T.I amezichapa na Mayweather

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Bondia Floyd Mayweather ameripotiwa kuzipiga na msanii wa miondoko ya rap T.I katika mgahawa mmoja mjini Las Vegas, Marekani. Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, T.I aliamua'kulianzisha' na Floyd Mayweather ambaye kazi yake na fani yake ni 'kurusha mikono'.

Tovuti hiyo ambayo huandika habari za udaku za'macelebrity', imesema mtafaruku huo ulitokea nje ya mgahawa wa Fatburger, ambapo T.I alimfuata bondia huyo hodari duniani na kuanza kumrushia masumbwi kabla ya walinzi waokuingilia kati na kuwatenganisha.

Polisi wa Las Vegas wamethibitisha kutokea kwa kasheshe hiyo, ingawa hakuna sababu hasa iliyotolewa ya kuzuka kwa ugomvi huo.
 
Kama T.I ndiye alimvamia tu Mayweather, basi hakuna shaka ni T.I hapo anatafuta KUmake headlines.........coz amesahaulika sana.
 
Huyo T.I si yule ambaye yeye na my wife wake mzuri yeye daah huyu jamaa bhana hamnazo kbs.
 
Kama T.I ndiye alimvamia tu Mayweather, basi hakuna shaka ni T.I hapo anatafuta KUmake headlines.........coz amesahaulika sana.

Haaaahaa anaitwa Clifford Joseph Harris, Jr. a.k.a T.I ukifiatilia mbilinge zake basi utagundua hana muda wa kutafuta kick ili a-make headline uyu ni mjelajela haswaaa hapo alizinguliw na Mayweather maana ndio ana tabia za kuongea kama mzee Yusuph na hapo bado halijaisha.
 
Seriously, sidhani kama TIP anaweza kuzipiga na Money May hata kama ni street fight.


Ingia hapo kwa habari zaidi.
 
Wapigane tu tujue mbabe nani, wivu unatesa sana
 
Ila TMT(siyo Hii ya kina Joti na Lulu Tanzania Movie Talent) Hii ni The Money Team Jamaa wana mipunga kinomaaa.
 
kweli papuchii kitu ingine!haya wazabuanee tu mpaka kieleweke
 
TMT wasijaribu vita na Tip hasa hii ya hood ndio maana kamwambia "u fight on the ring but i fight in street" mwenzie jela kama Maisha club tu haaaahaa nimemsikiliza 50cent anamwambia Floyd aache vita na uyu OG hasa ukifuatilia mapenzi yake na bunduki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…