Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Hebu chukulia kwamba, umeolewa na umeishi na mumeo kwa takriban miaka kumi. Siku za karibuni mumeo ameanza tabia chafu ya kutembea na wasichana wa kazi, mpaka ukaamua kutokuwa na wasichana wa kazi kabisa.
Lakini kutokana na ugumu wa kazi za nyumbani na malezi pamoja na majukumu ya kazini kwako ulipoajiriwa, umeamua kumleta mdogo wako wa kike mliozaliwa tumbo moja ili wakati anasubiri matokeo yake ya kidato cha nne akusaidie kazi za hapo nyumbani.
Baada ya wiki kadhaa mdogo wako anakujulisha kwamba anataka kuondoka kwa sababu mumeo amemtongoza na baada ya kumkatalia amejaribu hata kumbaka zaidi ya mara mbili, na inaonekana amedhamiria kutekeleza jambo hilo, hivyo ili kuepuka hali hiyo ameamua kuondoka…………
Je kama ni wewe ungefanyaje?