Swali la Ugomvi: Kwani Wenzetu Hawa Walisomea Nini? - Part 1

Ulishapoteza Credibility baada ya kununuliwa na yule mwovu na kugeukia upande wa watesi!! Nakushangaa hii nguvu ya kutamka haya unaitoa wapi? Si ulikua upande wa aliyetaka kutawala milele?

Siku zote muda ni hakimu wa yote.... ungejikalia kimya tuu kuliko kujaribu kukirudia kichaka chako cha zamani, huaminiki zaidi sana unatia kinyaa!!
Tunapinga Udikteta wa JPM na kuulani wakati sisi tunataka kupangia watu nani wa kuunga mkono ? Kwamba sababu hakukemea wakati au kile wewe ulichoona hakipo sawa hivyo chochote anachosema kuanzia hapo ni Pumba ?

Nadhani tungefika mbali sana kama tungekuwa tunapima na kujibu kilichowekwa mezani na sio nani amekisema.., Sababu Even a Broken Clock is Right Twice a Day; Na being personal kunapunguza muda wa kujikita kwenye concrete issues...
 
Mkuu, uliunga mkono juhudi enzi ya JPM ukajua atakupa cheo, na yeye akafa, ukatoka patupu, heshima huna na cheo huna, miaka ile ungekuwa na comments elfu tanunaishi

Ulishapoteza Credibility baada ya kununuliwa na yule mwovu na kugeukia upande wa watesi!! Nakushangaa hii nguvu ya kutamka haya unaitoa wapi? Si ulikua upande wa aliyetaka kutawala milele?

Siku zote muda ni hakimu wa yote.... ungejikalia kimya tuu kuliko kujaribu kukirudia kichaka chako cha zamani, huaminiki zaidi sana unatia kinyaa!!
Duh..mnafikiri nilikosoea? Mliosema "alipo tupo" hamjakubali tu labda JPM Alienware shule nyingine. Mliposhangilia kifo chase nilidhani Tanzania ingekuwa inapaa....uko mitaani watu wanammiss jembe wao...Mungu amlaze pema peponi na kumbukumbu lake liendelee kusimuliwa vizazi vingi vijavyo. Amina.
 
Tanesco wanasaidia sana sio kwamba hawafanyi kazi hapana maana ukisema toka uhuru hadi sasa umeme umesambaa eneo kubwa sana nchi hii.

mimi ninachokiona uhitaji wa nishati ya umeme ni mkubwa kuliko budget ya serikali hao tanesco wanasubili bunge na serikali iwape pesa na bahati mbaya wanapata mgao kiduchu

Tanesco hawana pesa zao mfukoni.
Hakuna mkandarasi mbobevu au mkurugenzi eti yupo teyari kukaa sehemu ili ashindwe tatizo ni pesa na bahati mbaya zaidi hii nchi ilivyo ya hovyo wanasiasa ndio watoaji pesa haohao ndio wachukuaji 10 percent ya hizo pesa na haohao ndio watumbuaji ili wao wajikoshe..
Siyo lazima uonekane umeandika hata kama huna facts zozote. Mleta mada kaja na hoja nzito na nyeti kwa mstakabali wa maendeleo ya taifa letu lakini wewe unakuja na ngonjera za Tanesco hugawiwa hela na serikali! Tanesco hawauzi umeme? Una uhakika kuwa bunge hupitisha bajeti ya Tanesco?
 
Duh..mnafikiri nilikosoea? Mliosema "alipo tupo" hamjakubali tu labda JPM Alienware shule nyingine. Mliposhangilia kifo chase nilidhani Tanzania ingekuwa inapaa....uko mitaani watu wanammiss jembe wao...Mungu amlaze pema peponi na kumbukumbu lake liendelee kusimuliwa vizazi vingi vijavyo. Amina.
Teh teh teh... ko ulifurahia mateso ya upinzani kisa Slaa hakugombea? Shida yenu ilikua ugombea? Nafsi inakusuta sana we mnafiki.

Muda umewahukumu vikali sana...
 
Nani kasema Dr. Slaa hakugombea? Kama hakugombea Nani aligombea? Muda haujatuhukumu sisi tuliopinga mabadiliko ya kuzungurusha mikono. Muda na historia itawahukumu tena vitality mwakani kwa kusaliti harakati zilizomwaga damu za upinzani.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Sikuwahi kuelewa kwanini wakati mwingine mtu anapokuwa na mawazo au ametatizika kimawazo anaanza kujikuna nywele. Au mtu anakuuliza jambo halafu hauna jibu unaanza kujishika kidevu au unakuna nywele hata kama haziwashi! Maswali au mambo mengine wakati fulani yanakwaza na yanaweza kukufanya ufike mahali utamani kujinyofoa nywele.

Mojawapo ya maswali ambayo yameanza kunijia siku hizi za karibuni ni hili kuhusu "ndugu zetu hawa". Hawa ndugu zetu wamekuwa wakija kila baada ya miaka mitano kuomba uongozi; wanabembeleza tena wameshika kakitabu kanaitwa "Ilani ya Uchaguzi". Ukiishika hiyo Ilani imejazwa maneno na ahadi nyingi tena ziko kwenye vifungu vyenye namba ili usindishwe kunukuu. Watakuja na muziki na bendi; vikundi vya sarakasi, na ngoma za kienyeji na ngonjera! Wakati mwingine watawaalika waimba mashairi na tenzi zenye mwendo wa taarab kabambe!

Yaani, ukichukua Ilani ya Uchaguzi ya chama chao kuanzia tu na mwaka 1995 hadi sasa kuna ahadi zimetolewa humo kuhusu suala la nishati na tatizo la umeme nchini hadi unajiuliza hivi huwa wanakumbuka walichoahidi miaka mitano kabla yake? Au inawezekana kila unapokaribia uchaguzi mwingine wanaanza kuangalia na kusema "duh mbona tatizo bado lipo, hebu tuahidi tena"! Halafu wanakaa na kuja na ilani nyingine halafu tunarudia tena.

Sasa tatizo sijui ni wanasiasa au ni watendaji. Hili ndilo linanileta kwenye swali la leo. Hivi kuna uwezekano hawa ndugu zetu waliingia shuleni lakini shule haikuwaingia? Hivi watu wote waliosomea shahada za sayansi na saa katika umeme, utawala, uongozi na menejimenti; wote waliosomea mambo ya fedha n.k Hivi ni kweli kabisa hawa watu wameshindwa kabisa kutatua hili tatizo la umeme? Yaani, tunachoshuhudia hadi leo hii ni upeo wa uwezo wao!

Huwa nasema "upeo wetu, ndio ukomo wetu". Yaani, ukijumlisha elimu ya watu wote kwenye serikali - wizara, idara, na wakala mbalimbali; yaani ukijumlisha uwezo wao wote jumla yake ni "tatizo la umeme". Yaani, kwa miaka yote hii walipoenda shule, kozi, na mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi ukijumlisha vyote hivyo jumla yake ni hii: Tatizo lisiloisha la umeme. Yaani, kukatika katika kwa umeme, mgao wa mara kwa mara n.k yote haya ni jumla ya elimu ya viongozi na watendaji ndani ya serikali hadi mitaani kabisa.

Ndio maana leo najiuliza; hivi hawa wenzetu wanaosimamia sekta hii ya umeme kwa miaka yote hii walipoenda shule ambapo walisifiwa kuwa hawakupata makarai au mayai; kwamba wanasiwa kuwa wao ndio walikuwa "vipanga"; yaani maprofesa waliowafundisha na wanafunzi waliosifiwa kuwa walipata "Upper Class" kwenye shahada zao za uzamaji, uvumaji, uvumbivu na uvunjifu yaani hawa ndugu walichosomea kilikuwa kitu gani?

Yaani, mnataka kabisa tuamini kuwa kama taifa na tunapoelekea miaka 60 ya Muungano uwezo wa wasomi wetu wabobezi ndio huu kwenye sekta ya umeme? Yaani, haya ndiyo matunda ya kujivunjia ya muungano? Au kuna kitu kingine walikisomea wenzetu hawa?
Umeme umekatika huku muda huu vp huko??
 
Nani kasema Dr. Slaa hakugombea? Kama hakugombea Nani aligombea? Muda haujatuhukumu sisi tuliopinga mabadiliko ya kuzungurusha mikono. Muda na historia itawahukumu tena vitality mwakani kwa kusaliti harakati zilizomwaga damu za upinzani.
Haha, huna tofauti na kima anayecheka uchi wa mwenzie. Babu najua imekuchua muda sana akili yako kurudi kwenue default mode! We una upinzani gani zaidi ya kufuata ushawishi wa yule kahaba ili usaliti mapambano?
Siasa za magufuli zimewadhalilisha sana wanaharakati uchwara sahv mnatafuta mtoke vipi!! Utawala wa yule Kichaa umewaacha uchi!
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Sikuwahi kuelewa kwanini wakati mwingine mtu anapokuwa na mawazo au ametatizika kimawazo anaanza kujikuna nywele. Au mtu anakuuliza jambo halafu hauna jibu unaanza kujishika kidevu au unakuna nywele hata kama haziwashi! Maswali au mambo mengine wakati fulani yanakwaza na yanaweza kukufanya ufike mahali utamani kujinyofoa nywele.

Mojawapo ya maswali ambayo yameanza kunijia siku hizi za karibuni ni hili kuhusu "ndugu zetu hawa". Hawa ndugu zetu wamekuwa wakija kila baada ya miaka mitano kuomba uongozi; wanabembeleza tena wameshika kakitabu kanaitwa "Ilani ya Uchaguzi". Ukiishika hiyo Ilani imejazwa maneno na ahadi nyingi tena ziko kwenye vifungu vyenye namba ili usindishwe kunukuu. Watakuja na muziki na bendi; vikundi vya sarakasi, na ngoma za kienyeji na ngonjera! Wakati mwingine watawaalika waimba mashairi na tenzi zenye mwendo wa taarab kabambe!

Yaani, ukichukua Ilani ya Uchaguzi ya chama chao kuanzia tu na mwaka 1995 hadi sasa kuna ahadi zimetolewa humo kuhusu suala la nishati na tatizo la umeme nchini hadi unajiuliza hivi huwa wanakumbuka walichoahidi miaka mitano kabla yake? Au inawezekana kila unapokaribia uchaguzi mwingine wanaanza kuangalia na kusema "duh mbona tatizo bado lipo, hebu tuahidi tena"! Halafu wanakaa na kuja na ilani nyingine halafu tunarudia tena.

Sasa tatizo sijui ni wanasiasa au ni watendaji. Hili ndilo linanileta kwenye swali la leo. Hivi kuna uwezekano hawa ndugu zetu waliingia shuleni lakini shule haikuwaingia? Hivi watu wote waliosomea shahada za sayansi na saa katika umeme, utawala, uongozi na menejimenti; wote waliosomea mambo ya fedha n.k Hivi ni kweli kabisa hawa watu wameshindwa kabisa kutatua hili tatizo la umeme? Yaani, tunachoshuhudia hadi leo hii ni upeo wa uwezo wao!

Huwa nasema "upeo wetu, ndio ukomo wetu". Yaani, ukijumlisha elimu ya watu wote kwenye serikali - wizara, idara, na wakala mbalimbali; yaani ukijumlisha uwezo wao wote jumla yake ni "tatizo la umeme". Yaani, kwa miaka yote hii walipoenda shule, kozi, na mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi ukijumlisha vyote hivyo jumla yake ni hii: Tatizo lisiloisha la umeme. Yaani, kukatika katika kwa umeme, mgao wa mara kwa mara n.k yote haya ni jumla ya elimu ya viongozi na watendaji ndani ya serikali hadi mitaani kabisa.

Ndio maana leo najiuliza; hivi hawa wenzetu wanaosimamia sekta hii ya umeme kwa miaka yote hii walipoenda shule ambapo walisifiwa kuwa hawakupata makarai au mayai; kwamba wanasiwa kuwa wao ndio walikuwa "vipanga"; yaani maprofesa waliowafundisha na wanafunzi waliosifiwa kuwa walipata "Upper Class" kwenye shahada zao za uzamaji, uvumaji, uvumbivu na uvunjifu yaani hawa ndugu walichosomea kilikuwa kitu gani?

Yaani, mnataka kabisa tuamini kuwa kama taifa na tunapoelekea miaka 60 ya Muungano uwezo wa wasomi wetu wabobezi ndio huu kwenye sekta ya umeme? Yaani, haya ndiyo matunda ya kujivunjia ya muungano? Au kuna kitu kingine walikisomea wenzetu hawa?
Kusomeshwa siyo kuelimika. Unachotakiwa kukifanya ni ku"soma" wewe mwenyewe.
 
M.M Mwanakijiji being amongst the greatest wa ili jukwaa na nyaraka zako za siri miaka hiyo ambayo wachangiaji wa leo wa hili jukwaa la siasa hawakujui wewe ni nani na uzito wa michango yako kufanya hadi serikalini kushinda jukwaa la siasa.

That’s a while ago wachangiaji wale wa amsha amsha zako, bila ya kupewa elimu awawezi kujua uzito wako kwenye kuinua hili jukwaa.

Hakina Zomba ambao walikuwa wanaogopa kutumia ID za kike miaka ile siku hizi wanajiachia na ID zinazo reflect gender zao na kujifanya walimu wa lugha.

Werevu wa miaka yako washakimbia hili jukwaa siku hizi asilimia kubwa ni watoto wa UVCCM na BAVICHA na siada za uchawa badala Ya kujibu hoja.

That was to remind JF wachanga M.M.M ni nani, huko kwenye concerns za elimu ya hawa watu walio kwenye uongozi ni kupoteza muda wenyewe wameshaamua bora liende. Mifano ni mengi ya kuelezea this people are not serious.

Just paying homage

Hii sio nchi ya meritocracy as you wish ndio maana ipo ilipo.
Bahati mbaya sana Mzee Mwanakijiji naye aligeuka kuwa Chawa Kunguni wa JPM, so sad!
 
Back
Top Bottom