Mazembe wanacheza soka safi sana na pia wana vijana wengi wa Kongo wanaoichezea. Niliangalia zile mechi za fainali na kwa kweli kiwango cha soka cha Mazembe kilikuwa juu sana kushinda cha Esperance kiasi cha kwamba inabidi mtu ujiulize Esperance waliwatoaje Al Ahly pamoja na goli la mkono.
Ushindi huu wa Mazembe umerudisha changamoto kidogo katika soka la Afrika maana siku hizi hii michuano ya CAF imekuwa ni kama vile ni michuano ya nchi za Afrika Kaskazini na kidogo Magharibi.
Natamani na sisi Bongo tupate Mazembe yetu, atokee Moise Katumbi Chapwe kitu ambacho akina Mo Dewji na Bakhressa wamejitahidi kujaribu, awekeze fedha maradufu katika soka. Ingependeza pia kama Mazembe yetu isiwe based Dar es Salaam, Tanga wala Morogoro. Ingetokea mitaa ya Mwanza au Shinyanga kwenye timu zenye genuine local fans ingependeza zaidi.
Dawa ya kukuza mpira wa Tanzania ni kupata mshindani kama huyu ambaye ataziua Simba na Yanga