Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 578
Nina swali dogo kwa walimu wenzangu Tanzania. Hivi inakuwaje wengi hampendi kutambulika kama walimu? Utamwona mwalimu ameandika kwenye profaili yake ya Facebook kuwa yeye ni Education Officer, Education Administrator n.k. Hivi kwa nini msiziache hizo kazi kama hamzipendi?
Ushauri:
Msiionyeshe dunia kama mko kwenye fani hiyo kwa bahati mbaya. Onyesheni kwamba mko kwenye fani hiyo kwa sababu mnaipenda na mmeisomea. Japokuwa serikali na Chama Tawala wameifanya hiyo fani ionekane haina thamani, ni jukumu la wenye fani kuiinua na kuifanya ithaminike mbele ya jamii. Je, mwakumbuka enzi za midahalo (debate) shuleni kukiwa na mada (motion) kama "A TEACHER IS BETTER THAN A DOCTOR"?