Swali: Mbinguni Kuna sikukuu ya Christmas 25 December?

Mzee una akili fupi sana. Unaulizaje swali kama hili???
 
Ishu ya x-mass haijawahi kuwa tatizo kwangu hata siku Moja SAWA na ishu ya siku ya kuabudu, namna sahihi ya kuabudu, suala la ubatizo, utatu mtakatifu, vyakula na vinywaji, pasaka na mambo mengine yafananayo na hayo.

Huwa nafanya kile nikiaminicho na nikiaminicho ni kile ambacho nafsi yangu imekisadiki toka katika maandiko matakatifu. Nikikutana na wenzangu niwaonao kuwa na Imani sawa na yakwangu Huwa namshukuru Mungu, lakni pia nikutanapo na wenzangu waaminio tofauti na vile niaminivyo Mimi huwa namshangaa Mungu kwa namna afanyavyo kila jambo SAWA na apendavyo. Kikubwa uzima na kuomba kukubalika kwa Mungu siku nikimuona, yaaani mwisho mwema.
 
Unajua kuwa umeamrishwa kuhubiri injili Kwa Kila kiumbe?

Usipowahubiri, wakaangamia bila we kuwaambia Kweli, utadaiwa siku ya mwisho,

Wambie Kweli ya Mungu usione Aibu na kujificha nyuma ya sababu za kuwaheshimu.
 
Yako wazi kabisa,

Asili ya 25 December ni Babeli, warumi wamecoppy huko na kuingiza Kanisani Kwa Siri.

Sasa tunatakiwa kuyachunguza maandiko.
Ninachofahamu kwanza biblia imekuja kuandikwa miaka zaidi ya 500 baada ya kuanza kwa Ukristu. Hivyo biblia sio kitabu kilicholeta ukristu wala kuanzisha ukristu, kukitumia kujua chimbuko la desturi za kikristu ni kupoteza muda.

Pili dhumuni la kutungwa kwa biblia lilikuwani kufanya wakristu waungane hasa kwa maslahi ya kiutawala na kisiasa zaidi kuliko kiimani ndio maana hadi leo biblia imekuwa ikibadilika badilika kukidhi matakwa/dhima yake hiyo kuu.

Kiuhalisia kabisa biblia sio kitabu kitakatifu bali inaitwa biblia takatifu. Haya ni mambo mawili tofauti sana.

Haya ni madokezo machache ninayoweza kuyaweka hapa.
 
NENO la Mungu ni pumzi ya Mungu, Haina mwanzo Wala mwisho,

Adam na EVE ndani ya Eden walimwabudu Mungu na kusikia neno la Mungu bila tatizo lolote.
 
Sawa. Ina make sense.

Lakini mimi nitaungana na watu wote duniani kusherehekea Christmas tarehe 25 December maana mimi ni mti mbichi mweupe ninaye zaa matunda leo na kesho hadi wakati wa uzee.Yesu Kristo alizaliwa na Bikra Maria tarehe unayoijua wewe ila Yesu Kristo anazaliwa rasmi ndani yangu tarehe 25 Mwezi wa kumi na mbili.
 
Rabon katafute au Kasome kwa Undani kuhusu Sol invictus na Ilikuwaje ikawa Xmass..
Sol Invictus & Christmas..
 
Point kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…