Ubungoubungo said:
sideeq wahangaika,kutuletea porojo
kitu moja nakuomba, mwezi utakapoanza
sisahau kunambia,uniungishe magimbi
mihogo na nyanyachungu,bila sahau mbatata
takuuzia bei cheee,ili uchukue vingi
Sikupi wangu muhogo, sikia mwanahizaya
Hupati hata kidogo ,malu`uni usiye haya
wachezewaje kichogo? ondosha wako udhiya!
Ni maajabu ya duniya jamani yatizameni
Hata naye mpigajeki, yuko kwenye disapora
Maneno haambiliki, kazidi wake ukora
Uzayoni naye shabiki, mradi tumbole kufura
Ni maajabu ya duniya jamani yatizameni
Kaja yeye kwetu mjini, kwao tabu zilizidi
Akajiita ni Salimini, kuficha zake hasadi
Ameishia kutukhini, yu ajikomba kwa yahudi
Ni maajabu ya duniya jamani yatizameni
Na Mbona Joni mwenzako, amekuwa ni Athumani
Mashakanini hayuko, humwoni vijaridani
Umebaki u peke yako,kusifiwa maglobuni
Ni maajabu ya duniya jamani yatizameni