Swali langu la leo!

Hamza Nsiha

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
221
Reaction score
197
Habari za muda huu ndugu wana jukwaa la Habari na hoja mbalimbali. Leo hii ninapenda kuwashirikisha jambo mojawapo ambalo limekuwa likitukwamisha katika maeneo mbalimbali hususani katika masuala ya madili/fursa.

Je! Ni kwanii watu wengi hupenda kupuuzia fursa mbalimbali zinazojitokeza kwa kuamini kuwa zitakuwa zimesha_fikiwa na watu wengi?

Mfano, Suala la sensa lilipokuja kuna baadhi ya watu walighairi kuomba nafasi katika ngazi ya ukarani, usimamizi wa maudhui na usimamizi wa tehama kwa kuwa waliona ni vigumu sana kupata nafasi hizo. Lakini walipoona majina yamerudishwa kwa ajili ya usaili ndipo wakashtuka kuona kumbe inawezkana.

Pia, katika shindano lililopo la STORIES OF CHANGE watu wengi tunaogopa kujaribu kwa sababu tunaamini kuwa uwezo wetu katika kuandaa maudhui unaweza usiwe bora ukilinganisha na watu wengine kwa sababu ya uwingi wa watu waliyoiona fursa.

Je, ni wangapi walishawahi kukosa dili la wazi au fursa kwa sababu tu ya kupuuza na kuamini kuwa ni vigumu kulipata dili hilo?
Karibu ku_share experience!
 
Nitakuwepo hapa kwa ajili ya Michango yenu
 
Umeeleza unataka kutushirikisha jambo moja.Weye ukiangalia vizuri ni kweli umetushirikisha jambo moja au majambo mengi?
 
Umeeleza unataka kutushirikisha jambo moja.Weye ukiangalia vizuri ni kweli umetushirikisha jambo moja au majambo mengi?
Jambo linahusu zaidi jinsi wengi wetu tunavyopishana na fursa lkn hayo mengine ni kama mifano hai mkuu!
 
Kujuana kumezidi, huko sensa tu aliyefanya usaili naye kajiingiza na mkewe na hawara zake,

Nafasi zilitakiwa 20 wasaili walikuwa 4 hivi kijana atapata hiyo nafasi ?

Hili shindano la jf ngoja nijikalie kimya sitaki life ban
 
Ukilitimba kujuana na rushwa ndio TATIZO kwenye jamii zetu!
Ongeza majungu wivu na fitina!
 
Mbona watu tunajaribu sana.Sijui umesema haya kwa kurejea wapi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…