Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Majuma mawili yaliyopita kwenye group letu moja kuna mwenzetu mmoja aliandika maneno hayo hapo chini:
"Jamani historia nzima ya Tanganyika ni Sykes and Sykes and Sykes and Sykes."
Nadhani alikuwa kachoka.
Kila ninapoandika historia ya uhuru wa Tanganyika Sykes hawakosekani.
Kwa hakika inachosha katika hali ya kawaida ila pale panapokuwa na kitu kipya.
Mathalan historia ya Abdul Sykes na Earle Seaton.
Msomaji akaja kusoma historia ya Abdul Sykes na Jomo Kenyatta.
Msomaji akaja tena kusoma historia ya Abdul Sykes na Julius Nyerere.
Akili itajiuliza.
Mbona imekuwa hivi?
Sykes kila wakati?
Mimi nikajibu kwanini Sykes wanatajika katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Jibu langu hilo hapo chini:
"Hili la Sykes, Sykes, Sykes lilionekana zamani sana baada ya uhuru.
Kuna mambo yanatokea na huwezi kuyazuia.
John Iliffe professor wa historia kutoka Cambridge University alifundisha historia University of East Africa, Dar-es-Salaam katika miaka ya katikati 1960s.
Alipoanza kutafiti historia ya Tanganyika ikawa kila anapogusa Sykes, Sykes, Sykes.
Ikasadif mmoja wa wanafunzi wake ni Aisha Abdul Sykes akisoma History and Education.
Iliffe akampa Aisha maarufu kwa jina la Daisy seminar assignment aandike historia ya babu yake Kleist Sykes (1894 - 1949).
Illife akawa amefungua Pandora's Box.
Daisy alimletea Iliffe mswada wa kitabu alioandika babu yake Kleist Sykes kabla hajafariki 1949.
Iliffe hakuamini alichokiona katika mswada ule.
Kleist kaanza na Vita Vya Shaka Afrika ya Kusini na jinsi babu zake walivyokimbia vita kuingia Mozambique.
Kleist katika mswada wake anamtaja Chief Mohosh Shangaan na Hermann von Wissmann na jeshi la Wazulu 400 chini ya Chief Mohosh Shangaan waliokuja Germany Ostafrika katika hao akiwa baba zake wawili - Sykes Mbuwane na Ally Katini.
Hili ndilo jeshi lililokuja kupigana na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa kisha na Mangi Meli.
Iliffe anasoma haya mwaka wa 1968.
Mswada huu wa Kleist ulikuwa na thamani kubwa sana katika duru za kisomi duniani.
Iliffe hakutosheka na historia hiyo ya Kleist aliyekufa 1949.
Akataka kujua kama kuna ya zaidi katika historia ya Sykes.
Yalikuwapo.
Sykes Mbuwane na watoto wa Chief Mohosh Shangaan wamepigana ndani ya jeshi la Wajerumani Vita Vya Kwanza Vya Dunia 1914 - 1918 chini ya Kamanda Von Lettow Vorbeck dhidi ya Waingereza.
Iliffe anazidi kushangaa anapoelezwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Wajerumani Germany Ostafrika yaani Germany Constabulary ni Mzulu Chief Mohosh Shangaan aliyeingia Tanganyika na Hermann von Wissmann.
Baba Mamluki watoto wao wako katika regular army.
Hawa ni Schneider Abdillah Plantan na Kleist Abdallah Sykes.
Sykes, Sykes, Sykes.
Iliffe amuuliza Daisy vipi Wazulu na Waingereza katika Tanganyika.
Daisy anampa historia ya babu yake na Dr. Kwegyir Aggrey 1924.
Iliffe anamjua Dr. Aggrey.
Mwafrika wa kwanza kupata Ph D.
Huyu Dr. Aggrey ndiye aliyemshauri Kleist kuunda African Association.
Unapotaka kujua historia ya TANU unatakiwa uanze hapa 1924.
Sykes anaunda African Association na Iliffe anasoma majina ya waasisi jumla yao tisa kati ya hawa sita ni Waislam.
1933 Kleist anaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1929.
Sykes, Sykes, Sykes.
Kila alipogusa Iliffe anasoma Sykes, Sykes, Sykes hadi Dar es Salaam Chamber of Commerce, Dar es Salaam Municipal Council, Maulidi Committee.
Na si maneno yote ni documented.
Abdul na Ally Sykes Burma Infantry, King's African Rifles (KAR) 1942 - 1945.
Abdul Sykes Secretary General Dockworkers Union 1949 na 1950 Secretary TAA, 1951 TAA Act. President na Secretary.
Abdul Sykes na Earle Seaton 1950 kufungua mazungumzo na UNO kupitia TAA Political Subcommittee.
Sykes, Sykes, Sykes.
John Iliffe akawa hoi.
Daisy anamwambia mwalimu wake kuwa baba yake ndiye aliyempokea Julius Nyerere Dar es Salaam 1952 na 1954 ikaundwa TANU...
TANU Card No. 3 Abdul Sykes, No. 2 Ally Sykes No. 1 Julius Kambarage Nyerere."
Yapo mengi.
Kwa nini historia ya Tanganyika imekuwa hivi?
Kwa nini Sykes, Sykes, Sykes?
Tuna haki ya kuuliza:

Kuna mtu anaweza kutupa jibu?
Kwenye Group Mtandaoni mwenzetu kaandika maneno haya baada ya Mkutano Maalum wa CCM Dodoma kuwataja akina Sykes:
"Here comes Sykes again mbona nina hisia kubwa kwamba bila hawa uhuru usingepatikana Tanganyika?
Ni kama mbuzi dume pekee wa kijiji wengine hawafui dafu.
Warabu wanamwita "Tess
Alhara."
Nimesoma nikatingisha kichwa.
Ukweli ni kuwa hata kama Kleist Sykes asingeunda African Association 1929 Tanganyika ingepata uhuru wake.
Ilikuwa kosa kubwa sana kujaribu kuifuta historia ya Sykes katika TANU na uhuru wa Tanganyika.
Leo walioifuta historia hii wanainunua kwa bei ghali sana.