nyamatala.
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 266
- 134
Hapo tatizo liko wapi? Fursa sawa iwe kwa wote. Kupata ziro siyo mwisho wa dunia. Ni siyo?
Unapofeli kwenye eneo moja, ni fursa nyingine ya kuongeza juhudi kwenye eneo hilohilo au kujaribu eneo jingine. Kama umefeli shule basi jaribu kazi za nguvu kama kilimo, uvuvi, biashara, kucheza dance n.k
Lengo la kukupatia elimu wewe si tu ikufae wewe, bali hata jamii inayokuzunguka inufaike. Sasa kila taaluma ina sifa zake kulingana na uzito wa taaluma yenyewe, sasa sifa za kuingilia kusoma hizo kozi huna, maana yake hufai. Kulazimisha kukuchukua ni kutaka kujaza nafasi ambazo zinawastahili wenye sifa zao ambazo huna.
Yule ziro mbona alimaliza miaka kumi kulikua na shida gani ? na kama zero in janga kwa nini na yenyewe iitwe division hoja ipo hapa hakuna mwenye division zero anaetembea uchi huyu nae asome chuo.
Mwenye kisu kikali ndiye anaruhusiwa kula nyama wewe kisu chako ni butu huna budi kula kwa macho.
Mpaka hapo nimeeleweka nini namaanisha.
Ni wewe huyu [emoji28]View attachment 1153162
Zamani kulikuwa na Marticulation Exam ambao ulitumika kuwachuja wanaostahili kujiunga na chuo. Utaratibu huo ulikuja kufutwa, na kuacha kipimo kiwe ni mtihani wa taifa wa form six na diploma kwa wale wa equivalent.Ikiwa nitashindwa kwenye ushindani dhidi ya wenzangu waliopata maksi nyingi kunizidi, hapo hakuna neno. Hata wenye divisheni wani kali hukosa nafasi kwa kuzidiwa na wenye divisheni wani kali zaidi. Lakini nipewe fursa ya kujiunga, nishindwe mwenyewe.
Zamani kulikuwa na Marticulation Exam ambao ulitumika kuwachuja wanaostahili kujiunga na chuo. Utaratibu huo ulikuja kufutwa, na kuacha kipimo kiwe ni mtihani wa taifa wa form six na diploma kwa wale wa equivalent.
Kwahiyo unatakiwa ujue kuwa ukifeli form six umefeli kipimo cha kuingia chuo chochote kwa ngazi ya digrii. Chukua cheti chako cha form four kaanze certificate.
Ulijiunga jamii forums ukiwa la kwanza ?Yap!
Lol,Chuo nasikia mkifika mnaanza sufuri. Mwalimu anawafundisha mwenyewe, anatunga mtihani mwenyewe, anasahihisha mwenyewe, maksi anatoa yeye. Unafelije kwa mfano? Ukifeli unapewa supu, unarudia mtihani. Ukiifeli mtihani wa supu unarudia tena somo mwaka mwingine. Nani atashindwa shule ya hivyo?