Swali muhimu kuhusu vifo vya Coronavirus

Swali muhimu kuhusu vifo vya Coronavirus

bizplan

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
592
Reaction score
574
Nimeguswa kuuliza swali hili.

Ikiwa kuna mgonjwa ambaye anasumbuliwa na saratani, TB, kisukari, kiharusi, tatizo la moyo na mengine yote yanayoua kirahisi na kwa haraka. Hali yake kwa ujumla ni ya mashaka muda wote. Mtu huyu akapata virusi vya korona akafa.

Swali la kwanza: Mtu huyu atakuwa kafariki kwa ugonjwa gani?

Swali la Pili: Ikiwa watu wengi wamepimwa na kukutwa na ugonjwa wa corona, na watu hawa hawakuwa na ugonjwa wowote mwingine. Watu hawa hawajatumia dawa yoyote na wamepona mwenyewe baada ya wiki.

Je, ni kweli ugonjwa huu ni tishio kiasi cha kuwekwa kuwa ni janga la dunia?

Swali la tatu: Ni kwanini dunia haisemi ukweli watu wanakufa kwa magonjwa gani?

Swali la nne: Je, unajua ni hofu kiasi gani ingejengwa ikiwa kila siku tungekuwa tunatangaziwa idadi ya wagongwa wanaokufa kwa magonjwa mbalimbali?

Ushauri: Serikali yetu ya Tanzania isifanye kosa la kutangaza vifo vya wagonjwa wa korona ikiwa mgonjwa huyo ana matatizo makubwa mengine ya kiafya yanayofahamika muda mrefu. Maana mtu huyo atakuwa amekufa kwa magonjwa mengine na siyo korona. Yaani magonjwa mengine yatakuwa yamechangia 90% huku corona ikiwa na 10% au chini ya hapo. Hivyo si sahihi kusema 10% imesababisha kifo wakati ipo 90% yenye madhara makubwa na imekuwepo muda. Kwa maana hiyo huyu mtu angekufa tu any time soon.

Lakini ikiwa mgonjwa hakuwa na historia yoyote ya ugonjwa unaofahamika na akakutwa na ugonjwa huu bahati mbaya kafariki. Basi ni sawa kusema kafariki kwa ugonjwa huu.

Tusiingie katika mkumbo huu.
 
Kwa hiyo shida hapo ni kutangazwa kwa vifo au vipi.
Yani unachosema ni sawa na mtu aje nyumbani kwako amekuta akiba ya ubwabwa akala ukaisha.

unaweza kusema akiba ilikua ndogo ukaeleweka na pia unaweza kusema mgeni kakumalizia akiba vyote ni sawa.

Ila kwenye hili la corona wengi severe pneumonia inawamaliza.
 
Kwa maana yako, UKIMWI hausababishi kifo.

Ukimwi unapoingia mwilini unaathiri kinga na mwisho mtu anapata magonjwa mengi nyemelezi na yanaweza kummaliza. Hivyo mtu huyu tunaweza sema Ukimwi umemuua.

Lakini huyu mgonjwa mwenye historia ya magonjwa fulani tena yanajulikana, nooo tusichanganye mambo.

Hata hivyo ikiwa tutafananisha na HIV basi hizi lockdown zitoke, watu waelimishwe kujikinga na maisha yasonge.
 
Mkuu chukulia mfano wewe unaumwa diabetes yako kwa miaka hata 15 ..unatumia dawa zako na umeshapanga diet vizuri hadi ikafikia kipindi diabetes iko under control.

Sasa akaja jamaa mmoja anaendesha gari kalewa akakugonga ukasustain injuries ambazo ni kubwa .. kutokana na ugonjwa wako wa diabetes(ambao ulikua ulishaukontroo kabla la ajari) ukasababisha vidonda vichelewe kupona ukapata sepsis ukafa..

Hivi hapo unadhani diabetes ndio imekuua? Je ungebaki na diabetes yako ungekufa?

Same applies kwa corona.. hao wati wanaokufa kwa corona sasa hivi unadhani kwa nini hawakufa kipindi corona haijafika.

Watu walikua wana presha zao ,cancer , DM ,CCF n.k lakini walikua wanaishi vizuri bila shida yoyote.. lakini corona ilipokuja ikafanya yake..
 
Mjomba Fujo,

Aaaaaaaahaaa mkuu umenichekesha this morning. Ukweli halisi ni kuwa hukuwa na akiba ya chakula hilo na mgeni ni zigo tu wamtwisha.
 
Si sahihi mkuu kwa ishu hii ya korona. Mtu huyu kwa kuwa anaumwa na tena amekuwa serious muda mrefu, angekufa tu soon.
Siyo kweli! Mtu mwenye HIV(au magonjwa mengine pia) bila ya Corona anaweza kuishi hata miaka 40,sasa kwa nini akifa ghafla baada ya kuvamiwa na Corona unataka tuseme kuwa amekufa kwa sababu ya HIV wakati bila ya Corona hapo angeishi miaka yake 40?
 
Kwa hiyo shida hapo ni kutangazwa kwa vifo au vipi.
Yani unachosema ni sawa na mtu aje nyumbani kwako amekuta akiba ya ubwabwa akala ikaisha, unaweza kusema akiba ilikua ndogo ukaeleweka na pia unaweza kusema mgeni kakumalizia akiba vyote ni sawa.
Ila kwenye hili la corona wengi severe pneumonia inawamaliza.

Na zaidi ambacho sikubaliani nacho naona kuna ukweli hausemwi na wakubwa wa dunia
 
Yani sawa na mtu aje akuazime usafiri wako, anatoka nje ya geti tu gari limeharibika halafu unasema ameharibu gari langu. Nimekuelewa mtona mada.
 
Mkuu sio kila kitu ulete dhihaka. Kitu ambacho huna ujuzi nacho sikiliza na angalia wenye uelewa nacho.

Wanasema mgonjwa kafa kwa corona kwa sababu kitaalam they are primary infectious, na hayo mengine secondary to corona infection.

(Kwa maana hao virus wanatengeneza msingi wa haya magonjwa mengine yatokee kwa watu ambao ni immunosuppressive au immune compromised)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ww unaumwa cancer halafu unakuja kufa kwa kushindwa kupumua kwa sababu ya lung infection (COVID-19) kilichokuua hapo si cancer bali ni Corona.

Chukulia kwa nn vifo vingi viko recorded Italy ama hata China katika kipindi hiki cha Corona kwa wazee na wenye other underlined medical condition na si wakati mwingine . Vifo vyao vimesababishwa na Corona. Hivyo vyeti vya vifo vitaandikwa Corona.

Hata watu wenye HIV vifo vyao huwa ni labda Pneumonia, TB, leukemia, Malaria n so on. HIV itself haileti kifo ila inapunguza kinga zako na kushambuliwa kirahisi na hayo magonjwa mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu chukulia mfano wewe unaumwa diabetes yako kwa miaka hata 15 ..unatumia dawa zako na umeshapanga diet vizuri hadi ikafikia kipindi diabetes iko under control...

Sasa akaja jamaa mmoja anaendesha gari kalewa akakugonga ukasustain injuries ambazo ni kubwa .. kutokana na ugonjwa wako wa diabetes(ambao ulikua ulishaukontroo kabla la ajari) ukasababisha vidonda vichelewe kupona ukapata sepsis ukafa..

Hivi hapo unadhani diabetes ndio imekuua?? Je ungebaki na diabetes yako ungekufa ??

Same applies kwa corona.. hao wati wanaokufa kwa corona sasa hivi unadhani kwa nini hawakufa kipindi corona haijafika.

Watu walikua wana presha zao ,cancer , DM ,CCF n.k lakini walikua wanaishi vizuri bila shida yoyote.. lakini corona ilipokuja ikafanya yake..
Okay mkuu. Kwa mfano wako huo huo. Ikiwa kuna mtu mwingine akapata injuries kwa case kama hiyo na akapata na corona vile vile ila yeye akapona. Huoni kuwa kilichomuua yule wa kwanza hasa hasa ni ugonjwa aliokuwa nao wa kisukari? Pamoja na kuwa aliweza kucontrol ila ingefika wakati hali ingekuwa mbaya tu.
 
Nimeguswa kuuliza swali hili.

Ikiwa kuna mgonjwa ambaye anasumbuliwa na saratani, TB, kisukari, kiharusi, tatizo la moyo na mengine yote yanayoua kirahisi na kwa haraka. Hali yake kwa ujumla ni ya mashaka muda wote. Mtu huyu akapata virusi vya korona akafa.

Swali la kwanza: Mtu huyu atakuwa kafariki kwa ugonjwa gani?

Swali la Pili: Ikiwa watu wengi wamepimwa na kukutwa na ugonjwa wa corona, na watu hawa hawakuwa na ugonjwa wowote mwingine. Watu hawa hawajatumia dawa yoyote na wamepona mwenyewe baada ya wiki.

Je, ni kweli ugonjwa huu ni tishio kiasi cha kuwekwa kuwa ni janga la dunia?

Swali la tatu: Ni kwanini dunia haisemi ukweli watu wanakufa kwa magonjwa gani?

Swali la nne: Je, unajua ni hofu kiasi gani ingejengwa ikiwa kila siku tungekuwa tunatangaziwa idadi ya wagongwa wanaokufa kwa magonjwa mbalimbali?

Ushauri: Serikali yetu ya Tanzania isifanye kosa la kutangaza vifo vya wagonjwa wa korona ikiwa mgonjwa huyo ana matatizo makubwa mengine ya kiafya yanayofahamika muda mrefu. Maana mtu huyo atakuwa amekufa kwa magonjwa mengine na siyo korona. Yaani magonjwa mengine yatakuwa yamechangia 90% huku corona ikiwa na 10% au chini ya hapo. Hivyo si sahihi kusema 10% imesababisha kifo wakati ipo 90% yenye madhara makubwa na imekuwepo muda.

Lakini ikiwa mgonjwa hakuwa na historia yoyote ya ugonjwa unaofahamika na akakutwa na ugonjwa huu bahati mbaya kafariki. Basi ni sawa kusema kafariki kwa ugonjwa huu.

Tusiingie katika mkumbo huu.
Dr Bizplan, MD, MMED (Clinical Microbiology), PhD (Virology)
 
Back
Top Bottom