Swali: Mbinguni Kuna sikukuu ya Christmas 25 December?

Swali: Mbinguni Kuna sikukuu ya Christmas 25 December?

Salaam, Shalom!

Msingi wa SWALI LANGU upo katika Sala Aliyotufumdisha Yesu sisi wanafunzi wake kusali Kwa hiyo, kwamba;

(Mathayo 6:10)
"Mapenzi Yako yatimizwe, hapa duniani kama ilivyo Mbinguni "

Swali no 1.
Kusherehekea Christmas tarehe 25 December ni mapenzi ya Mungu aliye Mbinguni?

Swali no 2:
Ni mapenzi ya Mungu kusherehekea Christmas tarehe 25 December tarehe hiyo hiyo pakiwa na sherehe hizo hizo Mbinguni?

Na msingi wa SWALI hili ujibiwe kupitia Katiba yetu Wana wa Mungu iitwayo BIBLIA.

Ikiwa unapenda kuwa raia wa Mbinguni Ukiwa duniani, fuatisha Sala hii,

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMIN

Karibuni 🙏
Mzee una akili fupi sana. Unaulizaje swali kama hili???
 
Ishu ya x-mass haijawahi kuwa tatizo kwangu hata siku Moja SAWA na ishu ya siku ya kuabudu, namna sahihi ya kuabudu, suala la ubatizo, utatu mtakatifu, vyakula na vinywaji, pasaka na mambo mengine yafananayo na hayo.

Huwa nafanya kile nikiaminicho na nikiaminicho ni kile ambacho nafsi yangu imekisadiki toka katika maandiko matakatifu. Nikikutana na wenzangu niwaonao kuwa na Imani sawa na yakwangu Huwa namshukuru Mungu, lakni pia nikutanapo na wenzangu waaminio tofauti na vile niaminivyo Mimi huwa namshangaa Mungu kwa namna afanyavyo kila jambo SAWA na apendavyo. Kikubwa uzima na kuomba kukubalika kwa Mungu siku nikimuona, yaaani mwisho mwema.
 
Unajua kuwa umeamrishwa kuhubiri injili Kwa Kila kiumbe?

Usipowahubiri, wakaangamia bila we kuwaambia Kweli, utadaiwa siku ya mwisho,

Wambie Kweli ya Mungu usione Aibu na kujificha nyuma ya sababu za kuwaheshimu.
 
Yako wazi kabisa,

Asili ya 25 December ni Babeli, warumi wamecoppy huko na kuingiza Kanisani Kwa Siri.

Sasa tunatakiwa kuyachunguza maandiko.
Ninachofahamu kwanza biblia imekuja kuandikwa miaka zaidi ya 500 baada ya kuanza kwa Ukristu. Hivyo biblia sio kitabu kilicholeta ukristu wala kuanzisha ukristu, kukitumia kujua chimbuko la desturi za kikristu ni kupoteza muda.

Pili dhumuni la kutungwa kwa biblia lilikuwani kufanya wakristu waungane hasa kwa maslahi ya kiutawala na kisiasa zaidi kuliko kiimani ndio maana hadi leo biblia imekuwa ikibadilika badilika kukidhi matakwa/dhima yake hiyo kuu.

Kiuhalisia kabisa biblia sio kitabu kitakatifu bali inaitwa biblia takatifu. Haya ni mambo mawili tofauti sana.

Haya ni madokezo machache ninayoweza kuyaweka hapa.
 
NENO la Mungu ni pumzi ya Mungu, Haina mwanzo Wala mwisho,

Adam na EVE ndani ya Eden walimwabudu Mungu na kusikia neno la Mungu bila tatizo lolote.
 
Kuhusu Kuzaliwa Kwa Yesu Iko wazi,

Ni mwezi wa SITA Maria alikwenda kumtembelea Elisabeth mama aliyemzaa Yohana mbatizaji.

Sasa ikiwa Mariam akiwa na mimba ya mwezi mmoja Mwezi wa SITA, sasa hesabu miezi Tisa itatimia mwezi upi!!

Siku ya kuzaliwa na kufufuka Kwa Yesu inakuwa pamoja,

Hilo ni fumbo kuu,

Karibu thread itakayoongelea jambo Hilo.
Sawa. Ina make sense.

Lakini mimi nitaungana na watu wote duniani kusherehekea Christmas tarehe 25 December maana mimi ni mti mbichi mweupe ninaye zaa matunda leo na kesho hadi wakati wa uzee.Yesu Kristo alizaliwa na Bikra Maria tarehe unayoijua wewe ila Yesu Kristo anazaliwa rasmi ndani yangu tarehe 25 Mwezi wa kumi na mbili.
 
Warumi na Babeli wote walikuwa waabudu miungu na sanamu kabla ya Kristo YESHUA HAMASHIACH kuja duniani,

Sasa waliposhindwa kufuta wafuasi wa KRISTO duniani, wakaamua kuanzisha dini Yao ya mchongo na kuingiza Ibada za sanamu na Ibada za miungu Yao inayosherehekewa 25 December Ili wakristo wawe aabudu miungu indirect.

Mimi nlistuka mapema, sisherehekei Kwa namna hiyo siku na mwezi huo.
Rabon katafute au Kasome kwa Undani kuhusu Sol invictus na Ilikuwaje ikawa Xmass..
Sol Invictus & Christmas..
 
Labda na mimi nikuulize ni kalenda ipi na iliyo vumbiliwa nyakati zipi maana hii ya sasa mnayo tumia ni gregorian ya papa gregory moaka ya 1500s, sasa ni ipi inayo wadhihirishia kuwa siku ya sabato ni jumamosi ?na ndiyo siku iliyo tambuliwa na kutajwa na biblia.!? Unapo jibu ukumbuke kuwa mzunguko wa siku 7 za wiki ulivumbuliwa na nani na umeanza kutumiwa lini na kabla ya nyakati hizo usabato uliabudu siku gani?
Point kubwa sana
 
Back
Top Bottom