Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Na. M. M. Mwanakijiji
Sikuwahi kuelewa kwanini wakati mwingine mtu anapokuwa na mawazo au ametatizika kimawazo anaanza kujikuna nywele. Au mtu anakuuliza jambo halafu hauna jibu unaanza kujishika kidevu au unakuna nywele hata kama haziwashi! Maswali au mambo mengine wakati fulani yanakwaza na yanaweza kukufanya ufike mahali utamani kujinyofoa nywele.
Mojawapo ya maswali ambayo yameanza kunijia siku hizi za karibuni ni hili kuhusu "ndugu zetu hawa". Hawa ndugu zetu wamekuwa wakija kila baada ya miaka mitano kuomba uongozi; wanabembeleza tena wameshika kakitabu kanaitwa "Ilani ya Uchaguzi". Ukiishika hiyo Ilani imejazwa maneno na ahadi nyingi tena ziko kwenye vifungu vyenye namba ili usindishwe kunukuu. Watakuja na muziki na bendi; vikundi vya sarakasi, na ngoma za kienyeji na ngonjera! Wakati mwingine watawaalika waimba mashairi na tenzi zenye mwendo wa taarab kabambe!
Yaani, ukichukua Ilani ya Uchaguzi ya chama chao kuanzia tu na mwaka 1995 hadi sasa kuna ahadi zimetolewa humo kuhusu suala la nishati na tatizo la umeme nchini hadi unajiuliza hivi huwa wanakumbuka walichoahidi miaka mitano kabla yake? Au inawezekana kila unapokaribia uchaguzi mwingine wanaanza kuangalia na kusema "duh mbona tatizo bado lipo, hebu tuahidi tena"! Halafu wanakaa na kuja na ilani nyingine halafu tunarudia tena.
Sasa tatizo sijui ni wanasiasa au ni watendaji. Hili ndilo linanileta kwenye swali la leo. Hivi kuna uwezekano hawa ndugu zetu waliingia shuleni lakini shule haikuwaingia? Hivi watu wote waliosomea shahada za sayansi na saa katika umeme, utawala, uongozi na menejimenti; wote waliosomea mambo ya fedha n.k Hivi ni kweli kabisa hawa watu wameshindwa kabisa kutatua hili tatizo la umeme? Yaani, tunachoshuhudia hadi leo hii ni upeo wa uwezo wao!
Huwa nasema "upeo wetu, ndio ukomo wetu". Yaani, ukijumlisha elimu ya watu wote kwenye serikali - wizara, idara, na wakala mbalimbali; yaani ukijumlisha uwezo wao wote jumla yake ni "tatizo la umeme". Yaani, kwa miaka yote hii walipoenda shule, kozi, na mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi ukijumlisha vyote hivyo jumla yake ni hii: Tatizo lisiloisha la umeme. Yaani, kukatika katika kwa umeme, mgao wa mara kwa mara n.k yote haya ni jumla ya elimu ya viongozi na watendaji ndani ya serikali hadi mitaani kabisa.
Ndio maana leo najiuliza; hivi hawa wenzetu wanaosimamia sekta hii ya umeme kwa miaka yote hii walipoenda shule ambapo walisifiwa kuwa hawakupata makarai au mayai; kwamba wanasiwa kuwa wao ndio walikuwa "vipanga"; yaani maprofesa waliowafundisha na wanafunzi waliosifiwa kuwa walipata "Upper Class" kwenye shahada zao za uzamaji, uvumaji, uvumbivu na uvunjifu yaani hawa ndugu walichosomea kilikuwa kitu gani?
Yaani, mnataka kabisa tuamini kuwa kama taifa na tunapoelekea miaka 60 ya Muungano uwezo wa wasomi wetu wabobezi ndio huu kwenye sekta ya umeme? Yaani, haya ndiyo matunda ya kujivunjia ya muungano? Au kuna kitu kingine walikisomea wenzetu hawa?