Swali la wakina dada

Swali la wakina dada

Habari za wakati huu.

Ama mimi mawazo yangu ni toauti na wengine labda inagwa nakubaliana na aliyesema kwamba wanawake wengi wanapenda mwanamme mwenye pesa lakini nimefurahi sana kusikia kuwa sio wanawake wote.

Mimi ni mwanamke lakini lakini kitu ninachokichukia ni mwanmme mwenye pesa na nina sababu zangu. sababu ya kwanza imani yangu inanielekeza kuwa mwanamme mwenye pesa atanisumbua kwa kunisimbulia lakini pia atajiona ananilazimisha nimpende kutokana na fedha zake. lakini pia atakuwa akichukua wanawake nikimgundua anaweza kunitovukia adabu kwa kusema kwani unajali nini fedha si zangu mwenyewe?

Kwa kweli kwenye mapenzi ya kweli nadhani mtu haangalii pesa wala nini ni mapenzi ya dhati kama yapo hiyo pesa inakuja by the way tu.

kuhusu wanawake kupenda fedha hilo linalotokana na mambo mawili moja umasikini kutokana na jengine ni tamaa kuwekwa mbele kwa sababu hasa wale vijana wa wenye tabia ya kwenda kujirusha wanataka kubadilisha magauni kila wanapotoka nje sasa watapata wapi hizo fedha za kubadilisha badilisha mavazi wasipopenda wanaume wenye nacho jamani?. please mimi simo katika hao.

Tukija kwa upande mwengine maana mimi napenda sana ku balance wapo wanaume wneye kupenda wa mama wenye pesa pia na hao mara nyingi huwa ni vijana ambao hupenda kujirusha mitaani na kwenye vilabu hawa nao wanawategemea sana wanawake wenye pesa ili wapate kutimiza malengo yao ya kupata wasichana wadogo wanaolingana na wao na jengine kujionesha kwa vijana wenzao kuwa wana gari na kila kitu cha kisasa.

lakini kwa upande wa wanawake wenye pesa wakipata wanaume hawana pesa wanapoamua kuwasimbulia laaaa laaa kuwashinda hao wanaume kwa masimbulizi maana uanweza mwanamme ukasema basi kama ni pesa yako basi bora nisamehe lakini unajua tena penye kitu fedha utakaa aaaa ukifkiri ujidai kukatisha amwasiliano siku moja lakini siku ya pili unarudi kuomba radhi ...e bwana weee mambo makubw ahaya yaani kwenye mambo haya we acha tu ndio mapmbo ya mapenzi eti.. mmmh.

bye
 
Stonetown pesa sio kitu katika mapenzi na mahusiano ya ukweli na haki , sema tu watu wanaiga wengine wanafanya nini na kufanya kama sehemu ya maisha yao lakini ni ukweli uliowazi kwamba katika mapenzi ya kweli na dhati ni rahisi zaidi kujipanga kushirikiana na kutafuta hizo pesa kwa pamoja .

Kwahiyo nawashauri watu vijana wenzangu hata unapoamua kuwa na mtu kwanza angalia mnaendana kwa kufanana baadhi ya vitu , je mipango yenu ni nini hapo baadaye je mipango hii unashirikiana na mwenzako au wewe mwenyewe ni vizuri ukamshirikisha mwenzako kwa faida zenu nyie wenyewe .

Mara nyingi kunatokea matatizo katika mahusiano mengi haswa yanayohusu pesa kwa sababu ya watu kuficha baadhi ya vitu na kukataa kushirikiana na mwenzi wake kwa asilimia nyingi au zaidi .

Kwangu mimi my gal is 1 others follow

let our love shine through the world
 
mimi naona pesa ni muhimu.
wanaume wenyewe wanajiamini wakiwa na pesa.
mwanaume anayejiamini katika mambo yake ni mzuri kuliko ambaye hana self confidence.
Bora mwenye kujiamini kwa decisions zake kuliko ambaye anahisi mara kalogwa, mara unamdharau etc.
 
Nyie wanaume bwana kila kitu tufanyacho wanawake si sawa, mwanamke akiwa na pesa mnamuogopa ati atawanyanyasa, akifanya kazi kwa bidii ili ainue kipato cha familia mnalalamika hampati matunzo mnaanza kutoka na nje, akihitaji za kwako anakuchuna,akipenda mwanaume mwenye pesa mnalalamika sasa atakupenda tuu bila kujua social and economic security yake na yako??
 
SWALI:Sasa mimi nauliza kwa nini wasichana wengi wanapenda wanaume wenye pesa hata kama wana uwezo wa kupata pesa pia.Kwa nini wasijiamini nao kama wanaume na kufikiria kuwa pesa siyo jambo la maana sana kama unampenda mwenzio?

pesa nimatokeo tu ingawaje pesa ndio kila kitu kalika maisha ya binadamu.
 
Pesa Pesa Pesa - unapoongelea Pesa kwenye mahusiano - ina maana ndio inawafanya watu wengine wasioweza kuipata kwa kutoa jasho kama Mungu alivyoagiza - wawe mafisadi, majambazi etc. Nadhani wanawake wanapenda wanaume wanaopata hela zao kiuhalali - lakini kama mwanamke atampenda mwenzi wake kwa pesa bila kupima zinatoka wapi - hapo tena kuna tatizo
Katika mahusiano UPENDO unavumilia hata kama pesa haitoshi. Halafu issue ya mashemeji kuwa sehemu ya familia ya mume na mke sio sawa - imefikia wakati Watanzania tubadili kidogo culture yetu ya extended family - utakuta mtu baada ya kupata pesa badala ya kutengeneza familia yake anataka sifa ya kumwaga sifa kwa mashemeji - nisemavyo MIMI
 
Kwa kweli mimi nashindwa kabisa kuelewa pesa ina nafasi gani muhimu katika mapenzi ya kweli nadhani umuhimu wa pesa katika mahusiano ni mtu kutaka kwenda juu kwa kupitia mgongo wa mwenzie au woga wa kuishi maisha yasiyo ya pesa (kwa wale wenye pesa wanaotaka kupata wenye nazo wenzao tu) kwa mtazamo wangu mimi kuwa na pesa kunaweza kuwa mzigo tu kuliko hata kutokuwa nazo, nani ambaye anaweza akasimama akasema anapesa karidhika na kusema baaasi hizi zinatosha!!?

Binadamu anavyozipata pesa zaidi ndio anavyozihitaji zaidi na ndio anavyozitafuta zaidi…na pesa zinaweza kusababisha insecurity kwa aliyenazo zaidi hata ya asiyenazo… kwa sababu mwenye pesa anakuwa kwenye presha akifikiria na ku fanya kazi ya ziada ku zi keep, mambo yakiyumba kidogo utamwona atakavo panic kuzikumbatia hizo hela, aki lose hata kama ni kiasi kidogo tu inakuwa kaaazi kwelikweli hata kwenye utapeli/ufisadi/wizi/uchawi atageukia tu almradi angalau asirudi kwenye kupanda daladala….

hata wenye utajiri mkubwa wanaodai wanausecurity ya kutosha kulinda mali zao bado hawapo excluded kwenye kufilisika na wanajua hilo na linawapa tumbo joto, ukiwaona outward utadhani wana raha sana, lakini ukiwa karibu nao mbona utajua mengi?

kama asiyenazo anakuwa kwenye presha akifikiria jinsi ya kuzipata na aliyenazo anakuwa kwenye presha ya kuzikeep na kupata zaidi ina maana fedha kama ilivyo haina msaada wowote kwenye mapenzi,

mie naona wawili wakipendana washirikiane, wasaidiane katika hali yoyote ile, watafute wote, waridhike na walichonacho (ni rahisi zaidi kuridhika kama huna pesa nyingi kuliko ukiwa nazo) maisha yakiwa ya dhiki au ya pesa (kuna waliolala matajiri wakaamka masikini na waliolala masikini wakaamka matajiri) washikamane pamoja wakati huo huo wa concentrate kwenye maswala yenye uzito ktk kuimarisha penzi lao
 
SWALI:Sasa mimi nauliza kwa nini wasichana wengi wanapenda wanaume wenye pesa hata kama wana uwezo wa kupata pesa pia.Kwa nini wasijiamini nao kama wanaume na kufikiria kuwa pesa siyo jambo la maana sana kama unampenda mwenzio?

mnani hapendi chips kuku jamani
 
Habari za wakati huu.

Ama mimi mawazo yangu ni toauti na wengine labda inagwa nakubaliana na aliyesema kwamba wanawake wengi wanapenda mwanamme mwenye pesa lakini nimefurahi sana kusikia kuwa sio wanawake wote.

Mimi ni mwanamke lakini lakini kitu ninachokichukia ni mwanmme mwenye pesa na nina sababu zangu. sababu ya kwanza imani yangu inanielekeza kuwa mwanamme mwenye pesa atanisumbua kwa kunisimbulia lakini pia atajiona ananilazimisha nimpende kutokana na fedha zake. lakini pia atakuwa akichukua wanawake nikimgundua anaweza kunitovukia adabu kwa kusema kwani unajali nini fedha si zangu mwenyewe?

Kwa kweli kwenye mapenzi ya kweli nadhani mtu haangalii pesa wala nini ni mapenzi ya dhati kama yapo hiyo pesa inakuja by the way tu.

kuhusu wanawake kupenda fedha hilo linalotokana na mambo mawili moja umasikini kutokana na jengine ni tamaa kuwekwa mbele kwa sababu hasa wale vijana wa wenye tabia ya kwenda kujirusha wanataka kubadilisha magauni kila wanapotoka nje sasa watapata wapi hizo fedha za kubadilisha badilisha mavazi wasipopenda wanaume wenye nacho jamani?. please mimi simo katika hao.

Tukija kwa upande mwengine maana mimi napenda sana ku balance wapo wanaume wneye kupenda wa mama wenye pesa pia na hao mara nyingi huwa ni vijana ambao hupenda kujirusha mitaani na kwenye vilabu hawa nao wanawategemea sana wanawake wenye pesa ili wapate kutimiza malengo yao ya kupata wasichana wadogo wanaolingana na wao na jengine kujionesha kwa vijana wenzao kuwa wana gari na kila kitu cha kisasa.

lakini kwa upande wa wanawake wenye pesa wakipata wanaume hawana pesa wanapoamua kuwasimbulia laaaa laaa kuwashinda hao wanaume kwa masimbulizi maana uanweza mwanamme ukasema basi kama ni pesa yako basi bora nisamehe lakini unajua tena penye kitu fedha utakaa aaaa ukifkiri ujidai kukatisha amwasiliano siku moja lakini siku ya pili unarudi kuomba radhi ...e bwana weee mambo makubw ahaya yaani kwenye mambo haya we acha tu ndio mapmbo ya mapenzi eti.. mmmh.

bye
S.T una mme/mchumba?
 
Back
Top Bottom