Swali moja tu kwa Felchesmi Mramba wa Nishati; huo umeme wa Ethiopia anaosema leo ni bei nafuu, mkataba unawazuia Ethiopia kupandisha bei milele?

Swali moja tu kwa Felchesmi Mramba wa Nishati; huo umeme wa Ethiopia anaosema leo ni bei nafuu, mkataba unawazuia Ethiopia kupandisha bei milele?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Bado tuna majibu mepesi mepesi na ya kisiasa kuhusu suala la kununua umeme toka Ethiopia. Kwanza tuliwauliza kama sisi tuna transmission losses kubwa kupeleka umeme mikoa ya kaskazini, Ethiopia hawana? Mkajibu kuwa kununua umeme ni sehemu ya kuimarisha usalama wa power supply nchini - ningewaona mna akili angalau mngesema line za Ethiopia zinatumia HVDC na za kwetu zipo kwenye HVAC hivyo sisi tuna losses zaidi kwa kila kilometer 100.

Sasa hili la kusema umeme wa Ethiopia una bei rahisi na kama kuna hasara sio suala letu, ni jibu pia halistahili kutoka kwenye mdomo wa mtu kama Mramba. Jibu lake linazua swali moja tu muhimu, kwamba huo mkataba tutakaotiliana sahihi na Ethiopia, una kipengele cha kutoongeza bei ya umeme kwa muda wote wa mkataba?

Kama sivyo, Mramba anapaswa kuwaeleza Watanzania, ni nini kitawazuia Wa Ethiopia kupandisha bei mara baada ya mkataba kuanza, hasa wakiona sasa Tanzania imekuwa tegemezi kwa umeme wa kutoka kwao?

Na Mramba anaposema kama kuna hasara sio suala letu, anawafanya Wa-Ethiopia ni wajinga kiasi gani ambao wako tayari kuuza umeme kwa hasara? In fact, kama wanatupa mkataba ambao tunajua wanatuuzia umeme kwa hasara, basi inabidi tushituke mapema. Mtu anapokuuzia kitu kwa bei ya hasara usikurupuke kununua,. Mramba hajui hili kuwa ni red flag katika biashara au mkataba wowote ule unaotakiwa kutia sahihi?
 
Aisee...
Ngoja nisubiri maelezo ya wataalamu, hata hivyo hongera mkuu kwa bandiko lako.
 
Aisee...
Ngoja nisubiri maelezo ya wataalamu, hata hivyo hongera mkuu kwa bandiko lako.
Asante Mkuu. Wataalamu wa serikalini huwa hawajibu maswali kama haya,maana wanajua msukumo ni wa kisiasa toka juu ambao hauwezi kupewa majibu ya kitaalamu
 
Back
Top Bottom