Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Swali hili linahitaji jibu; jibu lake linaweza kuwa rahisi au gumu. Lakini ni jibu linalotegemea ujuzi wa historia. Ni jibu linalojaribu kuangalia kama uamuzi wa serikali ya Tanzania kutekeleza sheria kwa upendeleo (selective justice) ni uamuzi sahihi au ni miongoni mwa maamuzi mabovu kabisa yaliyowahi kuchukuliwa na watawala wetu. Na pia ni swali ambalo linauliza kama kutoa adhabu ya jumla (collective punishment) kwa kosa la Kagame ni jambo sahihi. Lakini pia ni lazima tujiulize baada ya muda uliotolewa kwa wahamiaji wageni kuondoka nchini wale waliobakia wakianza kutendewa vibaya na wenyeji serikali itawachukulia hatua hawa wenyeji au itawaachia kwa sababu wale ni wageni wahamiaji?
Quran na Biblia vinafundisha (na vinakubaliana kwa kiasi kikubwa) jinsi ya kuwatendea wageni wahamiaji katika nchi; na haihusishi kuwafukuza kwa nguvu! Katika Biblia kuna uhamiaji wa aina nyingi ambao wote una mafunzo kwa waamini; kuna uhamiaji wa Ibrahim (Abram) toka Uru wa Wakaldoyo kwenda nchi ya ahadi; kuna uhamiaji wa Yusuph kwenda Misra (baada ya kuuzwa na nduguze) na uhamiaji wa kundi kubwa la Waisraeli Misri; kuna uhamiaji (katika Agano Jipya) wa Yesu Masihi kwenda Misri pia baada ya kutafutwa na Herodi auawe akiwa kichanga.
Katika Uislamu bila ya shaka somo kubwa kabisa la uhamaji (hijra) ni ule wa Mtume Mohammed kutoka Mecca kwenda Madina. Ni uhamiaji mkubwa na muhimu sana katika Uislamu kiasi kwamba mwaka wa kwanza katika Kalenda ya Uislamu unaanzia katika tukio hilo (Al Hijra) la mwaka 622 (AD). Ujio wa Mohammed Medina ulitenganisha matendo aliyotendewa na njama alizotendewa na watu wa Mecca hadi kumlazimisha yeye na waamini wa mwanzo kuondoka hapo kwenda Medina katika hali ya kificho na hatari tupu!
Dini zetu kubwa hizi mbili (hata ya Kiyahudi) zinatufundisha kuwatendea wageni vizuri; haijalishi kama walihamia kihalali au la. Tuweke utaratibu mzuri wa kuwashughulikia na kuwahalalisha au hata kuwarudisha makwao katika heshima inayotokana na utu wao. Tukumbuke kuwa Katiba yetu inasema (Ibara 12 hadi 13) kuwa:
Utaona kuwa Ibara hizo hazisemi "kila Mtanzania" au "Kila raia wa Tanzania" na wala hazisemi "Kila aishiye TAnzania"! Zinasema kuwa "Kila mtu" anazaliwa akiwa huru na ni wote ni sawa! Yaani, Mhaya wa Kagera na Mkurya wa Tarime wote ni sawa! Kwamba inasema "Kila mtu anastahili heshima na haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake"; yaani Mndengereko na Mzaramo wana haki sawa kabisa ya kuthaminiwa utu wao kama ilivyo kwa Mnyarwanda na Mhabeshi! Yaani, hata kama wamevunja sheria ya uhamiaji - na inawezekana wengi wamefanya hivyo - hilo peke yake haliwafanyi wawe binadamu nusu au siyo watu kama wengine na hivyo hawalindwi na Katiba yetu! Katiba yetu inamlinda kila mtu aliyeko Tanzania!
Ndio maana hili swali linaendelea kusimama, Nyerere alishughulikiaje wahamiaji haramu kutoka Uganda wakati wa chokochoko? Kuna mtu anakumbuka au tuwasaidie hawa wa kizazi kipya somo la historia kidogo maana inaonekana watu wasiojua historia wanaenda kurudia makosa yake!
Tunaweza vipi kukubali serikali ichukue hatua za sheria kwa mfumo wa kibaguzi na udhalilishaji wa utu wa binadamu na bado tunajiita Watanzania?
Mungu atusaidia tusifurahie vitendo kama hivi kwa jina la 'uzalendo'!
MMM

12.-(1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na
kuthaminiwa utu wake.
13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki,
bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya
sheria.
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka
yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo
ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya
watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo
vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa
mujibu wa sheria.