Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mhe. Sylivia Francis Sigula - Mbunge Viti Maalum kupitia kundi la Vijana
Mhe. Sylivia Francis Sigula, Mbunge Viti Maalum kupitia kundi la Vijana tarehe 05 Mei, 2023 alipata nafasi ya kuchangia suala la Tanga Cement na Twiga Cement wakati wa kuwasilishwa kwa hoja ya bajeti ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara iliyosomwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
"Jana nilikwenda kusoma hukumu ya Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara (FCT) katika #SakataLaTwigaCementTangaCement , nikajiuliza kwa nchi ambayo inafuata utawala wa sheria na kuheshimu sheria hivi chombo cha serikali kinapata wapi ujasiri wa kupingana na maamuzi ya mahakama?" - Mhe. Sylivia Francis Sigula, Mbunge Viti Maalum kupitia kundi la Vijana