Dunia inaenda kwa kasi sana, ukizubaa unaachwa!
Wakati wa vita baridi neno Mabeberu lilitumika sana hapa Tanzania. Enzi zile beberu alikuwa ni mtu yoyote asiye mjamaa, mpinga mapinduzi, anayeamini katika soko huria na uliberali.
Polepole neno mabeberu lilianza kufifia baada ya kuanguka kwa ukuta wa Berlin, na nchi zetu zikaanza uchumi na siasa za kiliberali. Hata mabeberu makaburu tukawakaribisha na kuanza kuwaita wawekezaji!
Kimsingi neno beberu likafa.
Hivi karibuni Mh Rais ameanza kurudisha msamiati huu wa Mabeberu, akimaanisha watu wote wa nje wanaompinga sera za nchi.
Swali langu hapa ni je, hawa ambao tunawaita mabeberu tunawajuaje, kwa sera zao, imani zao, au kitu gani?
Au inategemeana tu na muktadha. Kesho Canada anaweza kuwa beberu kesho asiwe.
Ni muhimu kuweka wazi hii Sera yetu hasa inasimamia nini?
Mungu ibariki Tanzania!
BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU
---