Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Huu uzi kumbe ulianza na uongo mkubwa hivi!

West haijaweka vikwazo vyovyote katika sekta ya Nishati ya Urusi. Gesi na mafuta ya Urusi havikuguswa katika vikwazo vya West.
 
Tunafunga mwaka 2023.

1. Urusi imewekewa vikwazo vya kiuchumi 17,000 na mataifa yenye uchumi mkubwa duniani.
2. Ujerumani taifa tajiri zaidi Ulaya limeingia rasmi kwenye mdororo wa kiuchumi.
3. Ukraine imepoteza asilimia 20% ya eneo lake la ardhi lenye rasilimali zenye thamani ya dola za marekani trilioni 10.
4. Msaada mkubwa wa kijeshi kutoka umoja wa kujihami wa NATO umeshindwa kuidhibiti Urusi kwenye uwanja wa vita.

Tutegemee nini tena ???
 
Tutegemee Ukraine kushinikizwa na wafadhili wake kutafuta njia ya kuanzisha mazungumzo ya amani na mvamizi.
 
Ila EU sio nchi MKUU
 
Naeka kituo
 
Ndege za F-16 kuwa game changer
Kwamba ndege zisizofika 100 ndiyo zinaweza kuipa Ukraine mkono wa juu dhidi ya majeshi ya Urusi ???

Mwaka 1967 Israel alitumia ndege zisizopungua 183 kuwa na mkono wa juu dhidi ya maadui zake akiwemo Misri. Urusi ana mifumo ya ulinzi wa anga aina ya S-400 isiyopungua 96 ambayo rada zake zinaweza kuona ndege ikiwa inaondoka uwanjani, upande wa pili ana ndege-vita zaidi ya 1000. Unadhani F-16 chache zinaweza mdhibiti Mrusi kweli ???​
 
Ukituliza kichwa sana utakuja kubaini kua ukubwa wa kijeshi na kiuchumi wa NATO upo vizuri lakini ni 'overrated '. Wakati Russia anaanza 'Special military operation ' pale Ukraine, niliwahi kusikiliza mahojiano ya DW na professor wa uchumi nadhani alikua anatokea UDOM au UDSM.

Yule professor aliulizwa mtizamo wake juu ya vikwazo alivyopewa Russia na West, majibu yake yalikua hivi " Urusi hana jinsi, inabidi asalimi amri tu. Ukiwekewa vikwazo kwenye mifumo ya dunia ya kamalipo hutoweza kununua au kuuza bidhaa katika soko la Dunia, hivyo Russia atashindwa kijeshi na ataanguka kiuchumi kwa kishindo kisichowahi kuonekana"

Kwa jinsi professor wa uchumi alivyokua akichambua, mie niliamini kabisa kua Russia ataanguka vibaya ndani ya miez 6 mpaka mwaka mmoja.. la haula! Pamoja na misaada ya kijeshi, intelligence, na mamluki wa kipiganaji West wamefeli vibaya kuiangusha Russia, nimekuja kubaini ulaya magharibi wanaitegemea sana Urusi kwenye nishati ya bei rahis na chakula..

Wazungu wa west wana 'Ego na Pride' hwapendi kujiona wanyonge ila superior, vita hii imetufungua macho wengi kimtazamo.
 
Ila EU sio nchi MKUU
Kwenye economics na data za World bank EU huwa ina stand alone maana pia ina currency yake na policy zake exclusively na nchi zisizo EU. Hii ni sawa na huku Africa huwa wanaigawa Africa kuwa sub saharan Africa alafu nchi za Afrika za kiarabu zinatambulika kama MENA yaani Middle East and North Africa.
 
Boy,nimeshaandaa notbuku mwaga notsi
 
Warusi akili kubwa.Ukifikiri hivi wenzio wameshakutangulia.
 
Urusi ana mifumo ya ulinzi wa anga aina ya S-400 isiyopungua 96 ambayo rada zake zinaweza kuona ndege ikiwa inaondoka uwanjani, upande wa pili ana ndege-vita zaidi ya 1000. Unadhani F-16 chache zinaweza mdhibiti Mrusi kweli ???
Hii hii mifumo iliyohujumiwa sana na Ukraine..

Warusi walishindwa kabisa kudhibiti anga la Ukraine japo wana ndege nyingi, hata 'SEAD' hawakuweza kabisa.....huenda military doctrine yao imechangia huo udhaifu...

Kwa doctrine ya Warusi 'airforce is an extension of artillery'

Anyway Warusi ni mabingwa wa propaganda.

T14 Armata
 
Biden na mabwanyenye wenzake ni kama ile hadithi ya fisi kumfuata nyuma binadamu akitegemea mkono wake utadondoka apate mlo. Urusi ni taifa kubwa kuliko yote duniani. Kwa hivyo linaweza kujitoshela bila hata ya kutegemea biashara ya kimataifa.
 

Urusi imetumia miongo miwili kujitayarisha dhidi ya hicho ambacho wanafanya leo!
Ni sawa kuiwekea vikwazo china leo itakua n too late nchi zitazoumia zaidi ni zile zilizoweka
 
Urusi imetumia miongo miwili kujitayarisha dhidi ya hicho ambacho wanafanya leo!
Ni sawa kuiwekea vikwazo china leo itakua n too late nchi zitazoumia zaidi ni zile zilizoweka
Tokea mwaka 2016 nimekuwepo humu ndani kuwaambia hawa ndugu zetu kwamba Urusi ni taifa kubwa na lenye nguvu iliyomithirika hapa duniani. Mwaka 2022 wakati Urusi anavamia Ukraine niliwaambia kwamba NATO hawawezi kulishinda kirahisi taifa lenye silaha za nyuklia, ushawishi mkubwa wa kidiplomasi, ujuzi mkubwa wa kisayansi na mtandao mkubwa wa kijasusi. Vijana wengi walinibeza na kusema maneno mengi sana, ila nilichowaambia ni kwamba muda ndiyo mwalimu mzuri.

Sasa tunaingia mwaka 2024, Urusi amewekewa vikwazo vya kila namna lakini bado yuko imara. Kuhusu kusema kwamba Warusi hawana nguvu kijeshi kwasababu Ukraine anawasumbua nadhani nalo limepoteza mashiko. Israel ni moja ya taifa lenye nguvu kubwa mno kijeshi lakini mpaka sasa ni mwezi wa pili hawajafanikiwa kuwadhibiti wanamgambo wa HAMAS. Hili halimaanishi kwamba Israel ina jeshi dhaifu bali ni kwamba uwanja wa vita huwa unabadilika kama upepo, kubwa zaidi nina uhakika asilimia 100% HAMAS anasaidiwa na mataifa makubwa ndiyo maana kafanya jambo linaloshangaza dunia.

Ukweli ni kwamba Urusi hapambani na Ukraine bali NATO yote. Kuamini kwamba Ukraine inaweza kuisumbua Urusi hivi ikiwa yenyewe tu, siyo jambo la ukweli. Kubwa zaidi, Urusi anajizuia sana kule Ukraine ukilinganisha na kinachoendelea kule GAZA. Ndani ya miaka miezi miwili, Israel imeua raia wengi kuliko hata wale ambao Urusi imeua ndani ya miaka miwili kule Ukraine. Mtu makini ni lazima ujiulize maswali kama haya.​
 
Unaweza kutupa ushahidi wa hii kauli yako?
Sasa hili nalo linahitaji mashindano ? Hebu zingatia haya yafuatayo:

Mosi, uchumi wa viwanda wa mjerumani umejengwa juu ya utegemezi wa nishati ya bei ndogo kutoka Urusi. Mpaka kufika mwaka 2022, viwanda vya Ujerumani vilikuwa na thamani ya dola za kimarekani Trilioni 1, lakini vinaendeshwa na nishati ya gesi kutoka Urusi yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 60. Utegemezi huu ulianza chini ya mawaziri wakuu wa Ujerumani, bwana Gerhard Schroeder na bibi Angela Merkel. Miaka zaidi ya ishirini, Ujerumani amekuwa akitegemea nishati tokea Urusi.

Utegemezi huu ndiyo umeifanya Urusi kuwa na rungu kubwa ambalo inalitumia kuuwagawanya UMOJA WA ULAYA. Nchi nyingi mbali na Ujerumani bado zinategemea mafuta tokea Urusi, hivyo vikwazo haviwezi kufanya kazi yoyote ile. Wameweka PRICE CAP, ila hapohapo Ufaransa anaendelea kununua mafuta ya Urusi kutoka India kwa bei ya juu zaidi.

Pili, Urusi alijenga mahusiano mazuri sana na mataifa ya mashariki ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi. Kuanzia miaka ya 2000, Urusi alianza Reproachment na Uchina, ambapo walianzisha mahusiano mazuri kwenye ulinzi na kiuchumi. Hakuishia hapo, taifa kama India linategemea silaha za kijeshi na nishati kutoka Urusi. Hivyo haya mahusiano ndiyo yalipelekea kutengenezwa kwa vyombo kama BRICS & THE SHANGHAI COOPERATION ambavyo ni mbadala wa IMF na WB, japo bado vinaendelea kukua. Kitendo cha mataifa kama Saudi Arabia, Iran, Ethiopia, UAE na Argentina kutaka kujiunga na BRICS ni ushahidi tosha kwamba Urusi alijipanga vizuri.

Ikumbukwe, BRICS ndiyo taasisi yenye mataifa yenye wetu wengi zaidi duniani, lakini pia ndiyo mataifa yenye rasilimali nyingi ambazo dunia inazitegemea. Kama UAE, Saudi Arabia, Iran na Urusi, mataifa yanayoongoza kwa uzalishaji wa nishati duniani, yatakuwa ndani ya BRICS, basi Uchina na India watakuwa wametatua changamoto zao za uhaba wa nishati. Kubwa zaidi, BRICS itakuwa na nguvu kuliko hata OPEC. Mikakati hii ilianza kufanyika miaka ya 2000, punde baada ya Vladmir Putin kuwa Raisi.

Tatu, kipindi chote cha vita baridi Urusi ilikuwa inategemea nafaka kutoka Marekani, jambo ambalo lilikuwa hatari kwa usalama wake. Kufika mwaka 2016 Urusi likawa taifa ambalo linazalisha nafaka ambayo inatosha na kubaki. Kufika mwaka 2020 Urusi ndiyo likawa taifa ambalo mbali na kuongoza katika uzalishaji wa nafaka duniani, likawa linaongoza katika kuuza mbolea duniani, mpaka kufika mwaka 2022, Ukraine na Urusi walikuwa wanauza zaidi ya asilimia 40% ya nafaka yote duniani, huku asilimia 24% nzima ikiwa inaenda barani Ulaya.

Waswahili husema ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Kiufupi huwezi kuutukana mkono unaokulisha. Walichokifanya Warusi, waliachana na ule ujinga wa kutumia maguvu, wakaamua kutumia akili. Waliusoma vizuri uchumi wa nchi za Magharibi na mfumo wake wa utandawazi, wakafahamu udhaifu uko wapi na wakaanza kuutumia kuminya Ulaya na Marekani.​
 
Umechambua Kama mpishi anavyotoa chuya na mawe kwenye mchele pitia hapo Machame road unywe mbege nakuja lipa nipo napa kiwandani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…