Synod 2009 na mtizamo wake dhidi ya Afrika

Synod 2009 na mtizamo wake dhidi ya Afrika

Lakini swali linakuja: kwa nini ameenda kusemea huko mbali kote si angesema hapa hapa ndani ya Tz wamsikie? Au mnaonaje wanaJF?
Natumaini ni kwenye mkutano wa Synod Africa, wanaelezea matatizo ya Afrika kwa ujumla wake, ni sehemu muafaka kabisa kuongea alichoongea. Angeyaongelea hapa:

  1. Vyombo vyetu vya habari huenda visingeandika
  2. Angeitwa na "wanausalama" ili akajieleze kwani anahatarisha 'Usalama wa Taifa'
  3. Angepuuzwa na kudaiwa ni 'mdini'
 
Maaskofu endelezeni msimamo huo wa kuongea ukweli...Nawapongeza sana.Angeongelea hapa hakuna ambaye angeguswa, maana wengi wangesema ni sawa tu na waraka wa Kanisa!

This is a very serious matter, na ndo maana hata Tuzo za Ibrahim Mo hazijatolewa kwa yeyote safari hii, ni kwa sababu kizazi hiki cha watawala wetu ni cha mabazazi!
 
Yani Askofu hapo amesema ukweli kabisa natamani ingekuwa rahisi mambo hayo yakarekebishika kama yanavyosemwa.

Lakini swali linakuja: kwa nini ameenda kusemea huko mbali kote si angesema hapa hapa ndani ya Tz wamsikie? Au mnaonaje wanaJF?

Mkuu,
Inaelekea mwenzetu umeingia kwenye hii mada baada ya gazeti la RAIA MWEMA kuitoa hapa. Hii mada ilianzia hapa ndipo RAIA MWEMA nao wakaamua kuimega kwa jamii.

Unasema Askofu kasemea mbali! Nilipoleta hii mada nilifafanua kwamba huu mkutano au Synod ni wa maaskofu wa Africa na Papa ndiye aliyewaita ili kusikia hoja zinazosumbua bara hilo.

Nakujibu kama nilivyomjibu Zitto kwamba kuna dhana kwamba kwa saabu Mtega ni askofu wa Tanzania basi kuna watanzania wanadhani wana hati miliki na alichokisema askofu huyu.

Narudia tena kwamba Nobert Mtega ni askofu wa Kanisa Katoliki. Leo yuko Songea kesho anaweza kuhamishiwa jimbo lolote duniani kulingana na Papa atakavyopenda. Ndivyo Kanisa Katoliki lilivyo. Jimbo la Bulawayo nchini Zimbabwe wamepewa askofu mhindi juzijuzi.

Alichotamka Mtega na maaskofu wenzake ni kuujulisha ulimwengu na hakuna wa kucmhagulia pa kusimama wakati anatamka. Hata hiyo Synod ingefanyika D'Saaam karibu na kituo cha Polisi au Usalama wa Taifa bado angekuwa na nguvu ya kutamka lilelile.

Synod inaisha Jumapili na maaskofu wanarudi makwao wiki ijayo. Nahisi waandishi watamvizia pale Airport kama atakuja na ndege ili wamuulize maswali kuhusu paper yake.

Lakini wakifanya hivyo watakuwa wanakosea maana mmiliki wa Synod ile ni Papa ambaye kwa kweli ndiye anapaswa kuulizwa na kuwajibika kwa lolote linalohitimika kwenye Synod ile. Yeye ndiye aliyeiitisha, yeye ndiye atakayeifunga na nina hakika atashukuru wote walioleta hoja zao na luujulisha ulimwengu jinsi Africa ilivyooza.

Nina imani maaskofu watanzania waliokohuko watamueleza jinsi mlivyompigia JK simu eti taasisi za dinin sasa zianze kukaa na kujadili na wanasiasa.

Sasa mkuu wa taasisi ya dini ya Kikatoliki ni Papa huyohuyo. Ndiye amebariki Synod na ndiye anayebariki hizo nyaraka mnazozipigia kelele kila siku. Nadhani kama mnataka kukaa basi kelele zianze kupigwa kumshinikiza Papa akemee maaskofu wake wasitoe nyaraka au wasitwange makala kwenye synod kama alivyofanya Mtega wa Songea na wengine wote waliotoa hoja kali huko Vatican.

Hivyo unaona ile dhana kwamba "tutakaa na taasisi za dini" ni dhana finyu kwa sababu ni nani atakayekaa na Papa kumuambia watu wako wanatoa nyaraka ovyoovyo?

Mimi naamimi hakuna atakkayefanya hivyo. Kwa nini naamimi hivyo? Ni kwa sababu kama mmedhamiria hivyo basi inabidi mjivue aibu ya kuonekana kwamba kuna nchi iko nyuma ki-exposure kiasi hawajui kwamba nyaraka za Kanisa Katoliki zina karne nyingi zikitoka. Kwamba nchi hiyo inaitwa Tanzania leo wamemuendea Papa kuzungumza nyaraka, na kwamba hilo jambo kwao ni geni kama vile "kipofu ameona mwezi".

Inabidi dunia iwashangae kwani nyaraka hizo na hotuba kama hizi wakomunisti waliinua mikono kushindwa kuzizuia hadi ulipoanguka.

Eti leo watanzania ndiyo wanaibuka na hoja kuhusu matamshi ya wakatoliki hawa! Kwa kweli dunia inabidi iwashangae tu na kuwauliza mlikuwa wapi kuuliza haya huko nyuma kiasi kwamba hakuna hoja mnayoleta ambayo haikuwahi kujibiwa na Kanisa Katoliki.

Hivyo Askofu Nobert Mtega na maaskofu wenzake Africa walioko huko Vatican wanazidi kuonyesha ni mzigo gani mnaotakiwa kujitwisha kama kweli mmeamua kusimamisha hoja za Kanisa Katoliki ambazo mataifa makubwa kama Marekani wameshindwa na wameamua kuchgua njia ya kuzipuuza kuliko kupambana nazo.
 
Back
Top Bottom