Muulize jiweDunia inaenda kwa kasi sana, ukizubaa unaachwa!
Wakati wa vita baridi neno Mabeberu lilitumika sana hapa Tanzania. Enzi zile beberu alikuwa ni mtu yoyote asiye mjamaa, mpinga mapinduzi, anayeamini katika soko huria na uliberali.
Polepole neno mabeberu lilianza kufifia baada ya kuanguka kwa ukuta wa Berlin, na nchi zetu zikaanza uchumi na siasa za kiliberali. Hata mabeberu makaburu tukawakaribisha na kuanza kuwaita wawekezaji!
Kimsingi neno beberu likafa.
Hivi karibuni Mh Rais ameanza kurudisha msamiati huu wa Mabeberu, akimaanisha watu wote wa nje wanaompinga sera za nchi.
Swali langu hapa ni je, hawa ambao tunawaita mabeberu tunawajuaje, kwa sera zao, imani zao, au kitu gani?
Au inategemeana tu na muktadha. Kesho Canada anaweza kuwa beberu kesho asiwe.
Ni muhimu kuweka wazi hii Sera yetu hasa inasimamia nini?
Mungu ibariki Tanzania!
BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU
---
Uko sahihi kabisa. Watawala wadhalimu kwanza huwaaminisha wananchi wao kuwa ni 'wanyonge'. Kisha uwapiga deki ya ubongo kuwa adui wao mkuu ni 'mabeberu'. Baada ya hapo huwaswaga kama 'makondoo' kwa namna wanavyojisikia. Unaweza kuwakusanya uwanja wa taifa ili waburudishwe na wasanii wa bongonjaa kuonesha unavyowapenda sana. Hayati mzee Mugabe ndivyo alivyowanyanyasa Wazimbabwe akiwaaminisha adui yao mkubwa ni mzungu, wakati adui wao mkuu alikuwa yeye. Alipoaga dunia, Wazimbabwe walimiminika mitaani kusherehekea!!!!Mabeberu ni neno linatumiwa na wanasiasa ili kulaghai wananchi ambao uelewa wao wa dunia ni mdogo. Wanasiasa wanao tumia neno wanasema kwa midomo tu ila mioyoni mwao wanajua kwamba siyo kweli.
Dunia inaenda kwa kasi sana, ukizubaa unaachwa!