sjawai...aitatokea
bt nimeona mdada kamchukua mkaka na mdogo wake
walipoachana na kakamtu akaamia kwa mdogo mtu the same haus ni kwamba bafu,jiko ni lile lile kilichobadirika ni badala ya kuingia chumba cha kushoto akawa anaingia cha kulia...bt swaga ni zilezile mdada hana wasiwasi ni kwa raha zake!!!!
hata mimi sijawahi.
ilaa maria huu ni ujasiri au ni akili kutokua timam??
bora bsi hata huyo kaka/mdogo mtu angkua mbali, nyumba1??
Sisi sote ni binadamu na kila mmoja wetu ana mapungufu yake,mi naomba niulize kijiswali hiki: Hivi ushawahi kuwa na mahusiano na mtu na na dada yake? na kama wewe ni mwanamke ishawahi kukutokea ukatembea na mtu na kakake? just in case mlibambwa ilikuwaje?
Kuna mtu wangu wa karibu yamemkuta.Ilianza kama masikhara tu ,ye ameoa mdogo ,karibu kila weekend wana tabia ya kutoka pamoja,jamaa,mke na ndugu wengine.Yeye anadai shemeji yake ndo alianza kumsuguasugua miguu chini ya meza wakati wanakamata ulabu na baadae isiwe isiwe mwisho walishtukia wanapeana miadi na kuishia gesti(shem naye ana ndoa). Sasa majuzi mme wa dada ndo kamfata mdogo mtu anamwambia 'nisindikize kuna kitu kitu nikauonyeshe' 'nini?' anauliza mdogo mtu,'we twende tu'.Haoooo mpaka farm maeneo ya Kibamba. Kumbe ukware wao walikuwa wanaufanyia kwenye banda la family farm Kibamba.Hilo valangati Mungu ndo anajua,tunavyoongea jamaa mke kahama nyumba,na huko dada mtu katimuliwa,yaani vurugu vurugu sijui itaishaje.Mie nilona kwa dada zangu walichanganywa bila kujua walipojua mkubwa akamwachia mdogo.
Na mimi nakuuliza swali la kizushi: Bishanga ulishawahi wewe kuwa na uhusiano wa mtu na mdogo wake
Sisi sote ni binadamu na kila mmoja wetu ana mapungufu yake,mi naomba niulize kijiswali hiki: Hivi ushawahi kuwa na mahusiano na mtu na na dada yake? na kama wewe ni mwanamke ishawahi kukutokea ukatembea na mtu na kakake? just in case mlibambwa ilikuwaje?
Niliishawahi... ilitokea nikiwa A level nikawa na demu fulani na nilipofioka Chuo nikawa na demu mwingine. sikujua kama ni ndugu kumbe ni mtu na dada yake maana wa kwanza aliishi mwanza na dada yake dar ila nilifahamu siku za mbele. haikuwa soo saaana maana walielewa ni nini sababu
sijawah...
ila nlipokuwa kabinti kuna aliyenitokea nilipomgomea,
baada ya muda hiv kaka ake naye akaleta story ile ile, nilimkimbiza mbaya.
Sijawahi, naomba Mungu aniepushie nisiwahi. Huwa nashangaa ni vipi mtu anatembea na rafiki ya mume wake achilia mbali kaka/dada. Na unajua kwa nini sitathubutu, namwoneaga huruma mume wangu naona kama atachoreka, rafiki yake/kaka yake/ mdogo wake anifanyie kama yeye anavyonifanyia, halafu ikitokea siku moja tuwe wote hapo yaani mume wangu na huyo mwizi, naona kama baba D wangu atakapokuwa anaongea kitu chochote hata kama kina point huyo mwizi atakuwa anawazia kichwani kwake, haaahhh wapi wewe kitu gani? unachokulaga na mimi ndo hichohicho ninakula sasa kama ni kitamu au ni kichungu mmhhh!!!! Hapana sijisikii vizuru kabisa kutenda hichi kitu kwa mtu wetu wa karibu ambaye najua kwa vyovyote vile ipo siku tutajumuika wote watatu, sitaki na nakemea kwa jina la YESU huyu pepo apishe mbali kabisa na upeo wa macho yangu.
Mkuu hili siyo swali la kizushi, yapo na yanatokea japo ni kwa uchache sana.
Niliwahi kusikia kutoka kwa mtu ninaye mwamini, yupo. Hawa walikuwa na mazoea toka utotoni, kaka na dada wanalala kitanda kimoja, wanaoga pamoja na walikuwa na ukaribu sana. Huo mchezo walianza enzi za utoto na walipokuwa wakubwa bado wanaendelea.
Mbaya zaidi jamaa kaoa na dada yake kaolewa, wakikutana huwa wanakuwa karibu sana na hata wanajifungia. Wifi yake huwa hana wasiwasi nao hajui nyuma ya pazia kuna nini.