Swali la kizushi........Asome mwanamke tu...

Swali la kizushi........Asome mwanamke tu...

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Hebu chukulia kwamba, umeolewa na umeishi na mumeo kwa takriban miaka kumi. Siku za karibuni mumeo ameanza tabia chafu ya kutembea na wasichana wa kazi, mpaka ukaamua kutokuwa na wasichana wa kazi kabisa.

Lakini kutokana na ugumu wa kazi za nyumbani na malezi pamoja na majukumu ya kazini kwako ulipoajiriwa, umeamua kumleta mdogo wako wa kike mliozaliwa tumbo moja ili wakati anasubiri matokeo yake ya kidato cha nne akusaidie kazi za hapo nyumbani.

Baada ya wiki kadhaa mdogo wako anakujulisha kwamba anataka kuondoka kwa sababu mumeo amemtongoza na baada ya kumkatalia amejaribu hata kumbaka zaidi ya mara mbili, na inaonekana amedhamiria kutekeleza jambo hilo, hivyo ili kuepuka hali hiyo ameamua kuondoka…………

Je kama ni wewe ungefanyaje?
 
Tusingefika huko, akitembea na mfanyakazi wa ndani mara ya kwanza tu, namtimua asirudi tena kwangu

Ahsante
 
ushaona anatembea na house girl then kwanini umlete mdogo wako,
 
ni ugonjwa gani tena huo...........anatakiwa kumketiisha mumewe chini na kuongea hilo sio jambo la kulifumbia macho na ikiwezekana kushirikisha ndugu kwa msaada zaidi
 
Mtambuzi wakati mwingine huwa ni ngumu kupredict utafanya nini kwenye kitu ambacho hakijatokea .............unaweza sema leo utamnyonyoa nywele ,mara utamfukuza lakini siku yakikukuta unaishia kuzirai nahata ukiulizwa imekuaje unaishia kuwa bubu.
 
Ha ha ha haaa! Hii thread imenichekesha lol! Huo ugonjwa unatisha aisee!
 
kizuri kula na nduguyo namwambia mdogo wangu ampe tu kama anataka loh
 
Dawa house boy tu tena handsom handsome fulani hiviii, halafu nakuwa karibu nae sana. No more house maids, wala mdogo wangu asingekuja. House boys tu na watoto wote boarding schools maana, huo ugonjwa mdadala wake unaweza kuwa watoto. Magonjwa ya wanaume, mengine hatari tupu jameni.
 
Hebu chukulia kwamba, umeolewa na umeishi na mumeo kwa takriban miaka kumi. Siku za karibuni mumeo ameanza tabia chafu ya kutembea na wasichana wa kazi, mpaka ukaamua kutokuwa na wasichana wa kazi kabisa.

Nilidhani hapo kwenye nyekundu pangezusha maswali lakini nimeshangaa wachangiaji wote wamepa over look.....LOL
Hebu jiulizeni kwanza miaka kumi ya ndoa halafu siku za karibuni mumeo ameanza kutembea na wasichana wa kazi, hivi hapo hapazushi maswali kweli?
Hivi haiwezekani kwamba kuna vita ya tendo la ndoa chumbani kwa wanandoa hao? Au haiwezekani kuna udhaifu fulani upande wa mke kweli?
Hebu jaribuni kufikiria majibu yenu upya bana..............................
 
je mwanamke hana tatizo kweli isije kuwa kawa busy sana na kazi mpk hamdumii mr ipasavyo,,,matokeo yake ni mume kutafuta mbadala,,,pia shukuru anachezeya uwanja wa nyumbani wengine huwa wanakimbilia kwa madada poa mtaani mwishowe magonjwa...mkalishe chini muulize nini chanzo then mrekebishe msonge mbele maana miaka 10 alikuwa safi iweje leo?nawasilisha
 
Back
Top Bottom