Sijawahi, naomba Mungu aniepushie nisiwahi. Huwa nashangaa ni vipi mtu anatembea na rafiki ya mume wake achilia mbali kaka/dada. Na unajua kwa nini sitathubutu, namwoneaga huruma mume wangu naona kama atachoreka, rafiki yake/kaka yake/ mdogo wake anifanyie kama yeye anavyonifanyia, halafu ikitokea siku moja tuwe wote hapo yaani mume wangu na huyo mwizi, naona kama baba D wangu atakapokuwa anaongea kitu chochote hata kama kina point huyo mwizi atakuwa anawazia kichwani kwake, haaahhh wapi wewe kitu gani? unachokulaga na mimi ndo hichohicho ninakula sasa kama ni kitamu au ni kichungu mmhhh!!!! Hapana sijisikii vizuru kabisa kutenda hichi kitu kwa mtu wetu wa karibu ambaye najua kwa vyovyote vile ipo siku tutajumuika wote watatu, sitaki na nakemea kwa jina la YESU huyu pepo apishe mbali kabisa na upeo wa macho yangu.