Swali la Wiki: Uzushi gani maarufu ambao umetawala mitazamo ya watu kwa muda mrefu?

JamiiCheck

Member
Joined
Nov 3, 2023
Posts
98
Reaction score
122

Baadhi ya Taarifa za Uzushi zimekuwepo kwa muda mrefu na kurithishwa kizazi hadi kizazi, hivyo kuathiri mitazamo ya watu

Je, ni Uzushi gani maarufu ambao umetawala mitazamo ya watu kwa muda mrefu?

Ili kujua Uhalisia wa Taarifa unazokutana nazo, tembelea Jukwaa la JamiiCheck
 
Uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
 
Kumiliki bunduki/ bastola ni mpaka uwe tajiri. Huu uzushi umefanya tuone kile mwemye bastola ni tajiri kumbe wapiii.​
 
Kuona nyota ya jah. Wanasema Bakhresa alikuwa fundi viatu Ila alipopata bahati ya kuona nyota ya jah akatajirika.
 
Mvua ikiwa inanyesha huku jua linawaka, tuliambiwa "ujue Simba anazaa" .

Ukiwa umekaaa huku umenyoosha miguu, akaja mtu mwingine kakuruka kukatiza miguu yako, basi, ujue hautakua (kurefuka).
 
Bila Ccm hakuna Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…