Toxic Concotion
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 5,760
- 20,837
Mzee uchawi hauna sura, siku hizi hata vijana wanayo hayo mambo! Ukimkuta nje yuko smart kachomekea huwezi amini! Ila kwenye anga zake ni gwiji kuliko Chriss Katembo kwenye fani yake ya uchoraji!
Kuna jamaa tulienda nae semina miaka ya nyuma. Kwa bahati mbaya alikula samaki ambae hakujua ana allergy nae, kupelekea kushindwa kuhema. Katika jaribio la kutoa huduma ya kwanza, watu wakamfungua vifungo vya shati na kumvua viatu; ndio kukuta bonge la hirizi jeusi kwenye socks. Alipopata nafuu na seminar yenyewe hakuitaka tena.