Bishanga (abashaija)!
Mimi nlishawahi kuwa na mahusiano na dada na mdogo wake - nyakati hizo za zamani.. Dada mtu na mimi tulikuwa tunasoma "O" level mkoani Kilimanjaro, shule tofauti tofauti though, kwahiyo katika harakati za kupanda TRENI & tukafahamiana and then boom! Mdogo mtu nilifahamiana naye shule ya msingi nilikuwa nimemtangulia madarasa kadhaa lakini alikuwa jirani kwahiyo ikawa hivyo...
Hii ilitokana na wazazi wetu(mimi na hao mabinti) kuoa wanawake zaidi ya mmoja kwahiyo - binti mdogo alikuwa anakaa kwa mama na binti mkubwa alikuwa anakaa kwa baba - na mimi nilisoma shule ya msingi nikiishi na baba na secondari nikiwa likizo nilienda kumsabai mama! Nilifahamu undugu wao baada ya kumdadisi sana binti mkubwa tukiwa kwenye TRENI kuelekea Moshi... Alikuwa na chuki sana na MAMA yake kiasi cha kutopenda hata kumtaja, lakini mwishowe aliponiambia kuwa Mama yake ni fulani na fulani ni mdogo wake wa "damu" ndiyo ulikuwa mwisho wangu na "wao"