwaani za kuwaponda ila hawawezi ishi bila misaada yao.Nyerere aliwaponda mabeberu lkn ndo waliomuokoa alipotaka kupinduliwa bila mabeberu awawezi kitu wanajimwambafy tu
 
Mabeberu miaka hii wansjuta kuijya Tanzania!
 
Mkuu hawa wahuni wanaotumia huu msamiati hata siku moja hawajawahi kuzitaja hizo Nchi za MABEBERU ni zipi.

 
Ubeberu ni hatua ya juu ya Ukoloni(imperialism), ambapo nchi tajiri zinaendelea kuzinyonya nchi maskini kwa njia ya uchukuaji wa rasilimali na pia misaada na mikopo yenye masharti magumu.
 
Mabeberu in wale wanaowakopesha ccm ambao huwaita wahisani
 
Ubeberu ni hatua ya juu ya Ukoloni(imperialism), ambapo nchi tajiri zinaendelea kuzinyonya nchi maskini kwa njia ya uchukuaji wa rasilimali na pia misaada na mikopo yenye masharti magumu.
Kwa tafsiri hii inawezekana China ni Beberu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…