Mzee Mwanakijiji nadhani ktk ule ulimwengu, ulikuwa kama utabiri fulani. Maana January alisema hapo walipokutania ni shimoni na patajazwa maji na hapataonekana milele. Nikashindwa kuelewa hivi anaelewq maana ya neno milele???? Je ni kujitabiria kuwa waliohudhuria hapo wote watakufa very soon kwa sababu wamefanyia kwenye shimo na uwakilishi wake ni kama kaburini kiasa kwamba symbolically they’re all buried?????? Yaani January hakufahamu namna ya kuchagua maneno. Haya tukija na hayo mawe inamaana gani kusema hayataonekana milele? Pia je kwa nini yalitolewa kwa walio hai kwanza badala ya kufuata kiawamu??? Je kutoa kwanza kwa walio hai ambao kwa mujibu wa baba yake January ni watu wazuri hawatakufa baadaye kutoa hizo zawadi wa waliotangulia kufa kwa sababu walikuwa watu wabaya inamaanisha nini??? Kwa nini wasingetoa kufuata awamu? Nikiangalia kwa jicho la kiroho kuna kitu kimefanyika hapo na matokeo yake yataonekana very soon.