Swali la kufikirisha: Kwanini wapinzani na wanaharakati tu ndio wanauawa na "wasiojulikana"?

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Tangu kazi ya kuteka na kuua raia ianze katika nchi hii, sijawahi kusikia kada wa CCM kapotezwa na kukutwa ameuawa. Ijapokuwa mauaji kwa njia ya kuteka yalikuwepo tangu awamu ya kwanza lakini nimejaribu kuvuta kumbukumbu zangu sijapata jina la kada hata mmoja wa CCM aliyewahi kutekwa na kuuawa. Kama kuna mtu anamfahamu walau kada mmoja tu wa CCM aliyewahi kutekwa na kuuawa, basi amtaje hapa.

Hili ndilo swali hasa linalofikirisha. Ikiwa utekaji na uuaji huu ni wa kawaida tu, kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha, inakuwaje wapinzani, wakosoaji wa serikali na wanaharakati ndio wauawe tu?

Hii inafikirisha na kutia wasiwasi sana, hasa tukikumbuka matamko mbalimbali yaliyowahi kutolewa hadharani na makada wa CCM kuhusu kuwashughulikia wapinzani na wale wote wanaoipinga au kuikosoa serikali yao.

Idadi ya makada wa CHADEMA na wanaharakati waliouawa au kunusurika kuua haina idadi. Tukianzia kwenye kifo cha Dr Mvungi, kutekwa kwa Sativa na Roma mkatoliki, kuuawa kwa mzee Kibao na kunusurika kifo kwa Tundu Lissu, utaona orodha inaziki kuongezeka tu kila kukicha. Wanaolengwa ni wapinzani tu au wakosoaji wa serikali.

MAONI YANGU
Kama haya mauaji yangekuwa ya kawaida, ni dhahiri yangehusisha makada wa vyama vyote vya siasa na raia wote wa nchi hii bila ubaguzi wowote. Kinyume na hayo, yawezekana haya ni mauaji ya kupangwa na wanaoyaoanga wana mbinu kali sana zinazo2afanya wafaniki2e katika utekaji wao. Tukae chini tujiulize: kwanini haya mauaji yanalenga kikundi cha watu fulani tu? Haya ni zaidi ya mauaji ya kigaidi yanayofanywa na alqaeda na vikundi vingine vya kigaidi. ICC wasipochukua hatua za haraka kukomesha ushenzi huu, tutarajie wapinzani na wanaharakati kuendelea kutekwa na kuuawa na "watu wasiojulikana" hadi kiama.
****************************
Pia soma:
PETER MSIGWA KWA SASA NI CHANZO CHA KUAMINIKA NA VYOMBO VYA USALAMA

#WAMEMUA MZEE KIBAO KWA TAARIFA FEKI ZA PETER MSIGWA

Wiki iliyopita jeshi la Polisi lilitoa tarifa kwamba viongozi wa CDM wamekaa na kupanga kuchoma vituo vya Polisi nchi nzima kama njia ya kushinikiza kuachiliwa huru kwa Mwenyekiti wa BAVICHA Temeke, Deusdedith Soka na wenzake wawili ambao walitekwa na watu wasiojulikana. Polisi walisema taarifa hizo ni za UHAKIKA na zimetoka kwenye chanzo cha kuaminika.

Sasa unajua chanzo chenyewe ni kipi? Ni P.M . Hiki ndio chanzo chao cha "kuaminika" ambacho Polisi walikitumia. Iko hivi, Samia aliagiza Msigwa apewe attention na vyombo vya ulinzi kwani ana taarifa nyeti za ndani ya CDM kwa sababu alikua mjumbe wa kamati kuu.

Sasa wiki iliyopita Msigwa akaviambia vyombo vya usalama kwamba CDM wamepanga kulipua vituo vya polisi nchi nzima. Akasema viongozi wakuu wa CDM walikaa kikao kupitia Zoom na kukubaliana kuunda vikundi vya vijana kukamilisha mpango huo. CDM walikanusha taarifa hizo na kudai kama Polisi wana ushahidi wauweke hadharani. Polisi walishindwa kufanya hivyo.

P.M aliviambia vyombo vya usalama kuwa anayeratibu zoezi hilo la kuchoma vituo vya polisi ni Mzee Ali Mohamed Kibao. Kwa wasiomjua Mzee Kibao alikua mwanajeshi wa JWTZ. Ni strategist mzuri kwenye medani za vita na ameshiriki mission mbalimbali za kijeshi kama vile Lebanon, DRC, Comoro etc. Baada ya kustaafu jeshi alijiunga na CCM akawa Katibu wa CCM jiji la Tanga. Baadae aliondoka CCM na kujiunga na CDM ambapo alikua mjumbe wa sekretarieti na strategist wa chama.

Sasa P.M akatumia hicho kama kigezo cha kuaminisha TISS kwamba mzee Kibao alipewa jukumu la kuorganize vijana nchi nzima ili waanzishe vuguvugu kama la Gen-Z wa Kenya lengo likiwa kuchoma moto vituo vya polisi na kuleta machafuko. Kuanzia hapo ndipo mzee Kibao akaanza kufuatiliwa kabla ya kutekwa na kuuawa kikatili.

P.M amewataja watu wengine anaodai walikua wanashirikiana na mzee Kibao kwenye mpango wa CDM wa kuchoma moto vituo vya Polisi ambao ni Boniface Jacob, Martin Maranja Masese, Tito Magoti, Godbless Lema, Maria Sarungi, Fortunatus Buyobe, Godlisten Malisa, Peter Madeleka, John Pambalu, Onesmo Olengurumwa (huyu ni kwa sababu ya issue ya Ngorongoro), Ananilea Nkya, Bob Wangwe, Yericko Nyerere, Kumbusho Dawson. Hawa wote wapo kwenye targets za kutekwa waambieni wawe makini.

Ameandika Simion toka DC Washington
 
Tangu kazi ya kuteka na kuua raia ianze katika nchi hii, sijawahi kusikia kada wa CCM kapotezwa na kukutwa ameuawa. Ijapokuwa mauaji kwa njia ya kuteka yalikuwepo tangu awamu ya kwanza lakini nimejaribu kuvuta kumbukumbu zangu sijapata jina la kada hata mmoja wa CCM aliyewahi kutekwa na kuuawa. Kama kuna mtu anamfahamu walau kada mmoja tu wa CCM aliyewahi kutekwa na kuuawa, basi amtaje hapa.

Hili ndilo swali hasa linalofikirisha. Ikiwa utekaji na uuaji huu ni wa kawaida tu, kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha, inakuwaje wapinzani, wakosoaji wa serikali na wanaharakati ndio wauawe tu?

Hii inafikirisha na kutia wasiwasi sana, hasa tukikumbuka matamko mbalimbali yaliyowahi kutolewa hadharani na makada wa CCM kuhusu kuwashughulikia wapinzani na wale wote wanaoipinga au kuikosoa serikali yao.

Idadi ya makada wa CHADEMA na wanaharakati waliouawa au kunusurika kuua haina idadi. Tukianzia kwenye kifo cha Dr Mvungi, kutekwa kwa Sativa na Roma mkatoliki, kuuawa kwa mzee Kibao na kunusurika kifo kwa Tundu Lissu, utaona orodha inaziki kuongezeka tu kila kukicha. Wanaolengwa ni wapinzani tu au wakosoaji wa serikali.

MAONI YANGU
Kama haya mauaji yangekuwa ya kawaida, ni dhahiri yangehusisha makada wa vyama vyote vya siasa na raia wote wa nchi hii bila ubaguzi wowote. Kinyume na hayo, yawezekana haya ni mauaji ya kupangwa na wanaoyaoanga wana mbinu kali sana zinazo2afanya wafaniki2e katika utekaji wao. Tukae chini tujiulize: kwanini haya mauaji yanalenga kikundi cha watu fulani tu? Haya ni zaidi ya mauaji ya kigaidi yanayofanywa na alqaeda na vikundi vingine vya kigaidi. ICC wasipochukua hatua za haraka kukomesha ushenzi huu, tutarajie wapinzani na wanaharakati kuendelea kutekwa na kuuawa na "watu wasiojulikana" hadi kiama.
Hukuwahi kusikia mauji ya kibiti, rufiji na mkuranga, waluliwa viongozi na makada wengi wa CCM ila serkali iliweza kukomesha yale mauji na kutoa matamko makali sana ila kwenye ilivwanakuwa kama wamepararize
 
Mimi naongelea mauaji ya kueka mtu mmoja mmoja na kumpoteza jumla au kumuua kama ilivyotokea kwa Ben Saanane, Sativa, kamanda Mawazo na mzee Kibao. Sio mauaji ya halaiki kama ya Kibiti mkuu.
 
Kuna mchungaji kawapa za uso watawala kwa haya mauji mpaka nimeshindwa kuamini hiyo clip.

Mama kapewa makavu live kuhusu uatawala wake.

Clip iko katika akaunti ya Martin Maranja Masese kwenye mtandao wa X.

Mchungaji hajamungunya maneno hata kidogo.

Juzi niliweka uzi hapa nikisema kuteka na kuua watu, hakuwafanyi watu kuwa waoga, bali huwafanya watu kuwa majasiri na kuona hawana tena cha kupoteza kama wenzao wanakufa.
 
Tangu kazi ya kuteka na kuua raia ianze katika nchi hii, sijawahi kusikia kada wa CCM kapotezwa na kukutwa ameuawa. Ijapokuwa mauaji kwa njia ya kuteka yalikuwepo tangu awamu ya kwanza lakini nimejaribu kuvuta kumbukumbu zangu sijapata jina la kada hata mmoja wa CCM aliyewahi kutekwa na kuuawa. Kama kuna mtu anamfahamu walau kada mmoja tu wa CCM aliyewahi kutekwa na kuuawa, basi amtaje hapa.

Hili ndilo swali hasa linalofikirisha. Ikiwa utekaji na uuaji huu ni wa kawaida tu, kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha, inakuwaje wapinzani, wakosoaji wa serikali na wanaharakati ndio wauawe tu?

Hii inafikirisha na kutia wasiwasi sana, hasa tukikumbuka matamko mbalimbali yaliyowahi kutolewa hadharani na makada wa CCM kuhusu kuwashughulikia wapinzani na wale wote wanaoipinga au kuikosoa serikali yao.

Idadi ya makada wa CHADEMA na wanaharakati waliouawa au kunusurika kuua haina idadi. Tukianzia kwenye kifo cha Dr Mvungi, kutekwa kwa Sativa na Roma mkatoliki, kuuawa kwa mzee Kibao na kunusurika kifo kwa Tundu Lissu, utaona orodha inaziki kuongezeka tu kila kukicha. Wanaolengwa ni wapinzani tu au wakosoaji wa serikali.

MAONI YANGU
Kama haya mauaji yangekuwa ya kawaida, ni dhahiri yangehusisha makada wa vyama vyote vya siasa na raia wote wa nchi hii bila ubaguzi wowote. Kinyume na hayo, yawezekana haya ni mauaji ya kupangwa na wanaoyaoanga wana mbinu kali sana zinazo2afanya wafaniki2e katika utekaji wao. Tukae chini tujiulize: kwanini haya mauaji yanalenga kikundi cha watu fulani tu? Haya ni zaidi ya mauaji ya kigaidi yanayofanywa na alqaeda na vikundi vingine vya kigaidi. ICC wasipochukua hatua za haraka kukomesha ushenzi huu, tutarajie wapinzani na wanaharakati kuendelea kutekwa na kuuawa na "watu wasiojulikana" hadi kiama.
1. Hii ni kutokana na nchi kuwa na Mifumo au Utaratibu wa Ujasusi wa Kidola. Nchi ambazo Zina Tawala zenye itikadi ya Ukomunisti/Ujamaa, huwa kunakuwa na mifumo ya Ujasusi wa kidola, Katika mfumo huu, Watu Wakosoaji wa Utawala uliopo Madarakani au wanaharakati wanaokosoa au kupinga Watawala huwa wanahesabika kuwa ni maadui wakubwa zaidi wa Utawala uliopo madarakani. Hivyo, wakosoaji wa Utawala huwa wanakuwa ni walengwa wakubwa zaidi wa vitendo vya utejaji na Mauaji vinavyofanywa na wadhalimu au 'mawakala wa siri wa watawala.' Mifano hai ipo mingi sana hapa duniani hususani kwenye hizi nchi zenye tawala ambazo Zina itikadi za vinasaba vya Ukomunisti/Ujamaa kama vile Tanzania, Urusi, China, Belarus na nchi zingine nyingi sana za Kiarabu, e.g. Iran, Saudi Arabia, n.k.

2. Yupo mwanaCCM mmoja pia aliwahi kutekwa na kupotezwa hadi leo hajawahi kupatikana, ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya huko mkoani Kigoma, sikumbuki Jina lake.
Lakini hata yeye naye sababu za kutekwa kwake inasemekana kuwa ni 'alikuwa mpinzani ndani ya CCM.'
 
Wanataka wote wawe CHAWA au NDIYO NDIYO tu! Kitu ambacho ni ngumu sana katika Dunia ya Utandawazi.
 
MaCCM yanataka kila mtu awe chawa wao wawatawale kwa urahisi.
 
Mimi swali langu imekuaje huyo P.M , amuuze mzee KIBAO kwa taarifa za uongo kwani alimfanyaje?
 
1. Hii ni kutokana na nchi kuwa na Mifumo au Utaratibu wa Ujasusi wa Kidola. Nchi ambazo Zina Tawala zenye itikadi ya Ukomunisti/Ujamaa, huwa kunakuwa na mifumo ya Ujasusi wa kidola, Katika mfumo huu, Watu Wakosoaji wa Utawala uliopo Madarakani au wanaharakati wanaokosoa au kupinga Watawala huwa wanahesabika kuwa ni maadui wakubwa zaidi wa Utawala uliopo madarakani. Hivyo, wakosoaji wa Utawala huwa wanakuwa ni walengwa wakubwa zaidi wa vitendo vya utejaji na Mauaji vinavyofanywa na wadhalimu au 'mawakala wa siri wa watawala.' Mifano hai ipo mingi sana hapa duniani hususani kwenye hizi nchi zenye tawala ambazo Zina itikadi za vinasaba vya Ukomunisti/Ujamaa kama vile Tanzania, Urusi, China, Belarus na nchi zingine nyingi sana za Kiarabu, e.g. Iran, Saudi Arabia, n.k.

2. Yupo mwanaCCM mmoja pia aliwahi kutekwa na kupotezwa hadi leo hajawahi kupatikana, ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya huko mkoani Kigoma, sikumbuki Jina lake.
Lakini hata yeye naye sababu za kutekwa kwake inasemekana kuwa ni 'alikuwa mpinzani ndani ya CCM.'
Asante kwa mchango huu mkuu. Mchango wako huu umenifanya nimkumbuke @yerickna kitabu chake cha Uasusi Wa Kdola.
 
Back
Top Bottom