Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

1. Nguvu ya Ukweli
Katika maadili ya msingi, ukweli una nafasi ya kipekee. Kuusema ukweli kunaleta uwazi, uwajibikaji, na imani katika jamii.

Ukweli unaofichua ufisadi, ukiukwaji wa haki za binadamu, au njama zinazohatarisha maisha ya watu wengi unapaswa kusemwa bila kuzingatia maslahi binafsi au ya kundi fulani.

2. Maslahi ya Taifa ni Nini?
Maslahi ya taifa mara nyingi hurejelea ulinzi wa ustawi wa jumla wa raia, usalama wa kitaifa, na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Wakati mwingine, kinachotajwa kuwa maslahi ya taifa huweza kutumiwa vibaya kuficha maovu, ufisadi, au udhalimu.

3. Je, Ukweli na Maslahi ya Taifa Hupingana?
Katika muktadha maalum, kunaweza kuwa na mvutano kati ya kusema ukweli na kulinda maslahi ya taifa.

Kuna nyakati ambapo kusema ukweli kunaweza kuhatarisha usalama wa taifa, kama katika masuala ya kijeshi au diplomasia nyeti. Katika hali kama hizo, maslahi ya taifa yanaweza kupewa kipaumbele.

Katika hali ambapo maslahi ya taifa yanapotoshwa na kundi la watu wachache wenye mamlaka, kusema ukweli ni muhimu ili kurejesha haki na uwajibikaji.

a) Kuchagua Wakati na Namna ya Kuusema
Ukweli unaweza kusemwa kwa namna inayolinda maslahi ya taifa huku ukiendeleza uwazi.
Kwa mfano, kutumia vyombo vya sheria au taratibu za siri kuufichua ukweli unaohusiana na masuala nyeti.

b) Uwajibikaji wa Kiutu na Kiadili
Ni muhimu kutafakari madhara ya kusema au kuficha ukweli kwa mtu binafsi, jamii, au taifa zima.

Uamuzi unapaswa kujengwa juu ya dhamira ya kulinda haki za msingi za watu.

4. Ni Lazima Kuusema Kila Ukweli?
Sio kila ukweli unapaswa kusemwa bila tafakuri. Kiongozi wa maadili anapaswa kuzingatia yafuatato;

Je, utasaidia jamii au yatazidisha migawanyiko?
Je, kuficha ukweli kutasaidia ustawi wa taifa kwa jumla?

Kwa hivyo, ni muhimu kuutazama ukweli kwa muktadha wake. Ukweli unaopigania haki, uwazi, na maendeleo ya taifa unapaswa kusemwa.

Hata hivyo, pale unapoathiri maslahi mapana ya usalama wa kitaifa, busara inahitajika katika namna unavyoshughulikiwa.

Ova
 
Wanabodi.

Kama kawaida yangu, kila nikipata muda, nashuka na zile makala zangu elimishi za KMT - "Kwa Maslahi ya Taifa". Mada ya leo ni swali la kitu kinachoitwa "morality": "Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia?.

Na tukija kwenye medani za siasa, kabla ya kuusema ukweli wowote tunaousikia, je ni lazima tuseme tuu kila kitu tunachokisikia au kwanza, tutangulize mbele maslahi ya taifa kwa kujiuliza kwanza, hicho unachotaka kusema kina maslahi kwa taifa?, na unatakiwa kuupima kwanza huo ukweli kwa kujiuliza, je, ukweli huu ukijulikana una matokeo gani kwa taifa?, ndipo tuuseme, au tuendelee tuu na hii tabia ya kusema kila kitu unachokisikia?. Ukisikia jambo lolote, wewe liseme tuu bila kujali jambo hilo linamatokeo gani as long as jambo hilo ni la kweli?.

Na ili kupata manufaa ya kisiasa, je ni lazima wanasiasa wetu, wapoliticise kila kitu?, kila jambo? na kila tukio?.

Declaration of interest.
Mimi Paskali ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na kanuni kuu ya kwanza ya mwana habari, (cardinal rule ni " tell nothing but the truth, no matter what!", lakini before telling the truth, mwandishi anatakiwa kutumia kitu kinachoitwa "objectivity test" yaani kuwa objective kwa kuupima ukweli huo una faida au manufaa gani kwa jamii, taifa na mhusika?.

Hivyo mimi as a journalist ni mtu mkweli daima, na ni muumini wa ile ahadi ya mwana TANU ya " Nitasema kweli daima, fitna kwangu mwiko", ila katika kuusema ukweli au kuandika ukweli, nasema na kuandika kwa kutumia kitu kinachoitwa responsible journalism kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, kabla sijaandika, ninajiuliza kwanza, je ukweli huu ukisemwa, utajenga, au utabomoa?.

Ukisikia jambo, au ukiona jambo, japo ni ukweli lakini kama ukweli huo, ukijulikana, badala ya kujenga, utabomoa, then ukweli huo, siusemi. Huu ndio uzalendo wa kweli wa taifa lako kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Mfano mzuri ni kwenye issue ya JPM, kuna ukweli fulani niliowahi kuusikia kumhusu JPM, hivyo niliposikia anaweza kuja kuwa rais wa JMT, niliusema kwenye bandiko hili
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe ...
Kwenye bandiko hilo kuna kitu nilisema nitakisema, mwisho wa siku, sikukisema!. Na baada ya JPM kuwa rais wa JMT, kuna siku nilikiulizia, Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko? nikakuta hakuna anayekijua. Kwa vile sasa tayari JPM ndie rais wetu, ukweli huo ninaoujua ukijulikana, hautasaidia kitu, sio tuu, haujengi bali unabomoa, hivyo siusemi kabisa, lakini ili kuzuia jambo kama hili lisijirudie in future, nilitoa ushauri Ili kuepuka possibility ya kutawaliwa na wageni, kuna haja kutumia DNA kuthibitisha asili halisi za viongozi wetu wakuu?
Sometimes ukweli too much unaponza!.


Hii Kamata Kamata ya Kila Waompinga Magufuli, Ni Magufuli Anawatuma au Polisi Wanajipendekeza Tuu?.
My honest opinion, ingawa ni kweli rais Magufuli hapendi critics, mimi nilimsikia mwenyewe kwa masikio yangu toka kwenye kinywa chake na sio kwa kuhadithiwa, alisema anapenda challenge, ila hizo challenge ziwe ni ukosoaji wa kweli wenye nia njema, hivyo naamini hizi kamata kamata zinazoendelea za kuwakamata karibu kila wanasiasa wanaompinga rais Magufuli, siamini kama ni Magufuli anawatuma!, naamini hivyo ni kazi ya polisi wetu ambao wana jikomba komba tuu ili kuonekana wanafanya kazi.

Kwenye siasa za multipartisim duniani kote, kazi ya the opposition ni kupinga, kuopose kila kitu kinachofanywa na chama tawala hata kiwe ni kitu kizuri namna gani!, that is their right, kupinga, ndio maana wanaitwa wapinzani. Na serikali zote zinazoheshimu demokrasia ya kweli, lazima zikubali kupingwa.

Nimeishi kidogo UK, US, na Uswiss. Uingereza pale Times Squire karibu kila siku ni maandamano. US ule mtaa jirani na Capitol Hill kuna uwanja unakuwa huru kupinga chochote, Uswiss uwanja huru wa kupinga, ni pale uwanja wa wazi nje ya ukumbi wa Bunge, the The Bundes House. Hivyo sioni mantiki ya sababu zozote wanaompinga rais kubughudhiwa!, this is not democracy, Tanzania sio nchi ya kidikiteta!, tena kiukweli, kama katiba yetu imeruhusu mikutano na maandamano, hakuna any justified reasons at all za rais Magufuli kupiga marufuku, ni ukiukwaji wa wazi wa katiba ya JMT, but to be honest, yeye kama rais wa JMT kwa mujibu wa katiba yetu, hana mamlaka ya kuzuia jambo lililoruhusiwa na katiba, and he gas nothing to loose akiruhusu mikutano na maandamano.

Wito kwa IGP, Kamanda Sirro, controll vijana wako watekeleze majukumu yao kwa sheria taratibu na kanuni na sio kwa kutaka kujipendekeza au kujikomba komba!.
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako ...
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti ...


Jee Wapinzani Kazi yao ni Kupinga Tuu Kila Kitu au Kukosoa Tuu Hakuna Kupongeza Hata kwa Mazuri?.
Japo kazi ya upinzani ni kupinga na kukosoa, lakini tunapokuja kwenye issues muhimu kwa maslahi ya taifa, maslahi yataifa ndio yanatangulizwa mbele, sisi sote kama Watanzania, we stand as one, tunakuwa kitu kimoja, tunakuwa watu wamoja, tunaweka mbembeni tofauti zetu za kisiasa, hakuna tena siasa za vyama, wala siasa za watu, tunaweka pembeni siasa, tunaitanguliza mbele Tanzania, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, we stand as one, na kila kitu kinafuatia baadae.

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie ...
Kwenye Haki za Wanyonge, Magufuli ni Kama Khalifa Mkuu Harun El ...


Mfano mwingine wa kuujua ukweli fulani na kutousema ni ukweli huu nilio uandika kuhusu Bunge letu tukufu. Kwanza niliandika Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?, kisha nikaandika Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali? Bunge likakasirika, nikaitwa Bungeni kuhojiwa na Kamati Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge nilihojiwa Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge na baada ya mahojiano, Bunge walinyamaza kimya, na mimi kuna ukweli niliwaambia ukawaingia wakanyama kimya na mimi sikuwahi kusema kilitokea nini kule , nimenyaza mpaka leo mpaka kesho, kwasababu sio lazima kila ukweli usemwe, ukweli mwingine ukijulikana ni aibu!. Ukweli mwingine una bagaza, na hausaidii chochote!.

Hata lile tukio la Machi 17, kuna watu tunajua lilitokea lini na Jamaa alichomoka kwa ugonjwa gani!, lakini kwa vile tumetangaziwa ni tarehe 17 na ugonjwa ni ule, japo ukweli tunaujua, lakini hatuusemi!. Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?
Conclusion
Namalizia kwa haya maswali ya msingi, kuhusu ni hoja za morality kusema kweli daima, lakini je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia?. Kwenye medani za siasa, kabla ya kuusema ukweli tunaousikia, je tutangulize kwanza mbele maslahi mapana ya taifa kwa kuupima kwanza, ukweli huo una matokeo gani, ndipo tuuseme, au tuendeleze kusema tuu, kupayuka na kuropoka kila ukisikia lolote, lisema tuu kwa sababu ni la kweli?. Je Ili kupata manufaa ya kisiasa, je ni lazima wanasiasa wetu, tupoliticise kila kitu?.
Wito wangu ni sio lazima kusema kila unachosikia hata kama ni cha kweli!, tujifunze kunyamaza, ukimya nao ni jibu!.

Wasalaam.

Paskali

Rejea.
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or ...
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public ...
Je, wajua amri za Rais sio final and conclusive?. Zinaweza kupigwa ...
Tusimlaumu Rais Magufuli Kwa Kila Kosa, Rais Yeye Hana Kosa Bali ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...
Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni ...
Kitendo cha kuita nchi majirani zako kuwa ni "vinchi" ni uungwana ...
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hoja ya Udikiteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi ...
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio ...
Ukweli ukisha Julikana kwa watu zaidi ya wawili unakuwa huwezi kufichika tena. Ni bora ukasemwa kama ulivyo maana usipo semwe na wanao ujuwa vizuri ipo siku utasemwa na wasio ujuwq vizuri Kwa masilahi yao . Na unaweza ukaleta madhara makubwa kwa taifa kuliko kama ungesemwa mapema. Kwa mfano Magufuli kuna watu wengi walijuwa anatatizo la akili na alikuwa sio raia lakini kwa sababu ya masirahi yao binafusi wakaamuwa kukaa kimya. Matokeo yake ni taifa zima kuteswa kwa miaka sita. Na watu zaidi ya elf kupotea . Kumbe watu wangekuwa na uwezo wa kusema ukweli huenda hata ubunge asinge upata.
 
Back
Top Bottom