Swali la mwaka: Nani alimleta Ballali nchini?


WB ndio walimpendekeza Ballali ili aweze kutekeleza mabadiliko ya kitaasisi kuwezesha utekelezaji wa sera zao mufilisi za SAP...

Tanzanianjema
 
Jamani samahanini kidogo, hivi Ruhinda ni mtu wa wapi? Alishawahi kuwa mbunge hapa Tanzania? Maana kuna mtu nimesikia amesema kuwa jamaa ni mtu wa Bukoba lakini pia kuna mtu niko nae hapa ameniambia jamaa ni mtu wa Mwanza na alishawahi kuwa mbunge... Kuna ukweli?
 
- Mkapa ni fisadi period kwa wale msiomjua vizuri, pale Tanesco kulikuwa na jamaa yangu ambaye pia anamiliki FM Academia "Wazee wa Mujini", huyu jamaa alikuwa mkurugenzi wa kitengo Tanesco, yalipokuja ya Netgroup aliandika paper ndefu sana kuikataa kabisa na kutoa sababu nyingi za kumsingi, Mkapa alipewa copy ya hiyo paper, aliwaamuru uongozi wa juu Tanesco kuomuondoa mara tu opportunity itakapopatikana, and yes they eventually did it lakini to this day Mkapa anajua wazi kwamba huyu jamaa ndiye anayejua vizuri sana maovu yote Mkapa aliyoyafanya Tanesco, kwa hiyo kwanza naomba kuweka wazi hapa kwamba huyu Mkapa alikuwa ni fisadi tena wa hatari sana siku zote, ndio maana kwanza Warioba na kamati yake ya rushwa hawakuenda kuchunguza wizara ya zamani ya Mkapa, na ndio maana ili kuficha maovu yake kule Elimu na sayansi akawapandisha vyeo wale wote aliokula nao kule, kina Mahalu na Dr. Bilali.

- Mkapa amekuwa karibu sana na familia tatu za Musoma, katika kutafuta insurance ya ajira zake serikalini, familia za Nyerere, Muganda, na Butiku, kwa muda mrefu sana aliwadaganya sana hizi familia kwamba he was a good man/leader, infact enzi za urais wa Mwinyi, Mkapa alikua haishi kukimbilia Butiama kulia kwa Mwalimu, kuwa Mwinyi na Malecela hawafai. Hizi familia ambazo ndizo zilizokuwa na power kwa muda mrefu sana bongo zikafikia mahali zikamuamini na hata kum-promote apewe urais na hasa Butiku, aliyekua mstari wa mbele sana kumpigia debe kwa Mwalimu, wakakosea wakampa kweli urais the next thing kwa mara ya kwanza akawaonyesha rangi zake za kweli, akawatupa wote nje na kutafuta marafiki wapya kina Ruhinda na Mushi.

- Mkapa akamrudisha Anna Muganda kuwa mshauri wake wa uchumi toka W/B, according to the dataz somehow Mama Anna alishituliwa na watu kuwa urafiki wa Mkapa na mshauri wake wa uchumi haukuwa wa kawaida, mama akaja juu sana ikabidi mshauri aondoke haraka sana, the next thing Ballali ni mchumba wa huyu ex-mshauri wa uchumi wa Mkapa na anakuwa governor BOT sasa the rest of the story unaweza kutumia common-sense ku-figure out how Ballali became a governor ninaamini wote hapa ni watuwazima.

Ila Mkapa, kwa viongozi wanaomjua siku nyingi wanajua kua ni mpenda anasa na mpenda makuu, mwenye majivuno na asiye na utu hata kidogo, ndio maana wajumbe wa NEC kwa kujua hayo walikuwa wakikataa kata kata juhudi zote za Mwalimu, kumfanya Mkapa kuwa mjumbe wa NEC na CC katika kipindi chote cha urais wa Mwalimu, sasa huwezi kusema kwamba eti wa-Tanzania tulikuwa hatumjui Mkapa, ni big hapana, na eti kwamba Mwalimu alikuwa hamjui Mkapa, that is a biggest lie of a century, Mkapa was a better devil kuliko all the other devils as far as Mwalimu was concerned na alikuwa na manufaa makubwa kwa Mwalimu as a person, kama huamini hili tizama Nyerere Foundation ilipo sasa.

Kwenye kumkoma nyani huwa hatumuangalii usoni.
 
FMES, hapo umedatisha. Ana Muganda ndio mastermind wa Ballali kuingia pale BoT.
 
Ndg Mtanzania,
Anaanza na jina (M), anatokea mkoa unaoanza na jina (M), na mimi naanza na Jina (M)ajita basi nakupoa mji MUSOMA ili "M" iendelee kuwa common factor.Kubaali basi na pls pasua jipu.
 
Well, sifa yake inaanza na Sir!.. Naogopa hata kumtaja..
 
Ballali aliletwa na Anna Muganda nchini (ingawa ni raia wa nchi hii). Swali labda lingekuwa nani alimrudisha.

Shinikizo la kupewa Ugavana ulitoka kwa Sir.....

Mwanakijiji nimekujibu?
 
labda swali langu la kwenye kichwa cha habari limekuwa too vague.. ukiingia ndani na kusoma maelezo ya ufafanuzi wa swali hilo bila ya shaka wengi wenu mtapata muelekeo wa jibu ambalo hata mimi nalihofia.
 
labda swali langu la kwenye kichwa cha habari limekuwa too vague.. ukiingia ndani na kusoma maelezo ya ufafanuzi wa swali hilo bila ya shaka wengi wenu mtapata muelekeo wa jibu ambalo hata mimi nalihofia.

Yes too vague! Na sioni kwa nini watu wananajadili hili suala:
1. Ballali ni Mtanzania
2. Mkapa alimjua Ballali siku nyingi kabla hata hajawa Rais. Ballali ni katika wasomi wa kwanza baada ya Uhuru, among mate zake ni Nyirabu, etc etc. Jamal (Amir Jamal) alikuwa personal friend wa Ballali.
3. Kwa wale watanzania waliofanya kazi world-bank na IMF Ballali amekuwa one of their referals.

Issue ya Ballali is complicated, and katika kiswahili kuna msemo huu: "Nyani anapokufa miti yote huteleza".
We know this man and everything will be said, but questions are; Tanzania have been corrupt and will be. Ballali is one of the victims of this vice; which to be uprooted; will need generations!
 
Vstdar mkuu heshima mbele. I stand to be corrected na hapa watu wa usalama wa Taifa wanaweza kutusaidia, lakini nadhani Ballali alitangulia kuja akawa anafanya kazi Ikulu na baadae Anna Muganda akaja nae kama Economic advisor! Hata baada ya kuwa gavana Ballali bado aliendelea kwa muda kufanya kazi Ikulu. It is Ballali who influenced his wife to be, to come home and not vice versa ;ikawa rahisi kwani BWM pia inasemekana alikuwa mdau wa siku nyingi si mnajua tena majina ya Anna yanavyomzingua chinga!! Kwahiyo Mtanzania asipewe mji hata kama ni Mwakaleli.
 
After all this "debate" what then?

Upuuzi mtupu! Why cry over spilled milk? That stuff is done for, kaput, a non-issue, upuuzi etc etc. The question should be: What should I do next? Or, as it is popular in Tanzania: What should the government do next? In management speak: What do we do next? How do we think outside the box and move forward?

Whether who brought Balali in, or what town to be given to release a name etc is utter upuuzi! Mwanakijiji already knew what he was asking but maybe his intentions was to add on another meaningless topic in this forum....

As Kibunango would say: Kazi kweli kweli.....
 
Mwanakijiji swali lako ni zuri sana na gumu.

Kwani nimpongeze aliyemwelezea vema mkapa tuliyempa urais 1995. mara nyingi tumekua tukimlaumu na kumwona huyu mzee ni mwizi na fisadi. lakini ukweli huyu mzee ni kati ya watu waadilifu sana mwalimu aliowaacha serikalini na lifanya kazi kwa makini pamoja na kuwa alikua mlevi. Kasoro yake kubwa ambayo alishindwa kujirekebisha hadi anaondoka kwenye urais ni tabia yake ya kujiamini na kuona wengine kama wajinga ikiwa hajashawishika kwa wanaliona ni sahihi. hii hua ni kawaida ya watu wengi amabo ni bright na wana ufahamu mkubwa wa mambo. ndivyo alivyo mkapa na kawaida hii ilimgharimu sana kuishi na kufanya kazi na wenzake. alikua haoni shida kumgombeza mtu hata mbele za wengine alipoona amefanya ujinga. Pamoja na yote na tukitaka kumtendea haki huyu mzee, tukubali kuwa ni hazina nzuri sana na uchafu mwingi tunaomwona nao umetokana na aliwaamini na tabia yake ya kunyamaza sana katika mammbo ya msingi (nadhani inaendana na tabia ya kiburi na dharau).

Kuna habari isiyothibitishwa kutoka huko jikoni kuwa kati ya vitu vilivyombadilisha sana mkapa ni report ya tume ya rushwa ya jaji warioba. niliambiwa kuwa mkapa alipopelekewa report ile ilimchanganya sana bze kila aliyekuwa anamfahamu kwenye system alikua ndani. karibu watu wote wanaomzunguka walikua ndani ya ile report na akashindwa aanzie wapi. alichofanya aliamua kwenda kulewa na kuiweka kabatini ile report halafu akaanza wimbo mpya kuwa huwezi kumshtaki mtu kwa rushwa kama huna ushaidi wa kisheria. hadi anamaliza uongozi hiyo ndiyo ilikua kauli yake.

Tukirudi kwa balali, ni kweli huyu alikua mchumi tegemezi na mwenye uzoefu wa kuisaidia nchi yetu. kama munakumbuka wakati anachukua ugavana infaltion rate yetu ilikua 30% na aliweza kuishusha (kushirikikiana na idara zingine chini ya mkapa) hadi 6%....one of the lowest in Africa by then. ninashawishika kuwa mkapa hakumteua balali kwa sababu zake binafsi wala za kifisadi...alimteua kwa ujuzi na uwezo wake wa kazi. ni kawaida kwa wanadamu kughafilika wanapoonekana kuwa ni mahiri sana au wao kujiona kuwa wanaaminika sana na jamii...pamoja na sababu zingine naamini Balali aligahfilika kwa njia hii. alifika mahali akaona watu wengine hawajui chochote na wezi wakamwingia kwa kasoro hiyo.

Kua ni nani aliyemleta kwa mkapa, pomoja na kuwa mkapa alimfahamu binafsi lakini inasemekana mama mmoja alijulikana kama Somebody Muganda (na ambaye alikuja kuwa mke wa Balali) ndiye alimwi-introduce Balali kwa mkapa na kuhakikisha anapata ugavana. Huyu mama nadhani twajua kuwa naye ni Big figure huko WB kama siyo IMF....amehusika pia kwenye ufisadi wa meremeta na wengine.

wenye info zaidi watanirekebisha.

herini ya mwaka mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…