Swali la kizushi

Swali la kizushi

Zeni2017

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
1,247
Reaction score
534
Ukiwa form five shule ya serikali halafu uache shule mwaka mzima. Ukirudi shule utaendelea na form six, utarudia form five au utakuta wameshakufukuza shule? Na ukiacha shule halafu baadae ukiwa na miaka 18 ukiamua kurudia la saba unakubaliwa kisheria hukubaliwi?
 
Nakumbuka niliwahi soma sehemu usipoonekana shuleni miezi 6 basi umeshajifukuzisha. mwenyewe.

Na hilo la kurudia LA Saba inawezekana ila urudie kwa jina la mtu mwingine.

Ruksa kusahihishwa.
 
Nakumbuka niliwahi soma sehemu usipoonekana shuleni miezi 6 basi umeshajifukuzisha. mwenyewe.

Na hilo la kurudia LA Saba inawezekana ila urudie kwa jina la mtu mwingine.

Ruksa kusahihishwa.

Lol sasa kama ni kurudia kwa jina la mtu mwingine ni ruhusa ya vipi?
 
Au nirekebishe swali ni umri gani kwa Tanzania mwanafunzi anatakiwa awe ameshamaliza elimu ya sekondari.
Kama niliishia la sita sikufanya mtihani wa la saba inaruhusiwa kurudia la sita nikiwa na miaka ishirini?
 
Ukijijibu haya maswali utaona hili suala la kuruhusu waja wazito shule halina mshiko. Kuna wenye sababu za maana zaidi sheria inawabana hawawezi kurudi shule.
 
Au nirekebishe swali ni umri gani kwa Tanzania mwanafunzi anatakiwa awe ameshamaliza elimu ya sekondari.
Kama niliishia la sita sikufanya mtihani wa la saba inaruhusiwa kurudia la sita nikiwa na miaka ishirini?
Inawezekana mkuu la sita miaka 20

Kibongo bongo wanamaliza sekondari wakiwa na miaka 18-21
 
Sheria inasemaje. Kama hakuna sheria hiyo ni vurugu mechi wizarani huko. Kuna haja ya kujipanga wizara itoe muongozo hadharani ili watu wajue kinachoendelea. Ingeondoa hili zogo la wanaojifungua wakiwa wanafunzi. Ikumbukwe wamekataliwa kurudi kwenye shule za serikali tu. Kwa sheria za nchi nyingine kama Marekani ukipita miaka 19 ndio basi hakuna shule ya serikali wala private itakayokupokea.
 
Back
Top Bottom