Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Nakula nondo huku nazimeng'enya mdogo mdogo 🙏🙏

Nimekuwa Forex Trader kwa miaka 7 na usheee.. hizi nondo zinanipa picha ya hata kinacho endelea sokoni.. shusheni mijadala zaidi
Mimi nipo nasubiri, kueleweshwa zaidi na ndugu yangu Zitto Jr kuhusu uchambuzi wake wa taarifa ya Fitch inayozungumzia hali ya uchumi ya Marekani. Imezungumzia pia suala zima la fedha ya Marekani, uhaba wa bajeti na makusanyo. Kuna mambo mengi sana, hebu tusibiri aje...
 
Mchumi mimi nimekusoma na nimekuelewa sana sanaaa tu. Ila nina mambo 3 tu:

Mosi, Suala zima la takwimu: Sasa naomba unisaidie zaidi kuelewa, INTERNATIONAL MONETARY FUND (IMF), tarehe 25 July walitoa takwimu zao ambazo zimerekebisha makadirio ya uchumi wa Urusi (Estimates) na kusema kwamba uchumi wa Urusi utakuwa kwa asilimia 1.5% kwa mwaka 2023 kutoka 0.7%.

Kumbuka, mwaka 2022 IMF walisema uchumi wa Urusi ungesinyaa (Contraction) kwa asilimia 12% kwa mwaka 2022, lakini kufika mwezi wa September wakarekebisha tena na kusema ungesinayaa kwa asilimia 2.1% tu. World Bank wamesema uchumi wa Urusi utakuwa kwa kasi chanya, japo kiwastani (Positive but modest growth) kwa asilimia 1.2% ifikapo mwaka 2024.

Lakini hebu tuzingatia takwimu basi, mtandao wa CIA unasema kwamba, mwaka 2021 kabla ya vita GDP (Purchasing Power Parity) ya Urusi ilikuwa ni USD Trilion 4, na baada ya vita wakasema ingeshuka hadi kufika USD Trilion 3.9. Ila katika kufunga mwaka 2022 IMF wakasema GDP (In Purchasing Power Parity) ya Urusi imefika USD Trilioni 5.51 ambayo ni kubwa kuliko Ujerumani ambayo ni USD Trilioni 5. Mtandao wa CIA, unasema hivi:

View attachment 2709542

Hii ni mwaka 2021, na ila sasa WB na IMF wanasema mwaka 2022 imefikia USD 5.51 Trilion. Sasa nachoomba kufahamu ni hiki, umezungumzia, DATA INTEGRITY, ila hizi takwimu zimetolewa na IMF na WB, je tusizitegemee na kuziamini kwasababu zimetolewa na Urusi yenyewe, ???

Pili, nimesoma makala ya, The Wall Street Journal, la tarehe 2 AUGUST 2023, kwenye kichwa cha habari kisemacho hivi "The West Attacked Russia's Economy. The Result is Another Stalemate" waandishi ni Alan Cullison na Georgi Kantshev. Ndani ya hii makala amehojiwa mchumi nguli, Prof Nicholas Mulder ambaye amebobea katika vikwazo vya uchumi amesema haya yafuatayo:

View attachment 2709557

Kwenye makala hiyohiyo, wanawanukuu wachumi wa The Carnegie Center ambao wanasema Urusi imepata faida ya ziada (Trade Surplus) mwaka 2022. Maneno yao ni haya hapa, naomba niyaweke tuyasome wote:

View attachment 2709567

Hapa naomba nieleweshwe kiuchumi. Wachumi wanaposema, (A country has a trade-surplus in current account) huwa wanamaanisha nini kitalaamu, ???

Tatu, umesema lengo la vikwazo ni kuzuia uchumi wa nchi ya Urusi kuweza kuendesha vita vya uvamizi dhidi ya Ukraine. Katika maana nyingine wanachotaka ni kuufanya Uchumi wa Urusi uweze kudorora kwa muda mrefu. WB na IMF watoa takwimu zao za National Development Outlook, ambazo baadhi ya takwimu zake zipo hapo juu. Kiuchumi naomba nieleweshwe, kwasasa taifa la Urusi lipo sehemu gani kiuchumi kati ya hizi mbili:

Is Russian Economy facing in recession, ???
Is Russian Economy facing a Soft Landing, ???
At what point can we say, Russia is facing a recession or a soft-landing, ???

Boy,punguza ukal wa maswal na huyu usije mkimbiza km ulivyomkimbiza yule mtaalam wa ndege vita
 
Hata Mimi nisiejua Mambo ya uchumi naona kaandika stori za vijiwe vya kahawa
Wakati mkuu BOY WONDER anaeleza facts
Appeasement policy ni story za vijiweni? Mbona kwa Hitler ilifanyika alipovamia nchi za Eastern Europe? Ndio kinachotokea kwa Urusi kwamba unahofia madhara ya vita ila sio kushindwa kumtandika!!
 
Vipi, mchumi umesoma taarifa ya Fitch niliyokuwekea hapa juzi kuhusu fedha ya Marekani na hali yake iliyopo. AU Fitch nao wamekosea, hawajachambua vizuri uchumi wa Marekani kama anavyosema, Janet Yellen, ???
An excerpt from the report
In Fitch's view, there has been a steady deterioration in standards of governance over the last 20 years, including on fiscal and debt matters, notwithstanding the June bipartisan agreement to suspend the debt limit until January 2025.

1. Fitch wanakiri hapa kwamba changamoto za uchumi ni sababu yame accumulate miaka 20 na sio short term effects kama za vita ya Ukraine au sijui kukosa rasilimali kama chakula au nishati.

Ratings Downgrade: The rating downgrade of the United States reflects the expected fiscal deterioration over the next three years, a high and growing general government debt burden.

2. Kingine wanasema issue ya deni ambayo pia ni accumulated over the years sio sababu ya vikwazo, rasilimali au vita ya Ukraine. Nitarudi tuchambue hili suala la deni maana 78% ya deni ni deni la ndani so hata waki default halina athari kiuchumi.

A) Deni Zima ni USD trillion 31 ila almost USD 24 Trillion ni deni la ndani ila USD 7 trillioni ndio deni la nje. Hii ni tofauti na nchi zetu masikini ambazo deni la nje ndio kubwa hivyo linatutesa maana lazima tulipe kwa fedha za kigeni. Ila kwa US deni la ndani linakua himilivu sababu ni la ndani.
us-dependency-on-foreign-lenders-to-finance-the-federal-debt-has-risen.jpg

B. Composition ya deni la ndani limetawaliwa na taasisi za umma za ndani.
the-federal-reserve-owns-about-40-percent-of-domestically-held-debt.jpg

Hii data inaonyesha hata waliokopesha zaidi serikali ni Federal reserve system!! Yaani ni sawa na kutoa pesa mfuko wa kushoto na kupeleka kulia!!

Waliobakia ni mifuko ya pensheni na uwekezaji ambayo ni long term obligations na sio SASA hivyo default yoyote haiwezi leta madhara hadi uchumi uporomoke ni sawa na Mme amdai mke wake!!

C) Kuna mikopo ya ndani ya serikali yaani taasisi Moja ya serikali inazikopesha taasisi nyingine. Hii ina maana wanaweza amua ku default bila madhara sababu Zina check out.
intragovernmental-debt-makes-up-nearly-one-quarter-of-all-us-public-debt.jpg

So tunaweza conclude kuwa matatizo ya kiuchumi ni accumulated debts and fiscal budgetary issues za miaka zaidi ya 20 as suggested by FITCH na hakuna connection na vikwazo au vita ya Ukraine.

NB: Deni kubwa ni la ndani Tena la taasisi za Umma hivyo wanaweza wasilipane directly na uchumi usiyumbe unless asilimia kubwa ingekua deni la nje then tungepata hofu kuwa wakitakiwa kuzilipa uchumi ungeyumba.
 
An excerpt from the report

Ratings Downgrade: The rating downgrade of the United States reflects the expected fiscal deterioration over the next three years, a high and growing general government debt burden.

Ndugu Mchumi unataka kusema, Unfunded Liabilities hazina madhara kwasababu ni madeni ya muda mrefu. Unafahamu ni lini kizazi cha Baby Boomers kinaondoka ofisini, hadi useme haya madeni ya zaidi ya USD Trilioni 128 hayana madhara. Ukifuatilia vizuri takwimu zinasema kwamba The American Social Security Fund will become insolvent in 10 years, propabably in 2032. Katika lugha nyingine, mfuko wa hifadhi wa Marekani utakuwa umefilisika ndani ya miaka kumi. Nchi haina fedha ya kulipa haya madeni. Unaposema kwamba hakuna madhara au hatari unamaanisha nini mchumi, ???

Pia hebu nisaidie kuelewa kuhusu, takwimu za serikali ya Marekani (The Congressional Budget Office) ambazo FITCH wamezinukuu kwenye taarifa yao. Zinasema haya yafuatayo kuhusu Marekani:

Mosi, Marekani anakusanya Trilioni 4 kwa mwaka, ila anatumia kama Trilioni 5 hadi 6. Hapa ina maana Marekani ana uhaba wa bajeti, lakini anaendelea kutumia zaidi ya alichonacho kupitia madeni. Mwaka huu peke yake Marekani atalipa marejeshi ya riba ya madeni kiasi cha USD Bilioni 640. Fedha ambayo imepishana kidogo na bajeti ya ulinzi ambayo ni USD Bilioni 891.

Pili, ndani ya mwaka 2024 Marekani atalipa riba ya madeni yake kiasi cha USD Bilioni 739. The Congressional Budget Office (CBO) wanasema kwamba baada ya miaka kuanzia mitatu, Marekani itakuwa inalipa riba ya madeni USD Trilioni 1, fedha ambayo ni kubwa kuliko bajeti ya ulinzi. Sasa, ndugu mchumi, hebu nieleweshe. Kama Marekani inakusanya USD Trilioni 4 kwa mwaka, halafu inalipa riba ya madeni USD Trilioni 1. Hapa atachomokaje, ???

Mbali na matatizo makubwa ya muda mrefu, jambo ambalo limesababisha haya ni kitendo cha serikali ya Marekani kupandisha juu riba (Hiking Interest Rates), kutoka 0.5% hadi kufika 6%, jambo ambalo ni hatari mno. Gharama za madeni zimakuwa kubwa ndiyo maana Marekani analipa riba kubwa mno. Mpaka sasa lengo kuu ni kujitahidi walau kushusha riba hadi 2%.

Mwisho kabisa, FITCH wanasema kwamba, riba kuwa juu (High Intererst Rates) zimeathiri uchumi kiasi kwamba Marekani inaweza kuingia kwenye mdororo (An Economic Recession). Jambo ambalo kama litatokea, litaathiri ukusanywaji wa kodi nchini humo, hivyo kupelekea zaidi uhaba wa bajeti kwasababu ya gharama ya shughuli za kiuchumi.

Hebu nisaidie wewe mchumi: Nini kimepelekea Marekani kupandisha riba juu hivi, ???

==========================================================
STAY WITH ME NDUGU MCHUMI,

Sasa hivi nahamia Ulaya kwenye taifa tajiri zaidi la Ujerumani, ambalo nalo limekumbwa na majanga makubwa. Takwimu za Organization for Economic Cooperation and Development (OECD) zinasema Ujerumani imepoteza uwekezaji (Foreign Direct Investment) kiasi cha Euro Bilioni 135 kwa mwaka 2022 peke yake. Wawekezaji wengi wamehamisha mitaji yake nchi za jirani.

Chanzo kikubwa ni mfumuko wa bei ya nishati nchini humo inayopelekea uzalishaji (Manufacturing) kuwa juu. Hivyo viwanda vya Ujerumani vimethirika mno kipindi hiki kuliko wakati wowote ule katika historia yake. Hawa hapa ni THE FINANCIAL TIMES, soma walichoandika kuhusu hili. Makala inaitwa, Germany Hit By Alarming Data On Foreign Investment, waandishi ni Martin Arnold na Patricia Nilson:
Recession in Germany.png

Ujerumani imeingia rasmi kwenye mdororo ndani ya mwaka 2023. Lakini sababu kubwa ni kwamba uchumi wa viwanda ambao ndiyo uti wa mgongo wa Ujerumani umeathirika vibaya mno. Wawekezaji wamehama kwa kiasi kikubwa nchini humo mwaka jana. Sababu kubwa ni kupanda kwa bei ya nishati. Sasa hebu nisaidie, nini kimesababisha nishati kupanda bei hadi kuvuruga uchumi wa Ujerumani, ???
 
Ndugu Mchumi unataka kusema, Unfunded Liabilities hazina madhara kwasababu ni madeni ya muda mrefu. Unafahamu ni lini kizazi cha Baby Boomers kinaondoka ofisini, hadi useme haya madeni ya zaidi ya USD Trilioni 128 hayana madhara. Ukifuatilia vizuri takwimu zinasema kwamba The American Social Security Fund will become insolvent in 10 years, propabably in 2032. Katika lugha nyingine, mfuko wa hifadhi wa Marekani utakuwa umefilisika ndani ya miaka kumi. Nchi haina fedha ya kulipa haya madeni. Unaposema kwamba hakuna madhara au hatari unamaanisha nini mchumi, ???

Pia hebu nisaidie kuelewa kuhusu, takwimu za serikali ya Marekani (The Congressional Budget Office) ambazo FITCH wamezinukuu kwenye taarifa yao. Zinasema haya yafuatayo kuhusu Marekani:

Mosi, Marekani anakusanya Trilioni 4 kwa mwaka, ila anatumia kama Trilioni 5 hadi 6. Hapa ina maana Marekani ana uhaba wa bajeti, lakini anaendelea kutumia zaidi ya alichonacho kupitia madeni. Mwaka huu peke yake Marekani atalipa marejeshi ya riba ya madeni kiasi cha USD Bilioni 640. Fedha ambayo imepishana kidogo na bajeti ya ulinzi ambayo ni USD Bilioni 891.

Pili, ndani ya mwaka 2023 Marekani atalipa riba ya madeni yake kiasi cha USD Bilioni 739. The Congressional Budget Office (CBO) wanasema kwamba baada ya miaka kuanzia mitatu, Marekani itakuwa inalipa riba ya madeni USD Trilioni 1, fedha ambayo ni kubwa kuliko bajeti ya ulinzi. Sasa, ndugu mchumi, hebu nieleweshe. Kama Marekani inakusanya USD Trilioni 4 kwa mwaka, halafu inalipa riba ya madeni USD Trilioni 1. Hapa atachomokaje, ???

Mbali na matatizo makubwa ya muda mrefu, jambo ambalo limesababisha haya ni kitendo cha serikali ya Marekani kupandisha juu riba (Hiking Interest Rates), kutoka 0.5% hadi kufika 6%, jambo ambalo ni hatari mno. Gharama za madeni zimakuwa kubwa ndiyo maana Marekani analipa riba kubwa mno. Mpaka sasa lengo kuu ni kujitahidi walau kushusha riba hadi 2%.

Mwisho kabisa, FITCH wanasema kwamba, riba kuwa juu (High Intererst Rates) zimeathiri uchumi kiasi kwamba Marekani inaweza kuingia kwenye mdororo (An Economic Recession). Jambo ambalo kama litatokea, litaathiri ukusanywaji wa kodi nchini humo, hivyo kupelekea zaidi uhaba wa bajeti kwasababu ya gharama ya shughuli za kiuchumi.

Hebu nisaidie wewe mchumi: Nini kimepelekea Marekani kupandisha riba juu hivi, ???

==========================================================
STAY WITH ME NDUGU MCHUMI,

Sasa hivi nahamia Ulaya kwenye taifa tajiri zaidi la Ujerumani, ambalo nalo limekumbwa na majanga makubwa. Takwimu za Organization for Economic Cooperation and Development (OECD) zinasema Ujerumani imepoteza uwekezaji (Foreign Direct Investment) kiasi cha Euro Bilioni 135 kwa mwaka 2022 peke yake. Wawekezaji wengi wamehamisha mitaji yake nchi za jirani.

Chanzo kikubwa ni mfumuko wa bei ya nishati nchini humo inayopelekea uzalishaji (Manufacturing) kuwa juu. Hivyo viwanda vya Ujerumani vimethirika mno kipindi hiki kuliko wakati wowote ule katika historia yake. Hawa hapa ni THE FINANCIAL TIMES, soma walichoandika kuhusu hili. Makala inaitwa, Germany Hit By Alarming Data On Foreign Investment, waandishi ni Martin Arnold na Patricia Nilson:
View attachment 2711091

Ujerumani imeingia rasmi kwenye mdororo ndani ya mwaka 2023. Lakini sababu kubwa ni kwamba uchumi wa viwanda ambao ndiyo uti wa mgongo wa Ujerumani umeathirika vibaya mno. Wawekezaji wamehama kwa kiasi kikubwa nchini humo mwaka jana. Sababu kubwa ni kupanda kwa bei ya nishati. Sasa hebu nisaidie, nini kimesababisha nishati kupanda bei hadi kuvuruga uchumi wa Ujerumani, ???

Boy, ujeruman wamepatwa na nin inakuaje wanakubal kuumiza uchumi wao kwa maslah ya us???
 
Mkuu FRANC THE GREAT hongera Kwa mchango wako mzuri na wakisomi, lakini binafsi ningependa ujibu suali la nyongeza la mleta mada kua.

1. Kipind vikawazo hivyo vikimuathiri urusi wao hali zao zikoje kiuchumi?.
Hali zao kina nani hao?

Kama ni EU, walikuwa kwenye kiwango kidogo cha ukuaji hasi cha asilimia 0.1 kuanzia mwaka jana mwishoni (technical recession) kwa mujibu wa data za hivi karibuni.
 
Mchumi mimi nimekusoma na nimekuelewa sana sanaaa tu. Ila nina mambo 3 tu:

Mosi, Suala zima la takwimu: Sasa naomba unisaidie zaidi kuelewa, INTERNATIONAL MONETARY FUND (IMF), tarehe 25 July walitoa takwimu zao ambazo zimerekebisha makadirio ya uchumi wa Urusi (Estimates) na kusema kwamba uchumi wa Urusi utakuwa kwa asilimia 1.5% kwa mwaka 2023 kutoka 0.7%.

Kumbuka, mwaka 2022 IMF walisema uchumi wa Urusi ungesinyaa (Contraction) kwa asilimia 12% kwa mwaka 2022, lakini kufika mwezi wa September wakarekebisha tena na kusema ungesinayaa kwa asilimia 2.1% tu. World Bank wamesema uchumi wa Urusi utakuwa kwa kasi chanya, japo kiwastani (Positive but modest growth) kwa asilimia 1.2% ifikapo mwaka 2024.

Lakini hebu tuzingatia takwimu basi, mtandao wa CIA unasema kwamba, mwaka 2021 kabla ya vita GDP (Purchasing Power Parity) ya Urusi ilikuwa ni USD Trilion 4, na baada ya vita wakasema ingeshuka hadi kufika USD Trilion 3.9. Ila katika kufunga mwaka 2022 IMF wakasema GDP (In Purchasing Power Parity) ya Urusi imefika USD Trilioni 5.51 ambayo ni kubwa kuliko Ujerumani ambayo ni USD Trilioni 5. Mtandao wa CIA, unasema hivi:

View attachment 2709542

Hii ni mwaka 2021, na ila sasa WB na IMF wanasema mwaka 2022 imefikia USD 5.51 Trilion. Sasa nachoomba kufahamu ni hiki, umezungumzia, DATA INTEGRITY, ila hizi takwimu zimetolewa na IMF na WB, je tusizitegemee na kuziamini kwasababu zimetolewa na Urusi yenyewe, ???

Pili, nimesoma makala ya, The Wall Street Journal, la tarehe 2 AUGUST 2023, kwenye kichwa cha habari kisemacho hivi "The West Attacked Russia's Economy. The Result is Another Stalemate" waandishi ni Alan Cullison na Georgi Kantshev. Ndani ya hii makala amehojiwa mchumi nguli, Prof Nicholas Mulder ambaye amebobea katika vikwazo vya uchumi amesema haya yafuatayo:

View attachment 2709557

Kwenye makala hiyohiyo, wanawanukuu wachumi wa The Carnegie Center ambao wanasema Urusi imepata faida ya ziada (Trade Surplus) mwaka 2022. Maneno yao ni haya hapa, naomba niyaweke tuyasome wote:

View attachment 2709567

Hapa naomba nieleweshwe kiuchumi. Wachumi wanaposema, (A country has a trade-surplus in current account) huwa wanamaanisha nini kitalaamu, ???

Tatu, umesema lengo la vikwazo ni kuzuia uchumi wa nchi ya Urusi kuweza kuendesha vita vya uvamizi dhidi ya Ukraine. Katika maana nyingine wanachotaka ni kuufanya Uchumi wa Urusi uweze kudorora kwa muda mrefu. WB na IMF watoa takwimu zao za National Development Outlook, ambazo baadhi ya takwimu zake zipo hapo juu. Kiuchumi naomba nieleweshwe, kwasasa taifa la Urusi lipo sehemu gani kiuchumi kati ya hizi mbili:

Is Russian Economy facing a recession, ???
Is Russian Economy facing a Soft Landing, ???
At what point can we say, Russia is facing a recession or a soft-landing, ???

Nashukuru kwa maswali, kiongozi wa mjadala!

Nitajibu swali la kwanza kama ifuatavyo:
Hizo ripoti za IMF za hivi karibuni kuhusiana na uchumi wa Urusi zimezua mjadala mkubwa miongoni mwa wataalamu, wachumi bila kusahau wanahabari duniani. Media maarufu ikiwemo Reuters ilitoka na article yenye kichwa cha habari: The IMF's outlook on Russia is too rosy to be true. Ndio maana katika mchango wangu uliopita, nilizungumza kuhusu hali ya kuaminika kwa taarifa zilizopo kwa sababu nimeona hizi takwimu za IMF zikitumika humu kujengea hoja kwamba "vikwazo havifanyi kazi".

The IMF's outlook on Russia is too rosy to be true:

Ili kujibu swali lako la kwanza, nitanukuu vyanzo mbalimbali ili kuonesha jinsi ambavyo takwimu hizo zimeleta shida na kuzua upinzani mkubwa katika uwanja wa uchumi.

Tafiti mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ambazo nimezileta hapa katika post iliyopita zinapingana kwa kiasi kikubwa na utabiri wa IMF. Miongoni mwa wakosoaji wakubwa wa makisio ya uchumi yaliyotolewa na IMF kuhusu maendeleo ya uchumi wa Urusi ni Professor Jeffrey Sonnenfeld wa Yale University nchini Marekani.

Miongoni mwa maandiko yake kuhusu hilo, akishirikiana na wachumi wengine kama vile Stephen Samuel Roach, mhadhiri mkuu [Yale School of Management] ambaye pia aliwahi kufanya kazi Morgan Stanley kama chief economist, unaweza kulipata kwenye website ya gazeti la Fortune lenye kichwa cha habari: How the IMF naively parroted Putin's fake statistics–and botched its economic forecast for Russia.

Article hiyohiyo imechapishwa pia kwenye website ya Yale School of Management (Yale Insights) yenye title: With 'Zero Visibility' into the Russian Economy, the IMF is Parroting Putin's Line.

Links hizi hapa:

Ili kurahisisha mambo, hivi hapa chini ni vipande vichache vya andiko hilo:

Fortune 1.png

Article imeendelea kwa kusema;

Fortune 2.png

Hoja kubwa ya Jeffrey Sonnenfeld na wenzake ni kuwa, kwa sasa IMF haina taarifa za kutosha kuhusiana na uchumi wa Urusi ili kuwawezesha wataalamu wake kukokotoa na kutoa makadirio yenye kuridhisha kitaalamu, huku kukiwa na ushahidi wa wazi kabisa wa wataalamu wa IMF sanjari na mashirika mengine kunyimwa taarifa muhimu za kiuchumi na serikali ya Urusi mara baada ya uvamizi wake.

Katika hiyo article, kuna mahali wameambatanisha link yenye nyaraka ambayo ndani yake kuna kauli kutoka IMF kwenda kwa Sonnenfeld na timu yake (Yale University) kuhusiana na takwimu zilizotolewa na shirika lao. Katika hiyo statement, IMF inakiri kuwepo kwa sintofahamu kubwa (massive uncertainty) kuhusiana na mustakabali wa uchumi wa urusi hali ambayo inapelekea kuwepo kwa utata mwingi kwenye issue ya kutoa makisio.

Nimechukua kipande (screenshot) cha hiyo statement kutoka katika hiyo nyaraka yenye takwimu na makisio ya uchumi wa Urusi. Inasema;

"We agree that there is massive uncertainty surrounding the future of the Russian economy, and hence doing a forecast could be seen as a "fool's errand"."

Wametumia msemo "fool's errand" wakikubali kwamba kitendo cha kufanya utabiri wa kiuchumi kuhusu Urusi katika mazingira ya sasa kinaweza kutafsiriwa kama kazi ya kijinga isiyo na tija. Statement hiyo vilevile inasapoti kile nilichokisema kuhusu Data Integrity na uhaba wa upatikanaji wa taarifa za kutosha.

Screenshot:
IMF Statement.png

Nyaraka nzima iko katika muundo wa PPTX:

Mkosoaji mwingine ni huyu anayefahamika kama Agathe Demarais ambaye ni mchumi, pia ni mtaalamu wa vikwazo vya kiuchumi kutoka kitengo cha utafiti wa masuala ya kiuchumi duniani (Economist Intelligence Unit) chini ya The Economist Group [media company]. Moja ya maandiko yake utalipata kwenye website ya Foreign Policy lenye title ambayo iko straightforward: Don't Trust Russia's Numbers (Moscow has made economic statistics a central part of its information war). Yeye amejikita zaidi kuelezea nguzo kuu za kile anachokiita "Russia's disinformation" kuhusiana na mwenendo wa uchumi wake.

Link:

Demarais anasema kwamba;

The latest controversy surrounds the state of the Russian economy and what Western media and others have been reporting to their audiences. Read anything about the war in Ukraine these days, and you'll probably find a mention that the Russian economy contracted by about 2 percent in 2022—a low decline that suggests little more than a mild recession. That number has entered the policy debate: For some, the low figure is proof that the Russian economy is resilient and sanctions do not work. Others use the same figure to argue that sanctions are starting to bite and Western countries should double down. These opposing arguments have one thing in common: They rely on a largely meaningless number.

Ukiendelea kumsoma huyo mchumi, anataja sababu kadhaa zilizochangia kuonesha huo upungufu mdogo ulioripotiwa tofauti na ilivyotarajiwa baada ya uvamizi wa Urusi mwaka 2022.

Even if Russia's reported GDP decline were truthful, it is clear that three factors artificially boosted the Russian growth number in 2022. First, the economic growth figure has been fueled by Russia's turbocharged production of military gear. Producing tanks and missiles does not improve living standards, however, and this part of Russian GDP will quickly be destroyed on the battlefield. Second, Russia's export earnings jumped in 2022 because of the war-induced spike in energy prices. And third, Western embargos on technology and other goods as well as sinking Russian consumer demand led to a plunge in imports, which dropped by almost 10 percent during 2022, according to Russia's official data.

Mwisho wa kunukuu!

Kwa kifupi, hoja yake kubwa ni kuwa, Urusi imekuwa ikichezea takwimu za uchumi wake kama sehemu ya disinformation war dhidi ya nchi za magharibi ili kujibu ama kukabiliana na hoja au tuhuma kwamba uchumi wa Urusi umedorora kutokana na vikwazo. Hivyo, taarifa hafifu za kiuchumi zinazotolewa na Urusi hazikidhi vigezo au sifa za kuweza kuaminika kutoa makisio yanayoweza kukubalika kiuchumi.

Swali la pili:
Current account surplus, kwa lugha rahisi ni hali ya kiuchumi ambapo thamani ya bidhaa na huduma zinazozalishwa kupelekwa nje (exports) zinazidi thamani ya bidhaa na huduma zinazoingia nchini (imports).

Kwa kifupi kuhusiana na rekodi ya current account surplus ya Urusi mwaka 2022:
Kushuka kwa thamani ya imports kumechagizwa na uamuzi wa makampuni mengi ya nchi za magharibi kujiondoa na kuondoa biashara zao nchini Urusi kutokana na vikwazo. Kilichoongeza thamani ya exports ni mapato ya mafuta na gesi kutokana na kuongezeka kwa bei ya nishati kulikochochewa na vita inayoendelea. Hiyo ni kabla ya bidhaa hizo hususani mafuta kuwekewa vikwazo.

Tafuta takwimu za hivi karibuni; current account surplus imepungua kutokana na kushuka kwa mapato yatokanayo na mafuta na gesi. Again, narudia, Urusi imesitisha utoaji wa taarifa muhimu za kiuchumi, zikiwemo data zake za capital outflow mwaka huu.

Kuhusu swali la tatu:
Uchumi wa Urusi hauko kwenye soft landing bali ulishaingia kwenye recession kwa mujibu wa data zilizotolewa mara ya mwisho na Urusi yenyewe. Hakuna mjadala kuhusu uchumi wa Urusi kuwa kwenye recession ama kinyume chake kwa sababu kwa mujibu wa wachumi wa pande zote, Urusi iko kwenye recession. Mabishano yako kwenye kiwango cha recession ilichonacho Urusi.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za GDP za mwaka 2022 zilizotolewa na Urusi, uzalishaji ulianguka kwa asilimia takribani 4.1 na 4 katika robo mbili mfululizo (3&4) ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka mmoja uliopita. Maana yake ni kwamba Urusi ilikuwa kwenye technical recession katika vipindi hivyo viwili mwaka jana. Takwimu rasmi za robo ya nne hazikutolewa hadharani.

Mwaka huu, Urusi ilitoa ripoti ndogo kwamba uzalishaji ulianguka kwa asilimia 1.9 katika robo ya kwanza ya mwaka ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2022; ripoti ambayo bado inaonesha recession pamoja na kwamba wachumi kadhaa wamekataa kuziamini hizo taarifa. Hata ripoti mbalimbali za mashirika na taasisi nyinginezo [independent] zinasema kwamba uchumi wa Urusi bado uko kwenye contraction mwaka huu.

Asante!
 
Tokea mwaka 1944, baada ya kutengeneza mfumo wa Bretton-Woods hakuna taifa ambalo limewahi kuwa na uchumi mkubwa kama Marekani. Kufika mwaka 1945, Marekani ilikuwa inamiliki nusu nzima ya uchumi wa dunia. Fedha ya Marekani ikishikiliwa na dhahabu (Gold-Backed) ilikuwa ndiyo inatumiwa kwa kiwango kikubwa kwenye biashara zote za kimataifa.

Mwaka 1957, baada ya Raisi Gamal Abdel Nasser wa Misri kutaifisha mfereji wa Suez, Uingereza, Ufaransa na Israel waliunda mkakati wa kuvamia Misri ili kumtoa Nasser. Mkakati huu ulikufa kibudu baada ya Raisi wa Marekani General Dwight Eisenhower kuwachimba mkwara mzito Waingereza kwamba wangeacha kununua hati-fungani (Sovereign Bonds) za Uingereza na nyingine wangeziuza, jambo ambalo lingeangusha uchumi wa Uingereza.

Kiufupi, baada ya hili kutokea Raisi wa Ufaransa General Charles De Gaulle alilalamika na kusema kwamba "The dollar gives America an exorbitant privilege in international financial system". Akimaanisha kwamba dola inampa Marekani nguvu iliyomithirika kwenye uchumi wa dunia dhidi ya mataifa mengine. Kiufupi Marekani akikutoa kwenye mfumo wake wa kifedha, lazima uumie.

Wataalamu wanatumia vipimo (Metrics) kama GDP na PPP kupima uchumi wa dunia. Ukitumia kipimo cha GDP, nadhani Marekani ndiyo taifa lenye uchumi mkubwa zaidi duniani likifuatiwa na Uchina. Uchumi wa Marekani peke yake ni asilimia 24% ya uchumi wa dunia (Global GDP). Kiufupi ni kwamba, all financial roads lead to America.

Marekani hayuko peke yake, anashirikiana na wenzake wa kule Ulaya (European Union) na wenzake wa chama cha mabwanyenye wa dunia almaarufu kama G7. Ukichanganya uchumi wa Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Italia, Canada na Japan, ambao ndiyo nchi tajiri zaidi duniani unapata asilimia 30.7% ya uchumi wa dunia (Global GDP).

Kiuhalisia, haya mataifa saba ndiyo yanayoendesha uchumi wa dunia kupitia mifumo waliyoitengeneza baada ya mwaka 1945. Viwanda vikubwa duniani ni vyao, masoko makubwa ya hisa ni yao, mabenki makubwa duniani ni yao, wao ndiyo wanaongoza katika kuzikopesha fedha nchi nyingine na wao ndiyo wanaongoza kwa kuuza huduma zaidi hapa duniani.

Maswali yangu ya kiuchumi ni haya yafuatayo:
Mosi, kwanini Urusi ambayo ni asilimia 4% tu ya uchumi wa dunia (Share in Global GDP) bado haijaanguka baada ya mataifa makubwa yanayomilikia asilimia 30.7% ya uchumiwa dunia kuwawekea vikwazo vikali ?

Pili, kwanini makampuni ya Urusi ya nishati ndiyo yameongoza duniani kwa kuuza zaidi nishati, ilhali yamewekewa vikwazi baada vikali ? Takwimu zilizotolewa na Marekani yenyewe zinasema kiujumla mashirika ya nishati ya Urusi yameuza zaidi na kupata faida kipindi hiki cha vita na vikwazo kuliko kipindi kingine chochote. Tatizo liko wapi hapa ?

Tatu, Je, tutegemee kwamba kuna siku hivi vikwazo vitafanya kazi na vitauangusha uchumi wa Urusi kama ambavyo Raisi Biden alisema mwaka 2022 kabla ya uvamizi kuanza ? Alisema kwamba uchumi wa Urusi ungeanguka ndani ya wiki chache tu, sasa ni mwaka na zaidi. Mataifa ya Magharibi yamefanikiwa au tuendelee kusubiri ?
Walikosea calculation zao na aliyeanzisha vita alijua hilo akajua namna ya kukwepa na kufaidika na vikwazo

Vita ni akili unaweza kuwa na gobore alafu mpinzani wako ana AK 47 akafa
 
Back
Top Bottom