Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Mkuu, pole kwa msiba huu mkubwa. Hata kuwa alikuwa mzima ilikuwa ni uzushi tu - ukweli (ambao haukuhitaji kutetewa kwa uongo ni kuwa alikuwa na tatizo la moyo). Mungu mwenye rehema aitunze roho ya marehemu.
 
Anapiga kazi eeh ?

Aibu yetu aibu yao?
 
Point

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu,
Au alikuwa mwongo aliposema kauli hii?
Mbona mapema Sana kumsahau?
 
Mkuu ukweli lazima usemwe bila kujali wale watakaoumizwa na ukweli huu.
Mkuu Mr Dudumizi , I'd like to differ, sio kila ukweli ni lazima usemwe, ukweli mwingine ni ukweli mchungu wa hatari, ukisemwa badala ya kujenga, unabomoa!. Ukweli ambao ni lazima usemwe ni ule ukweli ambao ukisemwa utasaidia. Hivyo kabla ya kuusema ukweli wowote, unaufanyia objectivity test kwa kujiuliza, jee ukweli huu ukisemwa utasaidia?, utayajenga au utabomoa na kuharibu?. Je ukweli huo una maslahi kwa taifa au majanga?. Baada ya kupata majibu hayo, unajifanyia self censorship na kumua au kusema au kunyamaza na kupotezea!.

P
 
Vitu vingine siyo lazima kuandika. Kuna ulazima gani kuandika Kila wakati na Kila kitu unachohisi?.
Naunga mkono hoja.
P
 
Jana kule jijini Brussels nchini Ubeligiji, Rais Samia amekutana na Tundu Lissu kwa mazungumzo yalliyodumu kwa takriban saa nzima. Taarifa rasmi ya Ikulu ikaeleza rais Samia amefanya mazungumzo na Lissu bila kuweka details wamezungumza nini, hivyo Tundu Lissu alipaswa to replicate by doing the same. Kwanini Lissu ameropoka mazungumzo ya wawili hao?. Japo yote laliyozungumza ni kweli, why did Lissu had to reveal mambo waliongea na rais in confidence?. Alichofanya Lissu ni a breach of confidence, this shows this is not a man to be trusted!. Ni mropokaji mpaka basi!.

Mimi ni miongoni mwa tuliomchagiza Lissu agombee urais 2020, kuna sifa yake moja mimi nilisema kwa Lissu ni zaidi ya JPM
Sikumalizia ni kwenye nini, nilikuwa na maana yangu.

Nikadhani kwa vile sasa huyu mtu almeishi ulaya, atakuwa amestaarabika...kumbe wapi!.

Sio lazima kusema kila kitu!. kiukweli Lissu akijirekebisa hii tabia ya uropokaji na kui control, 2030 he can make a very serious contender kwenye urais.
P
 
Hatuna haja na thread zako za kinafiki unazoungaunga kutafuta huruma ya wanaJF. Ulitaka asitoe tips za alichoongea ili Leo muanze kutoa ya kwenu vichwani? Amesema tu mmeanza kubadilisha eti kaomba msamaha, aaingesema si ndo mngeongeza uzushi juu ya uzishi?
LISSU anawajua vizuri CCM ukiwemo wewe Ndumilakuwili mgomvi wa Ndugai.
 

Paul, una right ya kuzungumzia unachotaka lakini pia sidhani una uhalali wa kusema kipi kingekuwa hivi ama vile. Kuna tabia ya kuhodhi taarifa imejitokeza Tanzania. Utakumbuka hata ni taarifa gani inatoka lilikuwa ni jambo lililodhibitiwa sana kipindi cha JPM. Kupata taarifa (za ukweli) ni haki ya kila mtu.

Pamoja na kwamba hujaeleza hapa kama Lissu alizuiwa kutotoa taarifa lakini ametaja tu mambo aliyosema kwa Rais. Hakufikia kusema "... Rais kasema atafanya hiki na kile ....."! Je unapendekeza kwamba mazungumzo yao yasingekuwa reported kabisa hata kwa Chadema? Ni vipi kama habari za mazungumzo yao vingesemwa na Mwenezi wa Chadema - si ungechukia zaidi??

Hiyo unayosema kustaarabika kwa kuishi Ulaya nadhani ni misstep kwa upande wako. Huko Ulaya hutoa taarifa za kuwepo kwa mazungumzo na ni mambo gani yamezungumzwa - huwa hawatoi ni mambo gani yamekubalika. Ndipo husikia habari za kuundwa kwa task force kushughulikia jambo, au kukutana tena baada ya miezi kadhaa kuzugumza. Hawafanyi unachopendekeza hapa - kunyamaza na kuficha!!!

Kwa wanaChadema yaliyosemwa ni mambo muhimu. Kwa wanaCCM yaliyosemwa ni maudhi, ninalewa uchungu wako kwa sababu ni mambo ambayo ungependa yasizungumzwe hadharani ili kuwe na nafasi kuwa hayakuwahi kuzungumzwa. Kwa neutrals kama mimi - kilichofanyika ni sahihi. Nimepata kujua zaidi ya kulikuwa na mazungumzo, ninajua sasa Lissu aliyeomba kukutana na Rais, alizungumza nae mambo gani.
 

Kuna “UKWELI” na kuna “UKWELI MTUPU”...Ukweli unaweza kusemwa wote ila sio ukweli mtupu
 
Kwa maoni yangu, Tundu Lissu anahitaji ushauri nasaha. Binadamu ukipitia maswahibu na mapito kama aliyopitia, unaathirika ki fizikia, ki emosheni na kisaikolojia, (physical, emotional and psychological), hivyo anahitaji ushauri nasaha jinsi ya kutoka kwenye jinamizi hili na kuendelea na maisha.

Huku kutaja taja majina ya watu, na kutangazia ulimwengu kuwa vyombo vyetu tukuka vya ulinzi na usalama kuwa ndio walio husika, shambulio lake, bila ushahidi wowote, ni kuzidi kuibagaza tuu nchi yetu!.

Ametaja Kikosi kazi kinachojumuisha Polisi, JWTZ na TISS,, hawa ni askari wetu, trained, how could they do such a messy dirty job?. Kwa trained snipers, only one single shot would have finished the job!. Hili hata Mama Samia amewahi kuizungumzia, askari wetu trained wakimiss target by two shots, wanaandika maelezo kujieleza!.

Mimi kwa upande wangu naendelea kusisitiza Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Pia Lissu niliisha mshauri na namshauri tena, ajifunze kunyamaza.


Kitendo cha Rais Samia kukubali kukutana na Lissu ni uthibitisho tosha wa kauli na matendo she is healing this nation.

kwenye bandiko hilo nilisema
Lissu ajifunze kunyamaza
P
 
You're such a disgrace.
 
hakuna uovu unaojenga taifa, hakuna uongo mzuri kaka, kama hakg ndio huinua taifa kwenye haki hakuna uongo nikweli maendeleo nimaslahi ya taifa, je' kila unapotaka mafanikio ni lazima uumize watu? unaweza tenda haki kwa kuvunja miongozo mliojiwekea? ukweli nikwawapenda haki ndomana ccm ya zamani waliliona hilo kwamba watakua wakweli daiama nakamwe hawatasema uongo maana kwao uongo ulikua mwiko, kaka p'hakuna uongo unaojenga taifa ukiona mtu anautetea uongo au maovu kwa kisingizio cha maendeleo huyo nimharifu kama waharifu wengine, hata katika vyombo vya kutoa haki watu wanaapa kusema ukweli ili haki itendeke huku wakimwomba mungu awasaidie''kila uongo lazima usemwe ili kukomesha ubaya''
 
Mkuu Pulchra Animo , naunga mkono hoja, hata kama kweli ni ukweli, lakini sio lazima kila ukweli lazima usemwe, ukweli mwingine sio lazima usemwe, unapaswa kufanya kitu kinaitwa objectivity test ya kuupima jee ukweli huo ukisemwa unajenga au unabomoa, ukiona ukweli huo unabomoa, then it's better ukweli huo usisemwe indefinitely.


P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…